Haya mapenzi jamani

g click

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2012
Posts
2,427
Reaction score
511
Polisi mjini Nairobi wanachunguza kisa cha mwanafunzi mmoja wa kidato cha tatu anayedaiwa kumuua mwenzake kwa kumdunga kisu.

Tukio hilo lilifanyika siku ya Jumatano mtaani Komarock viungani mwa mji wa Nairobi ambapo wawili hao inaarifiwa waLikuwa wanazozania msichana mmoja mpenzi wa mmoja wa vijana hao.


Maafisa hao wanamtafuta mshukiwa ambaye anadaiwa kumdunga Geoffery Onyango mwenye umri miaka 16 kisu kifuani alipokuwa akirejea nyumbani kutoka shuleni.

Wenzake wanasema kuwa wawili hao walikuwa na ugomvi kati yao kabla Onyango kudungwa kisu.

Hatimaye alikimbizwa hospitalini lakini alifariki akipokea matibabu.

Mkuu wa Polisi mjini Nairobi alisema kuwa bado wanaendelea kumtafuta mshukiwa huyo.

SOURCE: BBC
 
Kijana mdogo wa miaka kumi na sita anadiriki kuingia kwenye ugomvi wa mapenzi, ameshapoteza maisha yake kirahisi rahisi, kweli majanga
 
Ndo vijana natamani sana nirudi hapa Duniani baada ya miaka 200 nione wanaishije hawa mabwana
 
ndio mapenzi
wanasema mapenzi hayana;
umri,
macho,
kabila,
dini,
elimu.
n.k.
 
^^
Maji ya ujana yasipoongozwa vema huweza kupanda mlima
^^
 
Kijana mdogo wa miaka kumi na sita anadiriki kuingia kwenye ugomvi wa mapenzi, ameshapoteza maisha yake kirahisi rahisi, kweli majanga
Maisha yamebadilika mno HARUFU! Sisi enzi zetu umri huo bado tulikuwa tunalala na watoto wa kike chumba kimoja bila shida lakini jaribu watoto wa siku hizi uone
 
Yaani watoto wa siku hizi ni balaa sio kama enzi zetu sisi kwa sasa wanadai
ni mambo ya globolization
 
Mama mtu anavyoumia sasa pale alipo?
 
Maisha yamebadilika mno HARUFU! Sisi enzi zetu umri huo bado tulikuwa tunalala na watoto wa kike chumba kimoja bila shida lakini jaribu watoto wa siku hizi uone
Umeona, tena hata kitanda kimoja wao wanakuwa wawili wewe mmoja katikati wala hufikirii chochote cha ajabu, lakini hii mitoto ya dijitali inazengua sana.

Dogo pimbi sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…