Hawa wanaofanya uhalifu mitandaoni wako juu ya TCRA?

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Jul 17, 2019
322
645
HAWA WATU WAKO JUU YA TCRA? NITUMIE KWENYE NAMBA HII 0657523389

Na Elius Ndabila
0768239284

Itakumbukwa kuwa tuliambiwa kuwa watu wamekuwa wanatumia simu kufanya uhalifu kwa kuwa hakukuwa na namna nzuri ya usajili wa laini zetu. Kwa kutambua hilo serikali iliweka mkazo kwa kila Mtanzania kuhakikisha anakuwa na kitambulisho cha Uraia kitakachomsaidia pamoja na mambo mengine kutumika kusajilia line ya simu tena kwa njia ya Vidole.

Serikali kwa kushirikiana na vyombo vingine kwa kutambua uzito wa vitambulisho vyenyewe iliweka ukomo wa mtu kutumia line ya simu ambayo haijasajiliwa na mtu mwenye kitambulisho halali cha Uraia/NIDA. Na tarehe 7/2/2020 Tangazo la serikali number 112 la 2020 la kanuni hizo likatangazwa, yaani The Electronic and Postal Communications (SIM Card Registration) Regulations, 2020).

Hii ilijibu baadhi ya maswala kadha ambapo sasa kisheria ni lazima Laini ya Simu kusajiliwa tena kwa alama ya Vidole. Usajili huu utafanywa kwa kutumia kitambulisho cha Taifa kilichotolewa na NIDA au Namba ya Kitambulisho cha Taifa.

Sheria inasema, Mtandao wa Simu unawajibika kuzima laini ya simu ambayo haijasajiliwa kwa njia ya alama za Vidole. Lakini inaenda mbali kuwa kila laini ya simu lazima iwe na PIN ambazo lazima iwekwe kwenye simu au kifaa cha kieletroniki kila wakati simu inapowshwa au badilishwa.

Pamoja na haya, mimi nimekuwa ninajiuliza, Je hivi vitambulisho tumepigwa? Au ni Usimamizi mbovu wa vyombo vinavyohusika? Au ni Hawa watu wako juu ya sheria?

Zimekuwa zikitumiwa meseji za mtu kuomba kutumiwa hela. Moja wapo namba maarufu ni hiyo niliyoweka kwenye kichwa cha habari. Mtu mwenye namba 0734741995 amekuwa akituma ujumbe kuwa nitumie pesa kwenye namba ya Tigo 0657523389. Na hata wengine wamekuwa wakipiga kuwa mwanao ameugua ghafla shuleni tuma pesa.

Na kwa ukiziangalia hizi namba ni za Tanzania. Swali mamlaka zinawatambua hawa watu? Je kama haziwatambui, namba zao zimesajiliwa kwa njia ya NIDA? Kama zimesajiliwa kwa nini wasikamatwe? Kama hazijasajiliwa kwa nini zinatumika wakati tuliambiwa namba isiyo sajiliwa haiwezi kutumika? Mwisho kama bado uhalifu kwa kutumia simu unaendelea kama kabla ya kuwa na hivi vitambulisho ambavyo vilifanya substitution kwenye vitambulisho vya uchaguzi, kuwa na NIDA kunasaidia nini?

Ninaomba TCRA mtusaidie kuwatambua hawa ambao bado wanafanya uhalifu kwa njia ya simu ilihali tuliambiwa NIDA itasaidia hasa kwa usajili huu ya Ki-biometric.
 
Kuna message huwa zina tumwa za kutoa taarifa mambo kama hayo ya kitapeli. Kama haujapata, soma hii

Ndugu Mteja, tuma taarifa za UTAPELI unaofanyika kwa njia ya simu kwa kutuma ujumbe wenye neno utapeli kwenda 15666 kisha fuata maelekezo au piga *148*90#
 
Wote tunajua makampuni ya simu ndiyo yanatoa simkadi cha ajabu adhabu kali imewekwa kwa yule asiyesajili kadi badala ya yule anayeruhusu kadi kutumika bila kusajiliwa
 
Kuna mtu amesha kujibu cha kufanya hapo mara ukipata ujumbe wa meseji kupigiwa simu ILA
Kwa TRA kuchukulia hatua kila namba inayotuma hizo meseji za kitapeli kwa kutumia kitambulisho cha taifa inahitaji uangalifu w kwani kuna wasajili laini wasio waaminifu wameweza kusajili laini kwa matapeli kwa kutumia foto kopi za vitambulisho vya watu wengine
 
Back
Top Bottom