Ushauri wangu kwa watu wa dini, na kwa hapa Muamsho
"Ya Ngoswe wamwachie Ngoswe".Si busara kwao kutumia
majukwaa ya kidini kufanya madai ya kisiasa. Madhara yake
tunayaona. Ijapokuwa nia yao ni nzuri na madai yao ni halali,
lakini jukwaa wanalotumia ni baya. Wanaweza kuifikisha
Zanzibar pabaya. Kama wana madai ya kisiasa, waunde chama
cha siasa chenyelengo la kuvunja Muunganona watapata wafuasi
wengi kutoka pande zote, kuliko kutumia dini ambapo matokeo
yake ni kuzipaka dini matope na kueneza chuki miongoni mwa
wafuasi wa dini mbali mbali.
BUSARA INAHITAJIKA ZAIDI KULIKO JAZBA