Lukansola
JF-Expert Member
- Sep 5, 2010
- 5,435
- 1,597
Ilikuwa majira ya saa saba mchana pale maeneo ya PPF Towers jijini Dar es Salaam leo tarehe 2 march 2011, nikiwa katika harakati za kusababisha mikono yangu na ya wale wanaonitegemea iende kinywani, ghafla nikawaona hawa, nikashawishika kuwapiga picha ili ku-share na wanajamii wenzangu The Great Thinkers.
Wanasema uchungu wa mwana aujuae ni mzazi, mimi ninao watoto, ninaujua uchungu wa mwana, nina amini hata watoto hao wana wazazi wao pia, najaribu ku imagine uchungu walio nao wazazi wa watoto hao, endapo wapo hai au wanawajua watoto wao hao. Maana kuna uwezekano hata baba zao hawajui kama watoto hao ni wao (si nasikia kuna watoto wengine huzaliwa bila mama zao kuwa na uhakika baba zao ni kina nani au kutowajua kabisa) anyway mwisho wa siku ni watoto wa Watanzania ni watoto wetu wote, ndio tunaowategemea waijenge Tanzania ya kesho.
CCM imeahidi maisha bora kwa kila mtanzania, ndio kauli mbiu ya chama hicho, na juzi katika hotuba ya rais wetu moja kati ya zile za kila mwezi alisema mafanikio mengi yamepatikana katika utawala wa CCM na yanaonekana ingawa mimi binafsi sijayaona kihivyo, najiuliza hivi itachukua muda gani kabla hatujaacha kukutana na taswira kama hizi katika Tanzania yetu.
Na hawa ni baadhi tu ya watoto wanao ishi kwenye mazingira kama haya kote Tanzania, achilia mbali wale wanaosafisha vioo vya magari pale kwenye mataa ya moroko na kwingineko huku wakitarajia ujira mdogo kutoka kwa wenye magari hayo.
Wapo wale wanaofanya biashara ya ngono wakiwa na umri mdogo, kwa ajili ya kuepuka kifo cha njaa, hakika siwezi kuwakilisha matatizo yote ya kijamii hapa.
Hebu na sisi tuchangie mawazo yetu hapa hivi kuna kitu tunaweza kufanya kuepusha aibu hii kwa taifa letu, nina amini hata wageni wanaona kama tunavyoona sisi, si wanapita humuhumu tunamopita sisi? unless mnaniambia hali hii hata kwenye nchi zilizoendelea ipo, mnaoishi majuu tuambieni.