Hawa "Wazimbabwe" hawaeleweki..... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hawa "Wazimbabwe" hawaeleweki.....

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ngoshwe, Oct 25, 2012.

 1. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #1
  Oct 25, 2012
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Hawa wenzetu hawana jema, awali walisema wanadhulumiwa na Serikali ya CCM wakaomba ya Mseto wakajitamba kuwa itaondoa, kero zao zote, lakini sasa bado wanalalamika tena kuwa Serikali ya Tanganyika ina wakandamiza na wanadai dola huru. Hata hivyo wakati huo huo wanamlalamikia "Mzimbabwe" mwenzao kuwatesa, na wanadai kuwa huru....

  CHRONOLOGY YA MATESO YA WAZANZIBARI CHINI YA UTAWALA WA DR. SHENI KUANZIA SIKU ALIOTEKWA SHEIKH FARID

  Written by Ashakh (Kiongozi) // 25/10/2012 // Makala/Tahariri // No comments


  [​IMG]

  Najiuliza kama je tumo ndani ya Zanzibar au ukanda wa Gaza huko Palestina? Kwani haya maafa tunayoyashuhudia tunayofanyiwa sisi wazanzibari na vikosi vya dola ni sawa na yale wanayofanyiwa ndugu zetu wa Kipalestina huko ukanda wa Gaza.

  Jambo baya zaidi, yanafanyika ndani ya Mwezi huu mtukufu ambao Waislamu wa dunia nzima wako kwenye ibada ya Hijja huko Makka. Je Dr. Sheni utakwenda kujibu nini mbele ya Allah (S.W) juu ya ufisadi na dharau yako ya dini yake ndani ya mwezi huu mtukufu, na pia wewe kuamrisha na kusimamia Waislamu na

  Wasiowaislamu (Wazanzibari) kuuliwa, kunajisiwa, kupigwa, kufungwa, kuzuwiliwa kumuabudu Allah (S.W), watu na watoto kuteswa na kupigwa risasi, watu kujazwaa khofu, n.k. Je siku hiyo ikiwadia utamjibu Allah kuwa maafa haya hukuyajuwa?

  Inshaallah naomba nikukukumbushe baadhi ya fisadi na hayo maafa unayoyasimamia na kuiendeleza ukiwa ndiwe mtawala ulioko madarakani.

  Ukurasa huu naomba uwekwe kwenye mtandao huu wa mzalendo ili uwe kumbukumbu kwa vizazi vya baadae juu ya mateso yanayofanyika ndani ya Zanzibar chini ya utawala wa Dr. Ali Moh'd Sheni.
  Yafuatayo ni baadhi tu ya maafa yanayoendelea kufanyiwa wazanzibari.
  Tarehe 24-10-2012:

  • Eneo la Kinuni mjini Unguja, vikosi vya dola viliwapiga wazanzibari kwa marungu, mateke, ngumi, fimbo, n.k. Baada ya mateso yote hayo, vikosi vya dola viliwatupa majeruhi hao kwenye gari kama mizigo. Kana kwamba mateso hayo hayatoshi, vikosi vya dola viliwamwaga majeruhi hao kwenye ukingo wa mlima wa Kinuni kama lori linavyomwaga kokoto, na hatiame wakaangukia bondeni wakiwa taabani.  • Vikosi vya dola, waliovalia kiraia, hapo uwanja wa Demokrasia (Kibanda Maiti) waliwapiga vibaya sana watoto wawili wa umri chini ya miaka 15 (kumi na tano) kwa kwa marungu, mateke, ngumi, fimbo, n.k mapaka wakawa taabani sana, huku wapitanjia wengi wakishuhudia mateso hayo. Baada ya mateso hayo watoto hao walikuwa taabani sana na wakawa wameinamia ardhi, na hapo ndipo vikosi vya dola vikaamua kuwafunga pingu na wakwa wanawapiga risasi za mpira miguuni. Na kisha majeruhi hao wakatupwa nay a gari aina ya Noah Baadhi ya walioshuhudia walikuwa wanatoka na machozi. Baadhi ya walioshuhudia waliwataja baadhi ya askari hao kwa majina ya Muhene na Haji Baunsa (ambaye pia ndie mmiliki wa gari hilo aina ya Noah).


