Hawa wakina dada wanahatarisha mahusiano yangu...!!

Phlagiey

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2013
Posts
3,500
Reaction score
1,688
Jamani kuna ndoto inamsumbua sana shemeji/wifi yenu mara ya kwanza wakati ananipigia simu asubuhi na kuniambia kaniota niko na mdada nilichukulia masiraha tukaishia tu kucheka huku nikimtania unawivu mpaka ndotoni lakini sasa kadri siku zinavyo sogea hii ndoto inajirudia mara kwa mara kunasiku nilikuwa nimelala naye kuamka asubuhi akanimbia tena akiniota niko na mdada chumbani kwangu..Mbaya zaidi anaota niko na wadada tofauti tofauti..

Mara zote alizo niambia nimekuwa nikimsihii na kumpa moyo kwamba hizo ni ndoto tu, tunamalizia na maneno mawili matatu ya kimahaba, lakini sasa imekuwa kama ni kero kwangu kujirudia rudia kwa ndoto hizo zisizo kuwa na ukweli wowote. Na nina hisi maneno ya kumfariji ya takwisha na ndoto zitaendeala kujirudia.

Binafsi nimetulia sana sina ule mpango wakando naangalia zaidi majukumu ya kimaisha, habari za kubadilisha wasichana hizo kwangu hakuna na hata yeye analitambua hilo. Namheshimu kwa sababu na ye anajiheshimu na kujitambua kwa nini niko nae, haijawahi kutokea au kuhisi jambo lolote linalo husiana na mpango wa kando sasa sijui hizi ndoto zinatokea wapi mfurulizo kiasi hiki.

Si ishi nae nyuko umbali kimasomo kama kilomita 2 na nusu kutoka mazingira ninayo kaa, swala la kuonana sio shida sana hasa tunapokuwa na muda wa kufanya hivyo. Mawasiliana pia hutuweka karibu zaidi kiasi cha kutojihisi kama tuko mbali kiasi hicho, Ile hali ya upekwe na kumissiana tunaidhibiti kisawa sawa..Zile weekend huwa tunazitumia vyema kabisa bila shari..Kwenye hili hapana shaka tatizo liko kwenye zile ndoto zinakotoka.

Nifanyeje aweze kuondokana na hizi ndoto tata.
Kunawakati nampigia simu asubuhi anakuwa katika hali ya kununa..japo haoneshi wazi ila baada ya huo wivu wa ndotoni kuisha huniambia "unajua nilikuwa nimenuna" nikiuliza kwanini naambiwa habari zili zile za ndoto..

Kwa mujibu wa maelezo yake hali hii ninampa maswali mengi na wasiwasi sana huku akijihoji mbona mwanzo haikuwa hivyo.
 
Fikra za mwanaadamu siku zote zinaambatana na ndoto...Mpenzi wako ana wasiwasi sana atakuwa na wenzake na ndio maana ndoto za namna hio hazimuishi,namaanisha anafikiria sana masuala hayo...ongea nae aondoe fikra hizo na muaminishe kwamba yeye peke yake ndio ameuteka moyo wako hakuna wapinzani...
 
Fikra zake tuu ila muoneshe yeye ndo kila kitu kwako pia chunguza kama kuna rafiki / ndugu walisailitiana au yeye wifi yetu huyo umeshawahi kuumizwa ndo mana fikra zinamrudia

Pia asali yawezekana ni mapepo
 
Umewahi kulala nae walau kwa siku moja au mbili alafu akaota???

Kama jibu ni ndio bac wasiwasi unamsumbua..

Kama jibu ni hapana bac si kweli kwamba anaota ila anahis una michepuko ya kutosha tu, anachojaribu kufanya ni kutaka kuhakikisha kama anachohis ni kwel ama la..

La msingi ni kumuhakikishia kwamba ni kwel unampenda kwa dhati na huna michepuko..
 
Inawezekana mwenendo wako wa nyuma ulikuwa hivyo,sasa yeye haamini kama umebadilia au yaweza kuwa x wake alikuwa na tabia hiyo kwa hiyo anadhani na wewe ni sawa. Ni jukumu lako kuwa naye karibu na kumwonyesha mwenendo anaoutaka yeye ili kumwaminisha kuwa ndoto anazoziota si kweli
 
nina shemeji yangu, yeye akiota jambo huwa lazima litokee kweli!

yawezekana na huyo dada anaona kupitia ndoto...

punguza michepuko km kweli unachepuka brother..
 
Heading na ulichoandika ndani kiko tofauti mbona...........

We ulitaka kiweje kwa mfano..??
Hao ni wadada wa ndotoni kwani umeona hapo nimetaja mawe si umeona kabisa nimezungumzia wadada ndani ya huo uzi..
 
nina shemeji yangu, yeye akiota jambo huwa lazima litokee kweli!

yawezekana na huyo dada anaona kupitia ndoto...

punguza michepuko km kweli unachepuka brother..

Kuchepuka nilichepuka wakati nasoma sekondari baada ya kumaliza hiyo michakato yote ya kimasomo na kuingia kwenye michakoto ya kujijenga kimasha hayo majambozi nikaweka kando yuko mwenyewe tu.

Labda kama na yeye ni wa aina hiyo ya shemeji yako lakini mi sifikiri kuwa na msichana mwingine tofauti na yeye.
 
basi mkuu, fikiria mpaka nje ya box... huwezi jua labda ni visingizio ili tu mtemane.. wahi jahazi lisije likazama!
 
Kama mmoja wa mdau alivyosema awali,binadamu anaota kile anachokiwaza during the day.kwa maana hiyo shemeji yetu hapo anawasiwasi na mwenendo wako.

