Hawa Speedaf wa mizigo ya China wapo haraka Posta hamna kitu

toplemon

JF-Expert Member
Mar 26, 2017
4,581
4,631
Wakuu kuna hawa watu wa kusafirisha viparcel kutoka aliexpress na mitandao ya China wapo vizuri sana naona ndo wamekuja kuleta mapinduzi ya manunuzi ya bidhaa za mtandaoni.

Kiukweli Posta wajipange kweli kweli hawa jamaa wapo fasta sana yaani mzigo wa kusafirishwa kwa posta siku 20 wao wanakusafirishia siku tatu tu.

Hakika wapo vizuri, changamoto inakuja kwa Tanzania wapo mikoa mingi ila bado hawajawa na ofisi specific kabisa ya kazi.

Mfano kwa Dsm wapo Mikocheni but still bado hawajawa na ofisi rasmi, ila kwa mizigo nawapa big up.

Posta nao wabadilike kwakweli waache ukiritimba ambao hauna maana.
 
Back
Top Bottom