Hatuwezi kupingana na hili, endapo Muungano utavunjika

mnoel

JF-Expert Member
Aug 14, 2012
211
98
Kuvunjika kwa muungano ni suala zito sana na sisi kama Watanzania tusiombe litokee kwa kizazi hiki na hata kijacho. Uwe CCM, CUF na hata kama huna chama utaathirika kwa njia moja au nyingine. Naomba kugusia resource moja ambayo tunashare. BAHARI. Kwa data zisizo rasmi zaidi ya 40% ya wazanbar wanategemea uvuvi, vivyo hivyo asilimia kubwa ya mikoa ya pwani ya Tanzania Bara inategemea uvuvi ili maisha ya familia zao yaweze kusonga mbele. Hali ilivyo sasa ni kwamba mzanzibar na mtanzania bara wana uwezo wa kuendesha shughuli zao za kivuvi katika eneo lote la bahari ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania. Hii inajumuisha (Territorial sea, ambayo huesabiwa 12 neutical miles from the lower water mark ambapo kwa Jamhuri ya muungano wa Tanzania hueasabiwa kuanzia pwani (Coastline ya Zanzbar ) kuelekea Mashariki mwa bahari ya hindi. Kutokana na Law of the Sea Conventiion ya mwaka 1982 inaeleza kwamba kama nchi ina visiwa na lower water mark(coastline) yake haipo straight basi vpimo vitakadiriwa pale ambapo coastline itakuwa imenyooka na ndiyo maana vipimo vya eneo letu la bahari linaanzia mashariki mwa visiwa vya Zanzbar kwenda deep sea. Maji yaliyopo kati ya Tanzania bara na Zanzbar they are regarded as internal waters.
Ukiachilia mbali hiyo territorial sea pia tuna Exclussive Economic Zone EEZ. Hii ina urefu wa 200 neutical miles from the lower water mark. Hili ni eneo linaloruhusiwa kufanyika kwa shughuli zozote za uvuvi pamoja na kuzisimamia rasilimali zote zipatikanazo hapo ikiwemo mafuta. Hapo ndio ukomo wa eneo la jamhuri ya muungano wa Tanzania kuelekea baharini kuhusu suala zima la uvuvi.

Swali. Endapo tukitengana na zanzbar itakuwaje? Jamii ya wavuvi itaathrika vp?

Kutokana na Law of the sea convention ya mwaka 1982 kama taifa lako linapakana na bahari halafu kuna kisiwa ambacho ni taifa jingne kwenye umbali usiofika 12Neutical miles kitakachofanyika ni EQUIDISTANCE , yaani unapimwa umbali kati ya mataifa hayo mawili then unagawanywa kwa mbili ndio mpaka unawekwa. Umbali kutoka Bara hadi Zanzbar unakadiriwa kufikia mile 46. Kila nchi ikipima umbali wa mile 12 kutoka kwenye lower water mark yake, yaani kwenye pwani yake zitabaki mile 22. Hiyo ni teritorial sea. Ninavyosema territorial sea..namaanisha ni eneo ambalo taifa lina total control ya kila ki2., lina regulate who can pass na huwezi kuingia katika eneo hlo bila ya ruhusa kutoka taifa husika. Baada ya hapo inafuata Exclusive Economic Zone ambalo lina extend up to 200miles from the lower water mark. Umbali uliobaki kati yetu na zanzbar ambao ni 22miles hautoshi kwa kila taifa kujipatia 200miles, hvyo basi itafanyika EQUIDISTANCE yaani pasu kwa pasu. Kila taifa litapata 11miles. Kwa muktadha huo eneo la bahari kwa upande wa tanzania bara kwa maeneo ambayo ukomo wake unaishia zanzbar, litakuwa na urefu wa mile 23 pekee.
Kwa upande wa Zanzbar sasa,, upande wake wa pili ni bahari tu hivyo itapima 12 miles territorial sea pamoja na 200 miles Exclusive Economic zone. Kutoka 200 miles kwenda mbele huko ni high seas yaani eneo la kimataifa..nchi yeyote ina haki ya kuchukua chochote.