La kujiuliza ni kwamba kwanini huo wasiwasi uanze sasa? Tena ukizingatia kwamba hajawahi kukufumania au kupata sababu ya aina yoyote ya kuwa na wasiwasi.Mbona before hakuwa hivyo,why now?

My take,"siku zote mwizi ndio huwa na hisia za kuibiwa".Shemeji atakuwa anachepuka,anaibia ndio maana anawasiwasi kuwa anaibiwa pia.Kama hujawahi kuona dalili za wewe kuchepuka kwanini awe na wasiwasi?

Nisipigwe mawe,ni fikira za upande wa pili wa shilingi.

Maisha ni kama kioo,ukicheka na yenyewe yanacheka
 
Umewahi kulala nae walau kwa siku moja au mbili alafu akaota???

Kama jibu ni ndio bac wasiwasi unamsumbua..

Kulala nae ni zaidi ya hizo mara maja na mbili.

Kuota nikiwa nimelala nae ilitokea siku moja.

Labda wasiwasi wake tu.
 
My take,"siku zote mwizi ndio huwa na hisia za kuibiwa".Shemeji atakuwa anachepuka,anaibia ndio maana anawasiwasi kuwa anaibiwa pia.Kama hujawahi kuona dalili za wewe kuchepuka kwanini awe na wasiwasi?

Nisipigwe mawe,ni fikira za upande wa pili wa shilingi.

Mwanzo naweza kukubali kwamba labda haikuweza kutokea kwakuwa hatukuwa na ukaribu wakati huo alikuwa mkoa tofauti na mie japo tulikuwa katika mahusinao zaidi sana yalikuwa mawasiliano..

Kuhusu kuchepuka si dhani kama kunaukweli wowote kwenye hilo anajiheshimu sana, binafsi sifikiri kwenye hilo hapo sina tatizo nae kabsa.

Usiogope mkuu hapa hakuna mawe napokea mawazo tofauti tofauti yakiwemo pia hayo yako..
 
Jamani kuna ndoto inamsumbua sana shemeji/wifi yenu mara ya kwanza wakati ananipigia simu asubuhi na kuniambia kaniota niko na mdada nilichukulia masiraha tukaishia tu kucheka huku nikimtania unawivu mpaka ndotoni lakini sasa kadri siku zinavyo sogea hii ndoto inajirudia mara kwa mara kunasiku nilikuwa nimelala naye kuamka asubuhi akanimbia tena akiniota niko na mdada chumbani kwangu..Mbaya zaidi anaota niko na wadada tofauti tofauti..

Mara zote alizo niambia nimekuwa nikimsihii na kumpa moyo kwamba hizo ni ndoto tu, tunamalizia na maneno mawili matatu ya kimahaba, lakini sasa imekuwa kama ni kero kwangu kujirudia rudia kwa ndoto hizo zisizo kuwa na ukweli wowote. Na nina hisi maneno ya kumfariji ya takwisha na ndoto zitaendeala kujirudia.

Binafsi nimetulia sana sina ule mpango wakando naangalia zaidi majukumu ya kimaisha, habari za kubadilisha wasichana hizo kwangu hakuna na hata yeye analitambua hilo. Namheshimu kwa sababu na ye anajiheshimu na kujitambua kwa nini niko nae, haijawahi kutokea au kuhisi jambo lolote linalo husiana na mpango wa kando sasa sijui hizi ndoto zinatokea wapi mfurulizo kiasi hiki.

Si ishi nae nyuko umbali kimasomo kama kilomita 2 na nusu kutoka mazingira ninayo kaa, swala la kuonana sio shida sana hasa tunapokuwa na muda wa kufanya hivyo. Mawasiliana pia hutuweka karibu zaidi kiasi cha kutojihisi kama tuko mbali kiasi hicho, Ile hali ya upekwe na kumissiana tunaidhibiti kisawa sawa..Zile weekend huwa tunazitumia vyema kabisa bila shari..Kwenye hili hapana shaka tatizo liko kwenye zile ndoto zinakotoka.

Nifanyeje aweze kuondokana na hizi ndoto tata.
Kunawakati nampigia simu asubuhi anakuwa katika hali ya kununa..japo haoneshi wazi ila baada ya huo wivu wa ndotoni kuisha huniambia "unajua nilikuwa nimenuna" nikiuliza kwanini naambiwa habari zili zile za ndoto..

Kwa mujibu wa maelezo yake hali hii ninampa maswali mengi na wasiwasi sana huku akijihoji mbona mwanzo haikuwa hivyo.

kumfariji haitoshi
kakosa meongozo wa kiroho/kaanza kupotea kiroho/ shetani anawanyemelea mahusiano yote
badala ya kumfariji mwambie muwr mnasali pamoja ..mkemee roho chafu na mumrudie mola mara kwa mara kabla ya kulala na baada ya kuamka
 
Ni jukumu lako kuwa naye karibu na kumwonyesha mwenendo anaoutaka yeye ili kumwaminisha kuwa ndoto anazoziota si kweli

Mwenendo wangu hana wasiwasi nao nimejaribu kuumliza mara kadhaa na kumwambia ni aina gani maisha anayotaka tuishi..yuko huru sana kwangu na kwenye vitu vyangu mzunguko wa maisha yangu ya kila siku anaujua mpaka naingia kitandani..na me pia hako kamchezo ka kuchanganya sketi sina .

Hakuna shaka nitalifanyia kazi wazo lako.
 
basi mkuu, fikiria mpaka nje ya box... huwezi jua labda ni visingizio ili tu mtemane.. wahi jahazi lisije likazama!

Hakuna dalili zozote za kutema mkuu ila hizo ndoto tu ndo huwa zinampa tabu kidogo.
 
Back
Top Bottom