MWENDAKULIMA
JF-Expert Member
- Jul 17, 2009
- 951
- 358
Jocelyne. Hao Makoma unawatolea mfano hawajapona kwenye tuhuma za mtoa mada.Kama nao wanatumia huo mfumo unaolalamikiwa pia wana la kujibu..si ndiyo?kwa hiyo tusitumie mapungufu ya watu wengine kuhalalisha uchafu wetu.kumbuka huuo uwanja wanalipia siyo bure, kuna spika na vipaza sauti wanalipia, kama uwanjani hakuwa umeme kuna mafuta ya jenereta, kuna mapambo ya uwanja yananunuliwa.
halafu kwa soko gani Tanzania la kuza kanda hadi aweze kurudisha gharama zote,
zamani ni zamani, zamani zipi unazoziongelea wewe za pontio pilato au?mbona kina makoma wanakuja huku mnalipa viingilio na wenyewe si wanaimba gospel? kwa ninin wasitumbuize bure.
binadamu anabadilika kutokana na mazingira yake. ndo maana sasa hivi wanapiga modern gospel ili hata wale waliokuwa hawapendi kusikiliza wasikilize.
Pamoja na kwamba wanaimba injili, lakini unatakiwa ujue ndio njia yao ya kuendesha maisha yao kwa hiyo lazima kuwe na kipato, kwa sababu kuna gharama ametumia mpaka kufika huko, nauli , vyombo kurekodi, kulipa waimbaji wanaomsaidia,
Kwenye biblia sikumbuki kitabu nikikumbuka nitakuambia , inasema kila mtu atakula mahali pake pa kazi, yani kutokana na kazi yake anatakiwa ale, ikiwa ni pamoja na hayo mapato.
ndo maaa hata kwa watumishi wa Mungu ni lazima tutoe sadaka, zaka ili na wenyewe waendeshe maisha yao.
Jamani sasa wasipo kusanya huo mshiko huo uwanja wa ccm kirumba wataukodi na nini?
Na hivyo vifaa vya muzic watavitoa wapi?
Na wao watakula muzic tu bila ugali?
any way ni mawazo yako endeleeni kujadili na kuchangia mada,
Badala tujiulize Kagoda atafungwa lini?,
mnaleta mambo ya watu Huyo mdada anatoza pesa kama yeye na wewe pia ukianzisha bureeeee its ok kuna watakao kuja na wapo ambao hawatakuja.
Mkuu tupo ukuraha mmoja, jamaa ameezea vizuri kabisa kuwa watu watumia mgongo wa injili kujinufaisha, hii hakuna tofauti na kuwapumbaza watu.Mkuu mwendapole,out of all huyu (post # 17) katoa majibu mujarab. Lakini hilo la kuwa na VIP kwenye tamasha la dini mimi sijaridhika nalo.dini inatambua uwepo wa VIP?..mbona wanalikwepa?
Kwanini wachague ama waende kwenye uwanja huo wa kulipia?? kuna viwanja vingapi vya wazi mitaani ambavyo ndio huwa vinatumiwa kila siku kwa mambo haya ya dini?? Wahubiri wanavitumia kila siku na hapo karibu huo uwanja wa CCM kirumba kuna kiwanja kikubwa sana tu cha wazi. Kwani wanakwaya wengine hivyo vifaa wao wanavitoa wapi..?? na hayo ya umeme na vitu vingine kwani kwa wanakwaya/wahubiri wao hawavitumii hivyo..?? kama hakuna soko la kanda zao kwanini wasifanye shughuli nyingine na dini ikawa ni sehemu ya huduma tu kama inavyotakiwa iwe..?? inamaana unakubaliana na wazo la kuifanya dini kuwa biashara..??kumbuka huuo uwanja wanalipia siyo bure, kuna spika na vipaza sauti wanalipia, kama uwanjani hakuwa umeme kuna mafuta ya jenereta, kuna mapambo ya uwanja yananunuliwa.
halafu kwa soko gani Tanzania la kuza kanda hadi aweze kurudisha gharama zote,
zamani ni zamani, zamani zipi unazoziongelea wewe za pontio pilato au?mbona kina makoma wanakuja huku mnalipa viingilio na wenyewe si wanaimba gospel? kwa ninin wasitumbuize bure.
binadamu anabadilika kutokana na mazingira yake. ndo maana sasa hivi wanapiga modern gospel ili hata wale waliokuwa hawapendi kusikiliza wasikilize.
Nimekuwa nikisilikiza radio maria na kwa siku kadhaa kumekuwa na tangazo la tamasha ambalo limepangwa kufanyika mkoani mwanza na huyu Msanii wa nyimbo za injili Flora Mbasha akishikilikiana na wengine. Ni tamasha linalohusu uzinduzi wa album yake pamoja na video CD. Tamasha litafanyika katika uwanja wa CCM kirumba na kitu kinachonishangaza ni kuwa kutakuwa na kiingilio katika tamasha hili la nyimbo za injili...!! kana kwamba hiyo haitoshi viingilio vimegawanywa katika makundi mawili, kawaida ni sh 2000 na VIP ni sh 5000.
Wakuu kadri siku zinavyokwenda hii inaonekana kama ni kitu ya kawaida kabisa kwa hawa wasanii wa nyimbo za injili kufanya matamasha na kuweka viingilio.
swali ni kwamba je? Inamaana kuna VIP kwenye dini...????? na inamaana watu inabidi sasa watambue kuwa injili sasa haipatikani bure..?? Je hayo ndio maagizo ya maandiko matakatifu..?? mbona dini sasa imevamiwa..?? na hawa wasanii wenyewe wanavyofanya hizo performance zao siku hizi hakuna tofauti kabisa na hawa wanamuziki wa lingara/boringo kutoka congo ama FM academia, je hii ni sawa kwa nyimbo za injili?? naomba mnisaidie kwani nina maswali mengi kuliko majibu manake hawa wanajiita wasanii wa nyimbo za injili wa siku hizi ni balaa, especially huyu Lady amekuwa so deep in business kabisa katika dini, you can tell it quite easily.
I miss those moments enzi za Mwanza town kwaya, Ulyankulu Tabora, Upendo Kwaya na pia kulikuwa na wenzetu kule Arusha walikuwa wanaimba vizuri sana .
Nisaidieni maoni yenu, Rev Kishoka, Exaud, Mchungaji na wengine woote nawasubiria....