  • Huko Kidongochekundu, mjini Unguja, vikosi vya dola vinapita nyumba hadi nyumba na kuwapiga wazanzibari na kuwaumiza vibaya sana bila kosa lolote.


  • Tarehe 23-10-2012:


  • Vikosi vya dola, vikiwa ndani ya gari nne (4) aina ya Landrover, waliwapiga vibaya sana watoto wanne wa umri chini ya miaka 13 (kumi na tatu) waliokuwa wanapita njia, kwa marungu, mateke, ngumi, fimbo, n.k mapaka wakawa taabani sana, huku wapitanjia wengi wakishuhudia mateso hayo lakini wakawa hawawezi kutoa msaada wowote. Baada ya mateso hayo watoto hao majeruhi waliokuwa taabani sana wakatupwa ndani ya magari ya Vikosi vya dola na haijuilikani walikopelekwa na walichoendakufanyiwa mbele ya safari.

  Viongozi wa UAMSHO wanyolewa ndevu rumande

  Written by Stonetown (Kiongozi) // 25/10/2012 // Habari // 3 Comments

  [​IMG]
  Na Salma Said
  VIONGOZI wanane wa Jumuiya za Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) huku wakiwa wamenyolewa ndevu wameshitakiwa mahakamani kwa madai ya kuhatarisha amani Zanzibar.

  Wakitarajiwa kufikishwa mahakamani jana kuendelea na kesi yao ya awali kwenye Mahakama ya Wilaya ya Mwanakwereke, viongozi hao walipelekwa Mahakama Kuu Vuga mjini hapa na kufunguliwa mashitaka mapya.

  Wakati wanafikishwa mahakamani kwa siku ya kwanza Jumatatu iliyopita washitakiwa wote walikuwa na ndevu videvuni mwao lakini jana walikuwa wamenyolewa. Na jambo hilo kuzua gumzo kubwa miongoni mwa jamii.

  Mkurugenzi wa Mashitaka Zanzibar (DPP), Ibrahim Mzee Ibrahim ameeleza kwa mamlaka aliyopewa na sheria ya Usalama wa Taifa kifungu cha 10 anawafungulia mashitaka watu hao akiwemo Sheikh Farid Hadi Ahmed ambaye kutoweka kwake hivi karibuni kulizua ghasia kubwa Zanzibar.

  Wengine waliofikishwa mahakamani ni masheikh Msellem Ali Msellem, Mussa Juma Issa, Azzan Khalid Hamdan, Suleiman Juma Suleiman, Khamis Ali Suleiman, Hassan Bakar Suleiman na Ghalib Ahmada Omar.
  Walisomewa mashitaka na Wakili wa Serikali, Raya Msellem liyekuwa akisaidiwa na Rashidi Fadhili na Ramadhan Nasibu mbele ya Mrajisi wa Mahakama Kuu Zanzibar, George Kazi.

  Hati ya mashitaka inasema kuwa kuanzia Oktoba 17 hadi Oktoba 18 mwaka huu katika barabara kadhaa za Mkoa wa Mjini Magharibi washitakiwa hao wanadaiwa kuwachochochea wafuasi wao kuharibu barabara, kuvunja majumba, kuharibu vyombo vya moto na kuleta hasara ya sh. 500 milioni.

  Shitaka lingine wanadaiwa kuwa kati ya Mei 26 hadi Oktoba 19 mwaka huu katika mandamano yaliyofanyika Lumumba, Msumbiji, Fuoni Meli sita na Mbuyni Unguja waliwshawishi watu wengine ambao hawapo kortini kufanya ghasia na kuhatarisha amani.

