Hawa jamaa wangekuwa wanaona mbali

Hawa jamaa wangekuwa wanaona mbali

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
52,648
Reaction score
164,806
Kuna kila dalili kuwa upinzani kupitia umoja wao wanaweza kushika dola na hata kama si kwa nafasi ya uraisi,basi hata kwa kudhibiti Bunge kwa maana ya kuwa na wabunge wengi wa upinzani na kudhibiti Bunge maana yake ni kudhibiti serikali kupitia Bunge.

Viongozi wengi wa leo wanakabiliwa na tuhuma nyingi na pia kumekuwepo na kashifa nyingi ambazo ziikiibuliwa na kusimamiwa ipasavyo mahakani,viongozi wengi wa sasa na waliopita ama wanaweza kufungwa au hata kusota mahabusu kwa muda wakisubiri dhamana kama zitatolewa(zitakuwa wazi).

Hata hivyo,watawala hawa wangekuwa wanaona mbali basi wangetumia kipindi hiki kifupi kilichobaki kuboresha hali mbaya za magereza yetu pamoja na mahabusu zilizopo ili yakiwakuta basi wasiumbuke sana.

Hivi katika magereza yetu kuna sehemu za VIP?Kama zipo,zitatosha kuwa-accomodate wote?

Msimu huu ongezeni bajeti ya wizara husika ili kukarabati magereza na mahabusu za nchi hii.

Kwa kifupu,watumie muda huu mfupi uliobaki kujiandalia makao.

Ni ushauri tu.
 
Hii nchi viongoz wanajuana, hakuna atakayefungwa.
 
Mkuu umenena. Hata kule Nigeria kuna kiongozi alimfunga mwenzake. Alipokuta hali ilivyokuwa akamwambia rais aboreshe magereza kwa kuwa anaweza akawa next victim hakusikia. Alipotoka madarakani tu akafungwa na akafa kutokana na hali ya gerezani Kama wamesoma hapa waboreshe mapema kwani dalili sio nzuri kwao.
 
Nimeipenda hyo.. Yani iwe kama kipindi kileee cha liyumba na mramba..du segelea kulibadlika ghafla.
 
Back
Top Bottom