Hawa wameinyonga media nchini

Hawa wameinyonga media nchini

Nsimbi

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2014
Posts
1,091
Reaction score
1,208
Katika miaka ya 90 na mwanzoni mwa 2000s kulikuwa na magazeti na wahariri walitoa mchango mkubwa sana kuihabarisha jamii na kuibua uozo na kashfa kubwakubwa ndani ya Serikali na wafanyabiasha wakubwa kwa ujasiri mkubwa.

Baadae miaka ilivyozidi kwenda moto ule ukaanza kupungua makali yake na wahariri kugawanyika vipandevipande.

Why? Kwa sababu media ilianza kuingiliwa na wenye fedha hasa wafanyabiasha waliogundua njia nzuri ya kuwanyamazisha wanahabari ujasiri ni kuwatia 'mfukoni' .... Penyeza rupia... oops....hapo wahariri wanahabari wazalendo kabisa kama, wakalegea kabisa kama mlenda!!

Kwa kweli kwa sasa suala la vibrance na upendo kwa nchi miongoni mwa wahariri wengi limebaki kuwa ni historia.

Hivi sasa wahariri wengi wanawatumikia wafanyabiasha na mwanasiasa kuliko jamii.
WAFANYABIASHARA ndio wamechangia sana kuiua media na kuifanya ibakie kama a tooth less dog! Ama joka la kabisa! Baadhi ya hao mabwanyenye ni Rostam Aziz?

Kundi la pili lililoharibu ujasiri wa editors ni wanasiasa. From both CCM na Chadema wamewagawa sana wanahabari. Hivi sasa habari zinaandikwa kwa kutegemea chama au mwanasiasa gani anatoa dau kubwa. Si mnajua ndugu yetu katika shetani ....rushwa.
Mtu kama Lowassa naye amechangia sana kupooza ukali wa baadhi ya wanahabari baada ya kutambua 'udhaifu' wao mapeeema na kisha kuufanyia kazi. Kwa baadhi ya wahariri waandamizi, Lowassa ni "infallible figure"!!

Kundi lingine lililochakachua ubora wa wahariri ni baadhi ya wakuu wa vyombo vya mashirika ya umma. Nani asiyejua kuwa wamewahonga sana jamaa hawa ili kufunika uozo mbali mbali. Baadhi yao ni Dk Dau? ama Erio? au Irene?

Kundi jingine lililoleta utepetevu katika magazeti na media kwa ujumla ni Serikali. Hivi sasa State limeleta hofu na perplexity ndani newsrooms.

Sheria zilizotungwa hapa katikati zinadaiwa kukandamiza uhuru wa habari. Ni Serikali ya 'waoga' hawataki kukosolewa. Wanataka kusifiwa tu.

Mbinu za baadhi ya wanahabari kutaka kuchukua alternative ya kujipendekeza kwa rais haijafanikiwa kwani wa sasa haingiliki.
 
Mkuu unajiamini sana, unataja majina ya watu wazi wazi kwenye issue ya rushwa? PCCB wapo humu humu ujue.

Halafu ni joka la kibisa, siyo kabisa!
 
Mkuu unajiamini sana, unataja majina ya watu wazi wazi kwenye issue ya rushwa? PCCB wapo humu humu ujue.

Halafu ni joka la kibisa, siyo kabisa!
Wala hawaonei hao aliowataja,
Edward Lowassa, Rostam Aziz na Andrew Chenge ni Public Enemies na dunia inalifahamu.
Magenge yao ya kibiashara yamechangia sana kuvuruga siasa na uchumi wa nchi kwa sehemu kubwa.
 
utafiti wako?? au twaweza?
Utafiti wa nini? Mambo yako wazi. Kuna mambo ya hovyo kabisa. Hao jamaa wameitumia njaa ya wahariri kama chambo cha kuiharibu media Tanzania.
Yes, hakuna watchdogs tena. Sasa ni holela tu. Press imekuwa pressed.
 
Mkuu unajiamini sana, unataja majina ya watu wazi wazi kwenye issue ya rushwa? PCCB wapo humu humu ujue.

Halafu ni joka la kibisa, siyo kabisa!

Ndio najiamini. I do not fear death. If that what you meant.
 
Back
Top Bottom