Extrovert
JF-Expert Member
- Feb 29, 2016
- 67,119
- 173,952
Juzi nimefanya trip toka mjini mpaka kitaa kutumia app yao ya Bolt. Safari ilikuwa ya approximately 12km ambapo kwa initial price ilinipa 7000-9000 nikajua ikizidi basi walau elfu 10 sio mbaya.Kilichotokea nafika jamaa ana end trip bei iliotokezea ni 16,000. Sikuelewea hasa ni kipi kimefanya ile bei iwe kubwa namna ile ila moja kwa moja naichukulia kama dhuluma tu. Ni wizii uliokithiri kwa kweli na hauvumiliki na sijui ni mimi tu ndio yamenikuta au kuna wenzangu nao wametokewa na hio situation ya overpricing!?
App ya Uber kwa umbali huo huo huwa inacharge 11000 ikizidi sana ni 12000! Very reasonable increment. Toka bei ya awali ya 9000-10000. Mwanzoni Taxify ilikuwa nzuri kwa bei nafuu ila sasa toka iitwe Bolt ni kigango cha ujambazi kwa kwenda mbele, halii hii haivumiliki watoa leseni wa hizi kampuni pigaji waziangalie upya.
Waliowahi kukutana na hii kadhia jitokezeni tupaze sauti