Siku yangu imeisha vibaya sana leo.
Niko kijiwe changu cha kuuza mbao, biashara hamna kabisa. Napigiwa simu na mama tunafahamiana kwa karibu anatuma watoto wake kuja kununua mbao. Nikaanza kujipanga na kufurahi kimoyo moyo, jf weka kule kwa sababu ndo iliyoniweka busy huku nikihesabu magari yanayopita barabarani.
Vijana wakafika wa kike na wa kiume tukaanza kupimiana mbao, shughuli ikiendelea yule wa kike akanifuata anataka nimdanganye mama yao bei ya mbao ili wabaki na hela. Watoto bila hata soni wataka kumuiba mama yao. Karibu nikubaliane nao sijauza hata mabanzi na wiki ndio inakata hii.
Hivi kuna haja gani ya kumuibia mzazi wako? Hela ya huyu mama ni pension yake baada ya kustaafu, watoto wake wa kuwazaa wasipoona huruma nani atamuhurumia?
Cha juu zipo nyingi lakini hii wacha inipite