Tata ya bana
JF-Expert Member
- Jul 14, 2018
- 304
- 369
Wakuu hebu tujadili kuhusu huu mtandao wa Tigo na usumbufu wanaotupa wa kupigiwa na no.zao zinazoanzia 0901.nimeblock kama 9 ila kila siku wanakubadilishia no.nina mitandao yote mbona wengine hawatupigii na kutusikilizisha manyimbo yao?kuna siku nasubiria dili LA kazi nipo toilet nikasikia simu inaita sebuleni nilikata na kuwahi kupokea kumbe wao,dah ingekuwa sio naongea na computer ningetukana pale.je mnalionaje?