  Jumatatu iliyopita watu 7 bila kuwemo Ghalib Ahmada Omar walifikishwa katika Mahakama ya Mwanakwerekwe kwa madai ya kufanya uchochezi katika mhadhara walioufanya Agosti 17 mwaka huu.

  Waliporudishwa tena Mahakama ya Mwanakwereke kwa kesi yao ya awali haikuweza kusikilizwa kwa vile halimu hakuwepo. Washitakiwa hao wamerudishwa rumande hadi Novemba 7 kesi yao ya Mwanakwerekwe itakposikilizwa na Novemba 8 siku ya kesi ya Mahakama Kuu.

  Watuhumiwa hao walifikishwa mahakamani bila ya kuwa na mawakili baada ya mawakili wao, Salim Tawfik na Abdallah Juma kujitoa katika kesi hiyo kwa madai ya kuwa wateja wao wanadhalilishwa.

  Wakizungumza na waandishi wa habari nje ya Mahakama Kuu Vuga, mawakili hao walisema kitendo cha serikali kuwashikilia wateja wao na kushindwa kuwaleta mahakamani ni dalili tosha ya kuonesha haki haiwezi kutendeka kwani ni kitendo kinachokwenda kinyume na sheria za kimataifa na sheria za nchi hasa kwa kuzingatia kupewa dhamana ni haki ya kila raia.

  "Inaonesha hapa haki haiwezi kutendeka dalili zimeanza kuonesha mapema kwa sababu kwanza wamezuiliwa kupewa dhamana wakati pande zote mbili hazikuwa na pingamizi ya kutoa dhamana lakini mahakama ndio inakataa kutoa dhamana, lakini jambo jengine na la kushangaza walitakiwa kuletwa hapa mahakamani lakini sisi tumekuja hapa mahakama ya Mwanakwerekwe tunasubiri wateja wetu hawajaletwa mpaka saa 5:30 asubuhi tunaulizia tunaambiwa twende Vuga na tunafika hapa Vuga hakuna mtu kwa hivyo tunajitoa katika hii kesi kwa leo (jana) ili kufikisha ujumbe wa serikali kwamba hawawatendei haki wateja wetu," alisema Tawfik.

  http://www.mzalendo.net/habari/viongozi-wa-uamsho-wanyolewa-ndevu-rumande
   
 2. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #2
  Oct 26, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  mbona katika vipengele vyako hujaandika kikundi cha uamsho kuvunja na kuchoma makanisa, kufanya fujo kwenye nyumba za wachungaji na kuwatishia wao na familia yao...THERE'S ALWAYS TWO SIDES OF A COIN you know!!
   
 3. J

  JERUSALEMU JF-Expert Member

  #3
  Oct 26, 2012
  Joined: Sep 19, 2012
  Messages: 2,739
  Likes Received: 1,797
  Trophy Points: 280
  Zamani nilikuwa nawaonea huruma wapalestina wakiteswa na waisrael kumbe kama tabia zao zina fanana na UAMSHO Bora wateswe milele. hao uamsho hata wakichomwa moto kwangu mimi sawa tu mbona wao wamechoma makanisa na kuharibu biashara za watu ambao wala hawahusiki kabisa na siasa za zanziba! AKUANZAE MMALIZE.
   
 4. B

  BUBERWA D. JF-Expert Member

  #4
  Oct 26, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 446
  Likes Received: 99
  Trophy Points: 45
  huna akili kweli! huo ndo ukurasa wa kutunza kama kumbukumbu? au umeona mitandao hii niyakutunza upuuzi. shein anawaongozeni vizuri! unaona wanayofanya uamusho ndo mazuri? ila tuache mashara kumbe selikalini kuna vinyozi wazuri sana! unaona wajihi wa farid ulivyopendeza.
   
Loading...