Hawa hapa Waliochaguliwa Kidato cha tano, Wanafunzi 3,000 waliofaulu waachwa

imabango1986

Member
Aug 20, 2013
18
95
Simbachawene-2_1497009543-1600x705.jpg

Waziri wa TAMISEMI, George Simbachawene

Serikali imetangaza orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha tano na vyuo vya ufundi kwa mwaka 2017 huku wanafunzi 2,999 wakiachwa.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), George Simbachawene ametoa idadi hiyo leo Juni 9, mjini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa ufaulu kwa mwaka huu umeongezeka kwa asilimia 3.75 ukilinganisha na matokeo ya mwaka 2015.

Amesema kati ya wanafunzi 96,018 waliofaulu kwa daraja la kwanza hadi la tatu ni wanafunzi 93,019 pekee waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya ufundi.

Amesema kutokana na mwongozo wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia wa Mei 15, 2017 jumla ya wanafunzi 93,019 ndiyo wenye Sifa za kuchaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya ufundi kwa kuwa wamefaulu kwa vigezo vyote vya msingi ambapo kati ya hao 92,998 ni wa shule na wanafunzi 21 ni wale waliosoma taasisi ya elimu ya watu wazima.

Aidha amewataka wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano kuwasili kwa wakati katika shule walizopangiwa Julai 17 mwaka huu na kwamba hakutakuwa na mabadiliko ya shule walizopangiwa.

"Na kama kuna mwanafunzi ambaye hataripoti kwenye shule aliyopangiwa kwa muda wa siku 14 nafasi yake itachukuliwa na mtu mwingine," amesema Simbachawene.

===========

Kuangalia Majina Bofya Hapo chini
1.Waliochaguliwa Kujiunga Kidato cha 5 na Vyuo vya Ufundi awamu ya Kwanza 2017

2.Watakaochaguliwa Kujiunga Kidato cha 5 na Vyuo vya Ufundi awamu ya Pili 2017
 

Kunguru wa Manzese

JF-Expert Member
Apr 20, 2016
4,519
2,000
duh! naomba mniangalie majina ya walioweza kupata nafasi ya kuchaguliwa kutoka usagara secondary school S.0345
 

Cognitivist

JF-Expert Member
Aug 7, 2011
1,059
2,000
Huyu simbachawe naye aache ulimbukeni na vitisho vya kukariri, yeye mwenyewe kasema wanafunzi wote wenye sifa wamepangiwa shule na kwamba walioachwa hawana sifa sasa hivyo anavyosema usiporipoti baada ya siku 14 nafasi yako itachukuliwa na mtu mwingine ni nani huyo?kutoka wapi kwa sifa zipi? Zero brain Vi.wonder
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom