sijui nini
JF-Expert Member
- Sep 29, 2010
- 2,553
- 1,290
Nimeamini siku hizi barabarani wenye magari ni wengi kuliko madereva....Hizi tabia zina kera sana barabarani..kama na wewe huwa unafanya haya barabarani basi jua unakera wenzako:
1. Unakuta barabara ya njia(lanes) mbili halafu mtu anaendesha gari katikati ya hizo lane mbili afu unaenda taratibu..hueleweki upo kushoto au kulia...kagari kenyewe kadogo sasa si ukae lane moja uwapishe wengine...?
2. upo njia kuu unakuja yeye anataka kuingia na anakuona kabisa lakini na yeye anaingia tu afu anaanza kutembea taratibu wakati mtu unaharaka zako...sasa si ungenisubiri nipite..si ndo sheria..kama uliona utawahi basi tembea mwendo wa kueleweka au mpishe mwenzako aendelee za safari zake na wewe uendelee na mwendo wako mdogo..au unaona raha kufuatwafatwa matakoni...??
3.haya nimeamua kuvumilia mwendo wako mdogoo wee nimepata nafasi nataka niku overtake..naanza kukupita na wewe unaongeza mwendo...iiish!! unaakili wewe..??nikipunguza nikuache utangulie unaenda kidogo unarudia mwendo wako ule ule..kwani nashindana na wewe jamaa..
4. saa kumi na mbili jioni hata giza halijaingia vizuri tena unapita katikati ya mji mtu ameshawasha taa FULL LIGHTs??? hivi unajua maana ya hizo taa? unawamulika wenzako..wanakuonyeshea na ishara kwamba unawamulika wewe walaaa..kwani unapita porini?? kuwa mstaarabu..au ndo hata hizo taa hujui kwanini zinawaka tofauti tofauti unavyowasha??
5. barabara nyembamba..mbele yako kuna msukuma mkokoteni tena anajitahidi kweli kusukuma kwa nguvu ili asiweke foleni ila wewe bado tu na mahoni yako..piii piii piii..sasa we unataka apae?? ustaarbu kitu cha bure..au unaona kuna foleni labda mbele kabisa kuna lori linakwenda taratibu na kwa kulipita hamna wewe unakuja tu huko unaanza kupiga mihoni yako..sasa unataka kitokee nini...
6.kisa wewe una gari basi waendesha pikipiki,(kumbuka si kila mwendesha pikipiki ni bodaboda), baiskeli na wapita kwa miguu kwako hawana haki ..kila sehemu wewe ndo unajifanya una haki..unakuta round about kuna mtu wa pikipiki au baiskeli anakatisha na wewe unaingia tu ...kisa wewe una gari..?? au wewe ndo unaingia njia kuu na kuna baiskeli inakuja au pikipiki na umeiona kabisa ila wewe unaingia tu... sheria huijui..hata ustaarabu pia??
7. barabara inapita katikati ya mtaa..kuna watoto kibao wanakatiza na kibao cha spidi kipo ila mtu unakimbia spidi 100...??bure kabisa...
8. ongezea na wakwako wanaokukera...

Last edited: