maramia
JF-Expert Member
- Jul 17, 2015
- 2,030
- 1,345
Kama wangekuwa wasakata ndinga ningewaita wachezaji bora wa mwaka. Hata hivyo niwafananishe na wachezaji nguli wa timu za Hispania za Barcelona na Real Madrid Lionel Messi na Christiano Ronaldo.
Tuhuma alizotoa Paulo Makonda dhidi ya Kabwe katika kadamnasi ile ya sherehe za ufunguzi wa daraja jipya la Julias K Nyerere mbele ya Rais na hatua ya mhe Rais kummwagia sifa Dk Ramadhan Dau kwa mchango wake ktk ujenzi wa daraja hilo imenivutia sana. Na bila hatua ile ya Rais sijui kama Dau angepata usingizi leo kwa watanzania kutoutambua mchango wake kiasi cha kupelekea kutotajwa hata jina lake katika ufunguzi ule.
Katika sherehe zile Makonda na Dk Dau wamefiti kuitwa mashujaa.