Haya matamasha ya dini yanatupeleka wapi...??? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Haya matamasha ya dini yanatupeleka wapi...???

Discussion in 'Entertainment' started by Mwenda_Pole, Jul 22, 2009.

 1. Mwenda_Pole

  Mwenda_Pole JF-Expert Member

  #1
  Jul 22, 2009
  Joined: Jul 5, 2008
  Messages: 260
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Nimekuwa nikisilikiza radio maria na kwa siku kadhaa kumekuwa na tangazo la tamasha ambalo limepangwa kufanyika mkoani mwanza na huyu Msanii wa nyimbo za injili Flora Mbasha akishikilikiana na wengine. Ni tamasha linalohusu uzinduzi wa album yake pamoja na video CD. Tamasha litafanyika katika uwanja wa CCM kirumba na kitu kinachonishangaza ni kuwa kutakuwa na kiingilio katika tamasha hili la nyimbo za injili...!! kana kwamba hiyo haitoshi viingilio vimegawanywa katika makundi mawili, kawaida ni sh 2000 na VIP ni sh 5000.
  Wakuu kadri siku zinavyokwenda hii inaonekana kama ni kitu ya kawaida kabisa kwa hawa wasanii wa nyimbo za injili kufanya matamasha na kuweka viingilio.
  swali ni kwamba je? Inamaana kuna VIP kwenye dini...????? na inamaana watu inabidi sasa watambue kuwa injili sasa haipatikani bure..?? Je hayo ndio maagizo ya maandiko matakatifu..?? mbona dini sasa imevamiwa..?? na hawa wasanii wenyewe wanavyofanya hizo performance zao siku hizi hakuna tofauti kabisa na hawa wanamuziki wa lingara/boringo kutoka congo ama FM academia, je hii ni sawa kwa nyimbo za injili?? naomba mnisaidie kwani nina maswali mengi kuliko majibu manake hawa wanajiita wasanii wa nyimbo za injili wa siku hizi ni balaa, especially huyu Lady amekuwa so deep in business kabisa katika dini, you can tell it quite easily.
  I miss those moments enzi za Mwanza town kwaya, Ulyankulu Tabora, Upendo Kwaya na pia kulikuwa na wenzetu kule Arusha walikuwa wanaimba vizuri sana .
  Nisaidieni maoni yenu, Rev Kishoka, Exaud, Mchungaji na wengine woote nawasubiria....
   
  Last edited: Jul 23, 2009
 2. Mwenda_Pole

  Mwenda_Pole JF-Expert Member

  #2
  Jul 23, 2009
  Joined: Jul 5, 2008
  Messages: 260
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hii makitu inapotupeleka bado sijapaelewa..
   
 3. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #3
  Jul 23, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Pamoja na kwamba wanaimba injili, lakini unatakiwa ujue ndio njia yao ya kuendesha maisha yao kwa hiyo lazima kuwe na kipato, kwa sababu kuna gharama ametumia mpaka kufika huko, nauli , vyombo kurekodi, kulipa waimbaji wanaomsaidia,
  Kwenye biblia sikumbuki kitabu nikikumbuka nitakuambia , inasema kila mtu atakula mahali pake pa kazi, yani kutokana na kazi yake anatakiwa ale, ikiwa ni pamoja na hayo mapato.
  ndo maaa hata kwa watumishi wa Mungu ni lazima tutoe sadaka, zaka ili na wenyewe waendeshe maisha yao.
   
 4. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #4
  Jul 23, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mbona hulalamiki suala la sadaka na zake ambalo nalo huendana na kipato?
   
 5. B

  Bull JF-Expert Member

  #5
  Jul 23, 2009
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu

  ukifikiria mambo mengi kwenye hii dini mwishowe utaiacha/convert to..!! bora fumba macho endelea kufuatafuata. inasikitisha sana!!!
   
