GE2010 Hawa ni hatari zaidi kwa taifa letu

GE2010 Hawa ni hatari zaidi kwa taifa letu

TandaleOne

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2010
Posts
1,644
Reaction score
709
Nyote mtakubaliana nami kuwa washabiki wa kisiasa (political commentators) ni watu muhimu katika taifa lolote lile katika kufanyia uchambuzi mambo mbalimbali ya kisiasa na wakati mwingine kijamii katika nchi au bara husika.Katika hawa wako waandishi wa habari (waliofuzu taaluma hiyo na hata wale ambao hawajafuzu kimsingi),viongozi wa dini (hasa zile dini zisizo na wafuasi wengi) ,viongozi wa asasi za kiraia na wengineo wafanyao kazi hiyo.Leo hii ukiamka na kwenda kununua gazeti,kwenda uwanjani kupata burudani na kwingineko watu hawa ndo tunakutana nao.Wapo wanaozungumza mambo ya msingi na wapo ambao ukitafakari wanachosema unapata ugumu kuelewa kama kweli wanatumia vizuri akili zao katika kutafakari mambo.Wapo wengine huenda mbele zaidi na kujiita watafiti wa mambo huku kile wanachokiongea kikiwa hakiendani kabisa na taaluma hiyo ya utafiti.Tanzania ya leo imegubikwa na chuki katika makundi ya watu wa kipato cha juu ambao nao hawa wametafuta support toka kundi la watu wa kipato cha kati (vijana,wasomi na wafanyabiashara).Hawa nao wametafuta pia support kwa kuwarubuni watanzania wa kipato cha chini walio wengi kujiunga nao kupitia kila aina ya propaganda.Wengine wanawanyonya kwa kujiita manabii na wachungaji huku wakianzisha makanisa na madhehebu lukuki,wakijineemesha wao na kujiita wajasiriamali.Wengine wameingia katika kundi la wanasiasa,hawa wanajiita wakombozi (inawezekana wapo wenye nia),hawa wanatumia kila aina ya unyonge na matatizo waliyo nayo wananchi kama ngazi ya kupandia kwenye mafanikio yao binafsi na vikundi vyao(muda utasema).Watu hawa kama nilivyosema awali,wana lengo la kuona yale wanayotaka yanatimia.Kama mwanafunzi anapodhamiria kufaulu mtihani kwa gharama yoyote ile.Wapo watakaosema uongo,watakaolia na hata wapo watakaosema wameshushwa na Mungu wakikomboe kizazi.Yote katika yote napenda kuwaasa Watanzania wenzangu wenye nia njema na taifa kutafakari yale ambayo tunayapitia leo,kesho na siku zijazo.Kujua nafasi ya kila mmoja wetu na kujua kwamba siasa na uongozi ni zaidi ya kile ambacho tunakisikia.Umoja wetu na mshikamano wetu si kitu cha msimu.
Mungu Ibariki Tanzania
 
Tandale One, asante sana kwa maoni yako ya angalizo dhidi ya watu hatari kwa taifa hili. Kwa maoni yangu, watu hatari zaidi ni wale wanaowadanganya watu kwa ahadi kemkem kama kuwaletea "Maisha bora kwa kila Mtanzania kwa kutumia Ari Mpya, Nguvu Mpya na Kasi Mpya". Miaka mitano imepita hayo maisha bora hayajaonekana sasa unakuja na ahadi nyingine ya "Maisha bora kwa kila Mtanzania ila sasa ni kwa Ari Zaidi. nguvu Zaidi na Kasi Zaidi!"
 
Mungu wakikomboe kizazi.Yote katika yote napenda kuwaasa Watanzania wenzangu wenye nia njema na taifa kutafakari yale ambayo tunayapitia leo,kesho na siku zijazo.Kujua nafasi ya kila mmoja wetu na kujua kwamba siasa na uongozi ni zaidi ya kile ambacho tunakisikia.Umoja wetu na mshikamano wetu si kitu cha msimu.
Mungu Ibariki Tanzania

CCM imekuwa ni Chama cha Mafisadi na hivyo kutishia umoja wetu na mshikamano na Mwenyezi Mungu kamwe hataibariki Tanzania kama sisi ni wavivu wa kuwatolea uvivu viongozi wabinafsi ambao mabilioni wanayaita ni vijisenti tu na wakati sisi wengine hata chumvi ndani ya nyumba zetu hakuna.

CHAGUA DR. SLAA CHAGUA CHADEMAAAAAAAAAAAAAAAAA
 
Tandale One, asante sana kwa maoni yako ya angalizo dhidi ya watu hatari kwa taifa hili. Kwa maoni yangu, watu hatari zaidi ni wale wanaowadanganya watu kwa ahadi kemkem kama kuwaletea "Maisha bora kwa kila Mtanzania kwa kutumia Ari Mpya, Nguvu Mpya na Kasi Mpya". Miaka mitano imepita hayo maisha bora hayajaonekana sasa unakuja na ahadi nyingine ya "Maisha bora kwa kila Mtanzania ila sasa ni kwa Ari Zaidi. nguvu Zaidi na Kasi Zaidi!"

Kuna umuhimu wa kufanyia uchambuzi ahadi zote na kuangalia uhalisia wake.Ila katika suala la maisha bora bado nakataa kwamba maisha bora si kama tunavyodhani.Si kifurushi cha zawadi.Ni means za kufikia maendeleo.Kama upatikanaji wa elimu,afya na mazingira mazuri kwa wajasiriamali.
 
CCM imekuwa ni Chama cha Mafisadi na hivyo kutishia umoja wetu na mshikamano na Mwenyezi Mungu kamwe hataibariki Tanzania kama sisi ni wavivu wa kuwatolea uvivu viongozi wabinafsi ambao mabilioni wanayaita ni vijisenti tu na wakati sisi wengine hata chumvi ndani ya nyumba zetu hakuna.

CHAGUA DR. SLAA CHAGUA CHADEMAAAAAAAAAAAAAAAAA

Mbona umeandika kwa rangi nyekundu?Au ina maana fulani.
 
Sikuona cha kujadili maana popo anaweza kuwa ndege au mnyama!
 
Harakati za ukombozi wa kifikra hazina chama, dini wala kabila.
Wananchi wenye mawazo ya hovyo hovyo watapata viongozi wenye mawazo hovyo hovyo kwa kuwa viongozi wanatoka miongoni mwa wananchi!
Hatutakiwi kushabikia wagombea kama shindano la mpira kati ya Simba na Yanga, jambo la msingi kabisa ni kuwaelimisha wananchi waweze kujua jema na baya, faida na hasara ya kuchagua viongozi kwa ushabiki tu na kujua uhusiano uliopo kati ya uongozi wa nchi na hali zao za maisha ambazo ni miongoni mwa zilizo duni kabisa duniani.
 
Back
Top Bottom