Hawakumaanisha walichokisema

Tumekusamehe KOIKA nishirika la misaada la korea kusini kama lilivyo JAICA la Japan labda ndilo ulitaka kumaanisha ukajikuta umeandika KOIKA na linaitwa KOICA na si KOIKA.
Asante
 
@mshanajr mbona umesahau Mbowe na yeye alileta mbwembwe akarudisha gari la kifahari la serikali huku media zikiona baadae alirudia kimya kimya pia?
Nimezungumzia kwa muktadha wa serikali sio kwa watu tena kwa majina
 
Nakumbuka hata ktk kampeni za uraisi Magufuli aliweka wazi kuwa akiingia madarakani haya magari atauza na hakuna kununua tena haya magari! hadi leo naona kimya au 'anayavutia pumzi'?
Tena ndio yameingizwa mengi zaidi haya new model
 
Dah!ktk vitu ambavyo mpaka leo vinaniuma ni kuona serikali yetu bado inanunua magari ya kifahari hasa haya ma Landcruza V8 wakati hospitali chanjo hakuna,shule shida,madawa kwa ujumla!!au haya magari wanapewa na wahisani labda mi cjui?!ila kama wananunua,hii sio kabisa!
 
Ukiwaangalia kwa mbali kama wazarendo, ukiwasogelea wezi wa kutupwa na tena hawataki kusimangwa wakituibia afadhar na zaman tunaibiwa tunaona na tunawasema
 
Kweli kabisa Wakuu. Kama kuna mahali sijamsoma JPM ni kwenye hii anasa ya magari serikalini. Nilifikiri alikuwa mtu sahihi kabisa kukomesha anasa hii. Lakini sijawahi hata kumskia akiongelea issue hii. Kuna rekodi kibao zilishatolewa kuhusu namna serikali inavyopoteza fedha kwa kuhudumia haya madude. Kwenye mambo ya anasa, sisi watanzania si maskini kabisa. Ni heri watu 500,000 wakakosa umeme lakini kiongozi mmoja akapata landcriser v8 mpya! hizi ndizo akili zetu..
 
RC Dar V8 la nini?
Hili ni swali fupi sana lakini hutapata jibu! Hata mimi naweza kuuliza tena! Hivi RC wa Dar ana umuhimu wowote kutumia gari la aina hii? Kuna magari ya bei nafuu na matumizi nafuu mengi sana amabyo angeweza kuyatumia!
 
Nimezungumzia kwa muktadha wa serikali sio kwa watu tena kwa majina
Acha unafiki bado kijana wewe, kwa hiyo Mbowe kutumia gari la serikali la kifahari ni sawa, anaahidi kurudisha lakini ni mbwembwe tu alifanya mwingine ndio unakuwa uongo.
KATAA KUWA NYUMB.U
 
Familia ya kambale, mama na mustachi, mtoto mustachi na baba mustachi, sasa swali ni nani wa kumnyoa mwenzie?
 
Ni takriban miaka zaidi ya 30 sasa tunatumia magari ya kijapani, mapya na chakavu, tafsiri yake ni kwamba mpaka vipuri nk ni vya kwao, ukija kuangalia kwa jicho angavu wajapani wamefaidika na sisi zaidi kuliko sisi tulivyofaidika nao..hawawezi kirahisi tu kukubali watupoteze!
 
Kwenye duru za siasa serikali ikaanza kupigiwa kelele kuhusu kutumia magari ya gharama kubwa bila sababu! Hii ikawa ni kama mtaji wa kisiasa, na joto lilipozidi watu ili wapate kura wakaanza kutoa ahadi za kutonunua hayo magari tena.
 
Sensa zikafanyika na baadhi yakaanza kurudishwa serikali kuu ikiwa ni maandalizi ya kuacha kuyatumia! Ilikuwa ni hatua moja mbele muhimu sana kisiasa kuna waziri mmoja wa ujenzi akajizolea umaarufu kwenye hili....!

Alichosahau ni kimoja kwamba hivi vitu vina mikataba rasmi kuwa ili upate msaada fulani inabidi kila mwaka wa fedha uagize toka kwao si chini ya magari kadhaa.

Leo hii pamoja na kelele zote zile ndio kwanza ma land cruiser ya ukweli na new model yanabanana serikalini na wizara na vitengo vyake.
 
Acha unafiki bado kijana wewe, kwa hiyo Mbowe kutumia gari la serikali la kifahari ni sawa, anaahidi kurudisha lakini ni mbwembwe tu alifanya mwingine ndio unakuwa uongo.
KATAA KUWA NYUMB.U
Small mind discuss people
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…