 6. P

  Preacher JF-Expert Member

  #6
  Jul 23, 2009
  Joined: Aug 25, 2008
  Messages: 328
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  pia ikumbukwe kuwa muziki asili yake ni mbinguni - malaika wanamwimbia Mungu usiku na mchana - adui ibilisi na shetani alikuwa anaitwa lucifer - aliumbwa kwa ustadi sana kiasi ambacho akitembea mwilini mwake vinanda vililia - na hii ni kuonyesha alikuwa kiongozi wa sifa kabla hajamwasi Mungu na kuwa shetani - soma kitabu cha Biblia - ufunuo wa Yohana 12:7 -9 ambapo Lucifa alimwasi Mungu akafanya vita na malaika Mikael naye akatupwa duniani - alipotupwa duniani bado ingawaje alinyang'anywa utukufu wote aliopewa na Mungu - bado anakumbukia ujuzi wake wa sifa na ndio anavuvia music isiyompendeza Mungu - hivyo kipawa cha sifa kimerudi kwa watu wa Mungu - ndio maana wanaimba na kusifu - MATAMASHA ni mpangilio wa kusifu - na CDs - Albums zinapotengenezwa na kusambazwa - ndio zinavyoendelea kupigwa majumbani na sehemu mbali mbali - na katika hizo mafundisho yanatolewa ndani ya jumbe na Jina la Bwana linainuliwa. Kiingilio lazima kiwepo - hivi nani akuandalie sehemu ya kwenda kusikiliza, au kucheza au kushiriki kitu chochote free of charge?? huyo anaendaa anatumia fedha na unapotozwa kiingilio ndio fedha za kutengenezea tamasha - mwimbaji anakula madhabahuni -na ndio maana unaweza kuona Mungu anawagusa watu wanatoa hata fedha za ziada (kutunza) wakati wa uimbaji - MTUMIKIE MUNGU KWA MALI ZAKO; WEKEZA KATIKA UFALME WA MUNGU na KATAA KUWEKEZA KWENYE UFALME WA GIZA - na MUNGU ATAKUBARIKI SANA - CHANGIA MATAMASHA YA NYIMBO ZA INJILI - watu waokolewe, wapate message za Kimungu, wengine wainuliwe na kuburudishwa mioyo yao katika BWANA
  amen!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 7. F

  FM JF-Expert Member

  #7
  Jul 23, 2009
  Joined: Jul 2, 2009
  Messages: 202
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hizo kwaya ulikuwa unazipata bure?
   
 8. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #8
  Jul 23, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,565
  Likes Received: 3,861
  Trophy Points: 280
  watu wakishachoka na ufisadi kwa kila kitu ufisadi!

  yaani mtu afanye mazoezi, atafute mwalimu, arekodi nyimbo(aende kulipia studio-hamna ya bure), atafute sare then aje alete bure!

  hainiingii akilini! wanakula wapi? kama unaweza kuonyesha mfano wa kitu chochote wanachotoa pesa watu wewe ukafanya bure itakuwa vizuri sana mkuu!
   
 9. BinMgen

  BinMgen JF-Expert Member

  #9
  Jul 23, 2009
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 1,816
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  .
  kwa hiyo tufuate tu! Bila kufikiri?

  Achana nayo kama! Kama inakuchanganya. Wengi wameshatupiliambali. Dini ya kufuata mkumbo.
   
 10. Mwenda_Pole

  Mwenda_Pole JF-Expert Member

  #10
  Jul 23, 2009
  Joined: Jul 5, 2008
  Messages: 260
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Point yangu ipo kwenye namna wanavyoendesha hizi shughuli zao.Yaani imekuwa hakuna tofauti na wanaume TMK. nilikuwa nasikiliza radioni pamoja na kununua kanda zao na pia katika mahubiri lakini sio kwa kwenda kutoa kiingilio uwanjani ili kuona show ya kwaya.wanaweza kurudisha pesa zao kwa njia ya kuuza kanda na sadaka kwenye mahubiri lakini sio kuweka mlinzi getini na kukusanya kiingilio
   
 11. Mwenda_Pole

  Mwenda_Pole JF-Expert Member

  #11
  Jul 23, 2009
  Joined: Jul 5, 2008
  Messages: 260
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mfano ni simple tu mzee.. kwani wale wa zamani wao walikuwa wanarudisha vipi hela zao za kurekodia..?? ninachopinga mimi ni ule utaratibu wao mzima wa kuweka mlinzi getini na kuzuia mpaka utoe kiingilio. Hii inafanya kuwa hakuna tofauti na bongo flava. Kwanini wasifungue tu geti na watangaze tu kuwa CDs zitauzwa uwanjani kwa wale wataopenda? na pia wanaweza kukusanya sadaka tu mwisho wa onyesho. vinginevyo itamaanish kuwa wale masikini wasio na hiyo 2000 hawana haki ya kupata neno la mungu.
  najua wanafanyakazi kubwa lakini kwa kuweka viingilio na walinzi getini kwa ajili ya kukusanya fedha mazee this is too far..
   
 12. Mwenda_Pole

  Mwenda_Pole JF-Expert Member

  #12
  Jul 23, 2009
  Joined: Jul 5, 2008
  Messages: 260
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Yeah ninaelewa shughuli zoote hizo ulizosema za maandalizi na hatimaye kutoa album but ninachopinga mimi ni utaratibu mzima wanautumia.vinginevyo tutahalalisha kila kitu kifanyike kwa mgongo wa dini kwa sababu tu ndio kazi yao.
  wanaweza kutumia njingine ya kujipatia kipato na at the same time watoe haki ya kila mtu kupata neno ya mungu bila kujali yeye ni VIP ama la.
  tazama majibu yangu kwa watu wengine chini.. pia kwa ufafanuzi zaidi
   
 13. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #13
  Jul 23, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Watanzania tutakapofika mahali pa kujua kulipia services ndipo maendeleo yatapatikana.
  Lakini kama ulivyoainisha hapo juu BURE imekithiri kila mahali.
  Hata serikali imefikia mahali kama haijaomba omba BURE toka ulaya inaona mabo hayaendi. madhehebu hata kujenga jengo la mita 7x5 lazima ulaya walete pesa.
  Hii imedumaza mawazo yetu na kuleta ujinga kwetu.
  Tujifunze kutoa japo kidogo kwa ajili ya huduma za wengine. Baa tunakwenda kunywa na kugawa bia tunavyopenda, makanisa na kwaya tupate BURE wapi kwa wapi?
  We angalia hata kusaidia JF watu maswali mengi! sababu kuzoea BURE.
   
 14. Mwenda_Pole

  Mwenda_Pole JF-Expert Member

  #14
  Jul 23, 2009
  Joined: Jul 5, 2008
  Messages: 260
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Wanawezaje kulipia hizo bia bar kama wamezoea bure..?? point hapa inabidi utambue na kutofautisha Dini/ Mashirika ya kidini na makampuni ya kibiashara. Mtoa maada hapingi kuuzwa kwa Cds za nyimbo za dini wala kupigwa nyimbo hizo redioni, kinachopingwa hapa ni Kufanya matamasha kama bendi za muziki wa dansi na kuweka mabaunsa milangoni
   
 15. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #15
  Jul 23, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Ni mfumo wa soko huria umevamia mpaka kwenye dini, hamna la ajabu.

  Ukiwastukia anza mbele, uzuri wa soko huria hawana monopoly katika biashara ya kutoa maliwazo ya kisakolojia kuhusu mbingu ambayo haijulikani kama ipo au la.
   
 16. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #16
  Jul 23, 2009
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Wanaoimba nyimbo za Injili wanajulikana kama "Wanamuziki wa Injili". Kumbe kwanza ni wanamuziki (siyo wanakwaya). Pili, ni wanamuziki wa Injili (Injili ndiyo mada yao). Wanamuziki hawa hawatofautiani kimsingi na wanamuziki wengine wa duniani ukiondoa mada. Wale wa duniani wanaimba ya duniani: mapenzi, siasa, nk. Hawa wa Injili wanaimba mambo ya Mungu.