Nimetoa huo ufafanuzi mfupi ili hata layman aweze kujenga taswira kwamba picha ikoje.
Kwa sasa Mvuvi kutoka bara na mvuvi kutoka zanzbar wanaweza kuvua katika fishing ground moja bila ya tatozo lolote kwani tunatambulika kama nchi moja.

Muungano ukivunjika..amani itatoweka baharini, badala ya wavuvi kukutana na wavuvi wenzao..watakutana na polisi na manuaro za kijeshi zikilinda mipaka yao.
Ukichanganya wavuvi wote wa pwani ya bara ukilinganisha na kaeneo ka bahari ..haviendani , itabd wavuvi watafute kazi nyngne mbadala maana wakiingia wote baharn..ndan ya mwez hawatapata tena chochote kitu ambacho ni uharibifu wa mfumo wa ikolojia. Pia si rahisi kwa wao kukubaliana na hali, watavunja sheria kwa kutaka kwenda kuvua eneo la Zanzbar, Suala ambalo litazua mgogoro mzito na ndiyo mwanzo wa vita.

Mtazamo wangu kuyaepuka haya ni kuulinda muungano bila ya kuakisi au kushirikisha vyama vya kisiasa. Watu wasiwe wepesi wa kusema tunataka au hatutaki. Angalia gharama zake endapo utakuwe au hautakuwepo ipi afadhali.

Hapo nimezungumzia uvuvi peke ake..cjazungumzia gesi na mafuta kwamba itakavyogawanywa bahari..huwa inafuata vpmo na siyo mali..so gesi na mafuta zikiwa upande mmoja ...vita nyingne hyo ambayo is even worse . Tutafakari kuhusu muungano kwa kuangalia faida na hasara.
 
Penye HAKI amani itakuwepo tu. Wazanzibar wasipopata haki ya kumchagua kiongozi wamtakae ndani ya muungano wataitafuta haki hiyo nje ya muungano.
Magamba matatizo mnaanzisha wenyewe mtangazeni mshindi wa uchaguzi wa oct 25, na mkubali katiba ya wananchi ijulikane wazi tanzania ni nchi moja au mbili.
 
Asante sana kwa elimu hii. Naupenda muungano bila kujua haya. Huwa nakereka sana na watu ambao wanasema hawaoni faida za muungano, kumbe ni ufahamu tu hawana. Wakulaumiwa ni viongozi ambao wana elimu hii lakini hawawaelezi wananchi wao faida za muungano. Nakuomba uendelee kutujuza faida za muungano katika maeneo mengine pia ili sisi waumini wa muungano tuweze kuutetea kwa hoja.
 
Muungano usingekua tatizo kama kila taifa likawa linapata haki yake kisheria na kutambulika kama ni taifa na kila taifa kuwa na jeshi na sarafu yake na kila kitu chake na sio muungano wa kumezwa mazima ukabakia kuitwa jina tu lkn huna lolote upo upo tu unapelekwa pelekwa tu ama huo utakua sio muungano nadhani hilo ndo tatizo
 
Hakuna anayependa muungano uvunjike, ila kama ccm itaendelea kukandamiza demokrasia basi wananchi wataendelea kuhoji uhalali wa muungano kama njia ya kuonyesha chuki yao kwa ccm, na watakuwa tayari uvunjike. Kadiri nguvu kubwa inavyotumika kuulinda ndivyo uhalali wake utazidi kuhojiwa. Katiba mpya itatuondolea wasiwasi wa kuvunjika muungano.
 
