Haya ndio madhara ya kufanyakazi na wanawake warembo..!!

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,331
33,141
Kufanya kazi sehemu moja au kuzungumza na mwanamke mwenye mvuto kunaweza kumfanya mwanaume apoteze
umakini wake, hii ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Jarida la New Study.

attachment.php



Wanaume wanaofanya kazi kwenye makampuni yenye ‘visura' wengi, ufanisi wao ni wa kiwango cha chini kulinganisha na wasiokuwa kwenye mazingira hayo, sehemu ya utafiti inaeleza.


Sababu ya kuwepo kwa hali hiyo ni uchunguzi kubaini kuwa, akili za wanaume wenye kuvutwa na sura wakati wakifanya mambo hukabiliwa na mgongano wa hisia mbili, za kazi na mapenzi.


Kuwepo kwa vitu hivyo viwili kwa wakati mmoja ndani ya akili ya mwanaume, utafiti wa kitaalamu uliochapishwa na Jarida la Journal of Experimental and Social Psychology, umebaini kuwa mwanaume ana hatari kubwa ya kufanya vibaya kikazi kwa sababu wakati akifanya kazi yake atakuwa pia akifanya kazi ya kushawishi au kuimarisha hadhi yake mbele ya mwanamke aliyemvutia.


Ukichunguza, utabaini kuwa, tabia za wanaume (si wote) hubadilika pindi wanapokuwa mbele ya wanawake warembo, hii ikiwa na maana kuwa, kama mwanaume ni mwenye maneno mengi na mpayukaji kwa mfano, hujikuta akilazimika kushusha sauti yake, kuongea kwa unyeyekevu na busara lengo ni kutaka kumvutia msichana.


Hali hiyo inapojitokeza ndiyo inayotajwa kudhorotesha umakini wa mtu na kumfanya afanye kazi zake kama ‘msanii' anayeigiza na hivyo kuathiri utendakazi wake.


Wakati nafanya uchunguzi wangu kwa kuoanisha na ule wa watafiti wengine wa kimatafa ukiwemo wa Dr. Irva Hertz-Picciotto, kutoka Chuo cha Carifonia Marekani, nilibaini pia viashiria vingine vya ufanisi duni wa kimasomo kutoka shule za jinsia moja na zile za mchanganyiko, ambapo uchunguzi unaonyesha kuwa wavulana wanaosoma shule huku wakiwa na uhusiano wa karibu na wasichana warembo huathirika kisaikolojia.


Hata hivyo, upo ushahidi mwingine kwamba kiwango cha kufaulu cha shule mchanganyiko kuwa chini kuliko wa shule za wasichana au wavulana peke yao, katika kulithibitisha hili mazingira ya shule na malezi yanazingatiwa.

Katika kumbukumbu iliyowashangaza wanasaikolojia na watafiti wa chuo cha Radboud cha Netherland ni pale mmoja wao aliposhindwa

kukumbuka na kumwelekeza msichana mwenye mvuto aliyekutanishwa naye ramani ya eneo analoishi, jambo ambalo wenzake walisema lilitokea kwa sababu alikuwa kwenye mhemko wa hisia za kimapenzi.

Utafiti wao huo ulihusisha pia watu wengine na matokeo yalionyesha udhaifu mwingi kwa wanaume, huku wanawake wakiwa na kiwango kidogo cha kuathirika kwa kukutanishwa na wavulana wenye mvuto.

Ingawa si jambo la hatari sana kufikia hatua ya kulitangaza moja kwa moja kuwa ushirikishwaji wa wanaume na wanawake warembo katika ofisi, masomo na kazi mbali mbali una madhara lakini kitaalamu imebainika kuwa ni vema kundi linaloathirika ambalo ni sawa na asilimia 19 ya wanaume wote likapewa elimu ili kupunguza zaidi madhara ya kisaikolojia.


Changamoto hii, inamtaka kila mwanaume kupima mwenyewe mhemko wa nguvu za warembo kwa kujiuliza maswali ambayo yatamuwezesha kujua kama yuko kwenye kundi la wanaume wanaoweza kuathirika kisaikolojia kwa kufanya kazi na wanawake wenye mvuto au la! Lengo likiwa ni kuchukua hatua za kujikinga na madhara ya kisaikolojia.


Mwanasaikolojia Dr George Fieldman anakumbusha kitu muhimu alichokipa jina la ‘Reproductively Focused' kuwa ndiyo sumu kali inayowadhuru wanaume wengi wanapokutana au kukutanishwa na wanawake wenye mvuto. Inaelezwa kuwa wanaume wanaovamiwa haraka na hisia za kimapenzi ndiyo wanaoweza kupata madhara ninayoyaeleza kwa kiwango kikubwa.


Itaendelea wiki ijayo.
 

Attachments

  • mwanamke mwenye mvutooooo.jpg
    mwanamke mwenye mvutooooo.jpg
    38.7 KB · Views: 1,178
Kujiendekeza tu! Afu hiyo picha inaendana na somo kweli? Wazungu hawavai kwa heshima hivyo bana, mapaja nje, samtmz hadi kota liko nje wala no time ya kupiga chabo kitu ambacho umekizoea
 
Kujiendekeza tu! Afu hiyo picha inaendana na somo kweli? Wazungu hawavai kwa heshima hivyo bana, mapaja nje, samtmz hadi kota liko nje wala no time ya kupiga chabo kitu ambacho umekizoea
Umesema ukweli Wazungu nguo zao zipo uchi tu hawana hata aibu ukifanya nahawa watu weupe inataka uwe na moyo ama sivyo kazi itakushinda tu utafukuzwa kazi.
 
Jamani mzizimkavu unataka sie warembo tuishie kugombea U-miss tu kwa kuwa hatustahili kukaa na nyie maofisini.
 
ahaaaa kumbeee! i wish ningekuwa na boss wa kiume angenikomaje?
 
Back
Top Bottom