  Lengo la wanamuziki wote (wa kidunia na wale wa Injili) ni (a) Kutoa ujumbe kwa watu, (b) Kuburudisha. Kama wanamuziki wa duniani wanachaji kwa nini wale wa Injili wasichaji viingilio? Mada ya nyimbo zao kuwa ni Injili si hoja. Wanaopewa hiyo huduma ya ujumbe na burudani lazima waigharamie. Nani aliwaambia wanamuziki wanajitolea? Watakula wapi? Kwao hiyo ndiyo ajira (yaani muziki), ndiyo kazi yao ya kuingiza kipato. Hawa si wachungaji ambao wanakula kwa sadaka za waamini. Hawa professional yao ni muziki huwezi kusema wategemee tu hisani ya wahudumiwa. Je, wasipowapa? Au wakiwapa kidogo sana, wafanyaje? Mi naona ni haki na sawa kabisa wadai viingilio.
   
 17. m

  mathew2 JF-Expert Member

  #17
  Jul 24, 2009
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 462
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 45
  Wanamuziki wa injili ni wafanyabiashara kama wafanyabiashara wengine tu. Ila opportunity wameipata kwenye hizo nyimbo- zina soko. Usidanganywe kwa maneno ya kidini wanayoyatumia wanapojinadi, wanachotafuta ni PESA ndo maana kuna Kiingilio na si sadaka. Ninachoelewa mie kama injili ingekuwa ndicho kipaumbele basi kiingilio kisingewekwa mbele na watu wangetoa kwa kuguswa na hilo neno linalotajwa pale. Lakini mbaya zaidi nikuwa baadhi ya hao wanamuziki wa injili hutafuta wachezaji toka popote pale ili kufanikisha show zao kwa kuwalipa kitu kidogo!
  Mungu atuhurumie sana. Hilo linanikumbusha pale Yesu alipoingia Hekaluni akakuta wale wafanyabiashara AKAZIPINDUA MEZA ZAO NA KUWACHARAZA VIBOKO akiwaambia NYUMBA YANGU SI PANGO LA WANYANG'ANYI. Naona inakuja tena kwa njia ya nyimbo. Mungu atupe hekima ya ku-balance mambo kwani inavyokuja sasa lazima tujiulize YANATUPELEKA WAPI????
   
 18. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #18
  Jul 24, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  kumbuka huuo uwanja wanalipia siyo bure, kuna spika na vipaza sauti wanalipia, kama uwanjani hakuwa umeme kuna mafuta ya jenereta, kuna mapambo ya uwanja yananunuliwa.
  halafu kwa soko gani Tanzania la kuza kanda hadi aweze kurudisha gharama zote,

  zamani ni zamani, zamani zipi unazoziongelea wewe za pontio pilato au?mbona kina makoma wanakuja huku mnalipa viingilio na wenyewe si wanaimba gospel? kwa ninin wasitumbuize bure.

  binadamu anabadilika kutokana na mazingira yake. ndo maana sasa hivi wanapiga modern gospel ili hata wale waliokuwa hawapendi kusikiliza wasikilize.
   
 19. Mwenda_Pole

  Mwenda_Pole JF-Expert Member

  #19
  Jul 24, 2009
  Joined: Jul 5, 2008
  Messages: 260
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Nashukuru kwa mchango wako, naona wewe umenielewa vyema swali langu
  na maana ya kuuliza hivyo. wachangiaji wengine naona wanashindwa kutambua ni kwa namna gani dini ilivyo vamiwa na kugeuzwa maana yake halisi kwa kigezo tu cha mabadiliko ya mfumo wa kimaisha.
   
 20. M

  MWENDAKULIMA JF-Expert Member

  #20
  Jul 24, 2009
  Joined: Jul 17, 2009
  Messages: 961
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Mkuu mwendapole,out of all huyu (post # 17) katoa majibu mujarab. Lakini hilo la kuwa na VIP kwenye tamasha la dini mimi sijaridhika nalo.dini inatambua uwepo wa VIP?..mbona wanalikwepa?
   
Loading...