Muungano usingekua tatizo kama kila taifa likawa linapata haki yake kisheria na kutambulika kama ni taifa na kila taifa kuwa na jeshi na sarafu yake na kila kitu chake na sio muungano wa kumezwa mazima ukabakia kuitwa jina tu lkn huna lolote upo upo tu unapelekwa pelekwa tu ama huo utakua sio muungano nadhani hilo ndo tatizo

Waliokosea ni walioondoa Tanganyika wakabakiza zanzibar. Tungekua tushazoea kuiona unguja kama tunavyoona Mafia
 
Ukichanganya wavuvi wote wa pwani ya bara ukilinganisha na kaeneo ka bahari ..haviendani , itabd wavuvi watafute kazi nyngne mbadala maana wakiingia wote baharn..ndan ya mwez hawatapata tena chochote kitu ambacho ni uharibifu wa mfumo wa ikolojia. Pia si rahisi kwa wao kukubaliana na hali, watavunja sheria kwa kutaka kwenda kuvua eneo la Zanzbar, Suala ambalo litazua mgogoro mzito na ndiyo mwanzo wa vita.
Ingawaje sipendi muungano uvunjike lakini hapo nilipo-highligh sio kweli hata kidogo. Ukichukua Mkoa wa Lindi peke yake, huu una karibu 1/3 ya pwani yote ya Tanzania na mkoa wa Lindi hauna ukaribu hata kidogo na Zanzibar. Ukichanganya kusini ya pwani ya mkoa wa Pwani ukachanganya na ile ya mkoa wa Lindi na Mtwara, hizi zina-make up almost 2/3 ya Pwani mzuri. Pwani inayoweza kukumbana na changamoto ni ile ya Tanga kutokana na ukaribu wake na Pemba.
 
kwa taarifa zenu watanganyika hamuna bahari. ikiwa munataka muungano basi haki iwepo hakuna haki basi musije kumlaumu mtu. nyiyi watanganyika muna kila kitu katika nchi yenu lakini kwa vile hamuna akili mutabaki hivyo hivyo tu masikini wa kutupwa na sasa munatafuta matatizo kwa kila njia kwa kusikiliza maneno ya kanisa haya twendeni lakini huko mbele mutakuja kujuta
 
yaani umuhimu wa muungano ni uvuvi. mbumbumbu kweli wewe. sababu pekee ya kuwepo kwa muungano ilikua ni kuilinda serikali ya mapinduzi ambayo ilikua dhaifu mno. kwa sasa hakuna faida yoyote l, hawa wazanzibari wanatunyonya tu hawana mchango wowote.
 
kwa taarifa zenu watanganyika hamuna bahari. ikiwa munataka muungano basi haki iwepo hakuna haki basi musije kumlaumu mtu. nyiyi watanganyika muna kila kitu katika nchi yenu lakini kwa vile hamuna akili mutabaki hivyo hivyo tu masikini wa kutupwa na sasa munatafuta matatizo kwa kila njia kwa kusikiliza maneno ya kanisa haya twendeni lakini huko mbele mutakuja kujuta
Graduate wa madrasa!
 
Mzee akili zipi unazoziongelea...coz wewe mwenye akili ata kuandika vizuri huwezi...Embu ona umeandika HAMUNA.....MUSIJE....MUNA...MUNATUTAFUTA....
 
Ingawaje sipendi muungano uvunjike lakini hapo nilipo-highligh sio kweli hata kidogo. Ukichukua Mkoa wa Lindi peke yake, huu una karibu 1/3 ya pwani yote ya Tanzania na mkoa wa Lindi hauna ukaribu hata kidogo na Zanzibar. Ukichanganya kusini ya pwani ya mkoa wa Pwani ukachanganya na ile ya mkoa wa Lindi na Mtwara, hizi zina-make up almost 2/3 ya Pwani mzuri. Pwani inayoweza kukumbana na changamoto ni ile ya Tanga kutokana na ukaribu wake na Pemba.
Nimekuelewa sana mkuu, ila Kenya ipo kaskazini mwa Pemba kilichofanyika ni equidistance, vivyo hivyo Zanzbar itapima mile miambili kuelekea kusini mwake na kama hazitoshi equidistance itachukua mkondo wake kwa hiyo kuwa na urefu mkubwa wa pwani bado itakuwa cyo kigeze cha kuwa na eneo kubwa la bahari. Bado tutakumbwa na geographical disadvantage.
 
Back
Top Bottom