Hawa Bolt (Old Taxify) ni majambazi wa mchana kweupe!

Juzi nimefanya trip toka mjini mpaka kitaa kutumia app yao ya Bolt. Safari ilikuwa ya approximately 12km ambapo kwa initial price ilinipa 7000-9000 nikajua ikizidi basi walau elfu 10 sio mbaya.Kilichotokea nafika jamaa ana end trip bei iliotokezea ni 16,000. Sikuelewea hasa ni kipi kimefanya ile bei iwe kubwa namna ile ila moja kwa moja naichukulia kama dhuluma tu. Ni wizii uliokithiri kwa kweli na hauvumiliki na sijui ni mimi tu ndio yamenikuta au kuna wenzangu nao wametokewa na hio situation ya overpricing!?

App ya Uber kwa umbali huo huo huwa inacharge 11000 ikizidi sana ni 12000! Very reasonable increment. Toka bei ya awali ya 9000-10000. Mwanzoni Taxify ilikuwa nzuri kwa bei nafuu ila sasa toka iitwe Bolt ni kigango cha ujambazi kwa kwenda mbele, halii hii haivumiliki watoa leseni wa hizi kampuni pigaji waziangalie upya.

Waliowahi kukutana na hii kadhia jitokezeni tupaze sauti
Taxify kabla haijabadilishwa ilikua hivo hivo,madereva wanaichezea nikategemea ilivobadilishwa itakua washafix tatizo hilo kumbe ndio hvo hivo
 
Hii inawezekana vipi, yaani nikubaliane na fundi kwamba ataifanya kazi kwa shs.10,000/=, halafu akishakamilisha kazi aje kunidai 15,000/=, sasa ukimpa hiyo 5,000/= ya ziada ni umetaka mwenyewe, maana yeye anajuaje labda sina?
 
Hii lilinikuta nilirequest bolt toka manzese tip top mpaka ferry, ilikua inasoma elfu 10 ila kufika kumaliza trip ikasoma elfu 16,nikalipa cash bado wananitumia email kua nadaiwa card yangu inabill sababu nilitakiwa kulipa kwa card nikawaona hawa kweli wehu, now bora kuongea na dereva wa tax anakucharge ambayo unajua ukifika ni hiyo hiyo. Uber nao walishanikera nilishapanda moja mwaka jana nikawachukia kabisa nilikua natoka ferry naelekea Manzese tip top ila dereva kwenye kupita pita tulipita mpaka Coco beach nikawa namuangalia tu nia yake mwisho wa safari route iwe ndefu, watanzania tunaharibu sana business kwakweli
 
Hivo vitu ni vya wenye pesa, kama huwezi endelea na maisha yako ya boda boda na vibajaji unataka kukimbia na hauna break! What do u expect?
 
Hivo vitu ni vya wenye pesa, kama huwezi endelea na maisha yako ya boda boda na vibajaji unataka kukimbia na hauna break! What do u expect?
Usizungumzie vya wenye hela. Ndio maana hata huko ulimwengu wa kwanza vilipoanzia kuna consumer protection agencies. Kwa kuwa wewe ni mteja hutakiwi kulipa tu bila wao kuzingatia ubora wa huduma. Huu upuuzi uko Africa tu.
 
Atleast Uber system yao haichezewi,uber ukirequest basi utalipa pesa ile ile uliyokadiriwa haitazidi zaidi ya hiyo.
Uber ni ahueni, afadhali kabisa yani japo inaonekanaga ni gharama kuliko taxify penye ku start trip
 
Taxify kabla haijabadilishwa ilikua hivo hivo,madereva wanaichezea nikategemea ilivobadilishwa itakua washafix tatizo hilo kumbe ndio hvo hivo
Kipindi nimeanza kutumia Taxify ilikuwa cheap sana kuliko uber. Ila nimekuja kuitumia ikiwa Bolt ndio hata sihitaji kuiskia tena nimeishaifutia mbali
 
Kipindi nimeanza kutumia Taxify ilikuwa cheap sana kuliko uber. Ila nimekuja kuitumia ikiwa Bolt ndio hata sihitaji kuiskia tena nimeishaifutia mbali
Mimi nimeanza kuikimbia taxify kaba haiajabadilishwa mtindo huo ulikua ushaanza..baada ya kubadilishwa nikajua watakua washaupdate system yao kumbe ni vile vile
 
Back
Top Bottom