Birdman
Member
- Oct 31, 2012
- 79
- 24
Wajameni nimepatikana kwa pesa mbili. Baada ya kuhangaika kutafuta msichana wa ndani mke wangu aliomba msaada na tukaletewa toka ukweni - kabila sitaji ila la wajeuri. Msichana hard working lakini masharti kibao. No kitimoto ndani ya nyumba, marufuku mbwa kumnusa, so hao nawalishe mwenyewe, pia marufuku kupishana nao, so mpaka wakishafungwa hatoki nje. No disrespect kwa imani za kidini, but msichana swala zote tano na mbaya zaidi, nikichelewa kurudi home - say 1130pm, yeye wala bosi wake (wife) hawashughuliki. Kumtimua gharama za kumsafirisha, offence kwa mke na mama yake. Kumwacha bughudha - sina imani naye especially na watoto - my kids love dogs. Shida sasa, nyumbani panaanza kuwa jela - natamani nirudi late kila siku kuepuka maudhi. Wajameneni - tuseme hayo ni makubwa ya kujitakia. Naombeni ushauri kabla ya kumtimua. Baadaye ntatoa ushauri kwa wazazi wenzangu - kutoka wapi usithubutu kuletewa msichanana wa kazi. Nawasilisha.