specialist88
JF-Expert Member
- Aug 31, 2014
- 1,140
- 619
Nashukuru Jamii forum kwa hili,
Leo nimepigiwa simu na kiongozi wa hii kampuni akiwa Zanzibar kwa namba ya halotel inayoishia na nambari 029, akasikiliza malalamiko yangu na kiukweli ameongea vizuri na mimi na kunielewesha mambo mengi na akaniniomba msamaha kwa ucheleweshwaji wa mzigo wangu na usumbufu nilioupata.
Binafsi nimepata nguvu na amani ya nafsi nilioukosa kwa muda wa miezi miwili.
----------------------------------------------------------------------
Nilichojifunza,
1.Bado kuna watu wazuri hapa Duniani, kuna watu wana utu na wanajali japo wamezungukwa na watu wasioeleweka, watu wenye makwazo, wenye dharau na kiburi,
2. Wafanyakazi wengi, waajiriwa wengi wapo kupokea mshahara tu, kupiga dili na sikufanya kazi kwa moyo, upendo na kujali wateja.-hivyo waajiri wanatakiwa kuwa kwenye nafasi yakuona makosa, udhaifu na upungufu wa wafanyakazi wao kwa haraka kabla ya hatari ya biashara kuharibika.
3. Jamii forum ni sehemu kubwa na nzuri sana ya kuelezea mambo mengi kwenye jamii yakafikia wahusika kiurahisi, na wahusika wanatakiwa kuyachukulia kwa uzito na kuyarekebisha na si kuona kama uwanja wa chuki au vita.....yaani kitu kikiongelewa humu kichukuliwe kama sehemu ya kurekebisha madhaifu na si kuchukulia kama chuki.
HITIMISHO
------------------
Naomba radhi kwa ndugu niliyeongea naye leo asubuhi lakini ningependa ajue bila '' ku-vibrate'' nisingesikilizwa au kupata call yake. Nilihangaika sana. Nilichoka akiri, ila nakushauri uwaangalie watendaji wako wa ofisi ya Dar es Salaam na kijana wako Abdul Aziz.
Pia mshauri Abdul Aziz wa China ajue``utility is what bring value in life`` sio bei ya kitu.
NB:NASHUKURU JF wote, hawa waliochangia mawazo kwenye uzi huu na DM.