Hausigeli Akatwa Mdomo na Bosi Wake Saudi Arabia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hausigeli Akatwa Mdomo na Bosi Wake Saudi Arabia

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Dec 22, 2010.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Dec 22, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  fanyakazi wa ndani raia wa Indonesia aliyekuwa akifanya kazi katika nyumba moja katika mji wa Madina nchini Saudi Arabia, amelazwa hospitali katika chumba cha watu mahututi baada ya kukatwa sehemu ya mdomo wake na kuchomwa kwa pasi ya moto sehemu mbalimbali za mwili wake.
  Wimbi la Wafanyakazi wa ndani kuteswa na mabosi wao katika nchi za kiarabu limezidi kuendelea ambapo safari hii mfanyakazi wa ndani mwenye umri wa miaka 23, amekatwa mdomo wake wa juu na bosi wake.

  Mfanyakazi huyo wa ndani, Sumiati Binti Sala Mustapa amelazwa hospitalini kufuatia mateso toka kwa bosi wake wa mji wa Madina, mwanamke raia wa Saudi Arabia mwenye umri wa miaka 53.

  Sumiati alishambuliwa na muajiri wake ambaye hivi sasa ametupwa rumande. Sumiati alikatwa sehemu ya mdomo wake kwa mkasi, aliunguzwa na pasi ya moto mgongoni na alipigwa sana miguuni kiasi cha miguu yake kukaribia kupooza na kumfanya atembee kwa tabu sana.

  Kwa mujibu wa gazeti la Saudi Arabia la Al-Watan, kipigo alichopewa Sumiati kilisababisha kuvunjika kwa baadhi ya mifupa ya mikono na mbavu zake.

  Maafisa wa Saudia na maafisa wa Indonesia walikutana juzi mjini Madina kujadili kesi ya Sumiati ambayo imesababisha mtafaruku mkubwa nchini Indonesia.

  Maafisa wa serikali ya Saudi Arabia wameahidi kuifuatilia kesi hiyo kwa ukaribu zaidi.

  Sumiati amelazwa kwenye hospitali ya Mfalme Fahdi mjini Madina ambapo madaktari wamelazimika kumfanyia upasuaji wa kurekebisha sura yake iliyoharibiwa vibaya.

  Hii ni miongoni mwa kesi ambazo zimekuwa zikitokea katika nchi za kiarabu katika siku za karibuni.

  Wiki iliyopita, maafisa wa Saudi Arabia waliuokota mwili wa mfanyakazi wa ndani wa kike naye toka Indonesia ambaye inaaminika alifariki kutokana na mateso toka kwa muajiri wake.

  Kesi za kuteswa kwa wafanyakazi wa ndani nchini Saudi Arabia zimesababisha watu wengi nchini Indonesia kuishinikiza serikali ya Indonesia kuzuia wafanyakazi wa ndani kupelekwa Saudi Arabia.
   
 2. mluga

  mluga JF-Expert Member

  #2
  Dec 22, 2010
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 678
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hivi ndugu zetu wazanzibari huwa hawachangamkii hizi tenda za kwen da kufanya kazi huko? wazee wa CUF mpo?
   
 3. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #3
  Dec 22, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Heheheeheheeheh hawa jamaa kiboko!
   
 4. Kimox Kimokole

  Kimox Kimokole Verified User

  #4
  Dec 22, 2010
  Joined: Jun 9, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Saudia kwa kutesa watu ni kiboko, si wafanyakazi wa ndani, madereva wote tabu tupu
   
 5. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #5
  Dec 22, 2010
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Hii Saudi ipi ? kule tunakokwenda kuhiji? Kule mahali patakatifu?
   
 6. Ustaadh

  Ustaadh JF-Expert Member

  #6
  Dec 22, 2010
  Joined: Oct 25, 2009
  Messages: 413
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Inasikitisha
   
 7. Kimox Kimokole

  Kimox Kimokole Verified User

  #7
  Dec 22, 2010
  Joined: Jun 9, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  hukohuko kulikolaaniwa
   
 8. Afrika Furaha

  Afrika Furaha JF-Expert Member

  #8
  Dec 22, 2010
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 329
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Inawezekana watu wanachanganya maneno, ni mahali PA TAKATIFU, au PA TAKAKIFO??
   
Loading...