bongo dili
JF-Expert Member
- Feb 13, 2015
- 12,345
- 25,322
Maisha ya vijana wengi below 35MDOGO WAKO:Kaka naomba 600,000/= Kwa ajiri ya ada . Walisema nisipolipa hawatanipokea kabisa .
BABA MWENYE NYUMBA:Missed Calls 83 na Ujumbe: Leo nakupatia Nafasi ya Mwisho
BINTI WA JIRANI: Nafikiri Nina Ujauzito wako .
RAFIKI YAKO: Kaka ,fedha yangu lini unanipa? Ni mwisho wa mwezi Sasa ulioniahidi mara ya Mwisho.
WAZAZI: Tunakufa Kwa Njaa kijana wetu .
Hatuna chochote , Tusaidie .
MCHUMBA: Sawa tu,naona umeanza kunionyesha dharau kabla hata hatujaoana. Endelea tu na Hao Malaya wako. Usinitafute mimi. Pepo wewe!
EX: Ulinitumia tu ,Mbwa wewe. Utakufa Kifo kibaya sana.
M PESA:Unakumbushwa kulipa Mkopo wako wa SONGESHA kiasi Cha Tsh. 93,200/=
TALA: Tunajua unapoishi , Wewe ni Mdaiwa sugu Sasa na tutakukamata tu.
MSHAHARA :Kiasi Cha Tsh. 187,000 kimewekwa kwenye akaunti Yako inayoishia 3214.
Hii inatosha kuufunga huu mjadalaKupanga ni kuchagua.
Wakati mwingine kubali lawama mpaka pale utakaposimama vizuri. Dhamira yako ikiwa safi mengine yote ni madogo na usijali lawama, kuchekwa wala kusemwa na watu. Na umakinikie mambo ya muhimu tu kipindi hiki (hayo ya wachumba na ma ex hayana nafasi kipindi hiki)
Vinginevyo utachanganyikiwa!
Ahsante Sana Mkuu kwa Mwongozo mzuri barikiwaKupanga ni kuchagua.
Wakati mwingine kubali lawama mpaka pale utakaposimama vizuri. Dhamira yako ikiwa safi mengine yote ni madogo na usijali lawama, kuchekwa wala kusemwa na watu. Na umakinikie mambo ya muhimu tu kipindi hiki (hayo ya wachumba, wapenzi na ma ex hayana nafasi kipindi hiki)
Tuliotoka familia za kawaida wengi wetu tumekipitia kipindi hiki. Hatimaye kitapita na siku moja Ma mkubwa anakupigia anahitaji 50K unatabasamu tu huyo unamrushia 200K. Mibaraka kama yote unaihisi mpaka kwenye simu....
Kutokata tamaa, kujikubali, kutojilinganisha na wengine, kuwa karibu na Mungu (kwa waaminio) na kuacha shobo zisizo na maana ni baadhi ya mambo ya muhimu sana kuzingatia katika kipindi hiki.