Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 26,006
- 51,231
Wakati hapa kwetu wale wanaopingana na serikali kwenye mambo mbali mbali huitwa ni vibaraka wa Mabeberu, nchini marekani kuna vikundi vingi sana vinavyopingana na serikali yao kuhusu kuingilia mambo ya nchi nyingine kwa kuchochea mapinduzi kwenye nchi hizo.
Tofauti na kwetu watu hao hawakamatwi kwa kupingana na serikali ya nchi yao wala hawaitwi vibaraka.
Kundi linalojiita "Code Pink" limevamia na kuishi kwenye nyumba ya Ubalozi wa Venezuela nchini Marekani kwa lengo la kuzuia wafuasi wa Juan Guaido wanaoungwa mkono na serikali ya Marekani kuingia kwenye Ubalozi huo baada ya maafisa wa ubalozi wanaomuunga Rais wa sasa wa Venezuala Nicolas Maduro kuondoka.
Hawa wako kwenye nchi ya "Mabeberu" na je na wao ni vibaraka wa nani?