MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,244
- 7,966
Tunataka tume ya taifa ya uchaguzi ijitegemee yenyewe kusimamia zoezi la uchaguzi ifikapo 2020, tume ipeleke wawakilishi wake kwa kila wilaya na sio kuweka wakurugenzi wa halmashauri na manispaa kusimamia uchaguzi kuepusha biases.
Hatuwezi kua na uchaguzi huru na wa haki hata siku moja kuendelea kuwatumia makada wa wazi wazi wa chama tawala.
Hii sio fair kabisa na ndio maana wanawekwa makada watiifu wa chama kwa kila wilaya na manispaa kwa lengo mahsusi la kukilinda chama tawala wakati wa uchaguzi badala ya kuutumikia umma.
Yaani unaweka mwamuzi kuchezesha mechi ya Simba na Yanga huku yeye ni shabiki wa Yanga, hapa hapawezi kua na fair play ndio maana tunaona wachezaji wanafunga mabao ya mikono.
Hili lazima tulikatae kwa nguvu zote kabisa awamu hii. Wakurugenzi wabaki kufanya kazi zao na tume ya taifa ya uchaguzi nayo ifanya kazi yake. Tume iachane na kisingizio cha uhaba wa rasirimali watu, iajiri watu wa kutosha iwasambaze kila wilaya ili washughulike na uchaguzi tu na usndikishaji badala ya kuwatumia wakurugenzi.
Yaani eti Godfrey Kunambi aliyekua mwanasheria wa CCM ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa manispaa ya Dodoma asimamie uchaguzi kati ya CCM na UKAWA? Kuna fair play hapo? Tuache hizi siasa za kizamani tubadili mfumo huu uliozeeka ambao ulitumika enzi za chama kimoja.
Hawa wakurugenzi wanaotafuna pesa za michango ya maafa wataacha vipi pesa za bure za wanasiasa? Lazima ifike mahali raia tushtuke juu ya hili! Tusikubaliane na baadhi ya mambo ambayo mwisho wake tunaishaia kupata wawakilishi wabovu na kubaki kulalama tu.
Wapinzani hili suala msiliache tena lishughulikieni kwa upande kwenu muache kulia lia na sisi kama raia wazalendo lazima tutalidai hili hatuwezi kuliacha. Titalidai kokote ili haki itendeke sehemu zote.