Hatutaki kujirekebisha lawama kwenye mitandao ya kijamii

kipara kipya

JF-Expert Member
May 2, 2016
17,353
21,451
amani iwe kwenu waungwana

Tukiri wiki hii ndugu zangu ni wiki nyeusi iliokumbwa na matukio tofauti tofauti nchini mwetu na kubwa ni kupoteza askari wetu walinzi wetu na mashujaa wakiwa kazini,dakika moja ya maombolezo....
aksanteni

Nakuja sasa kwenye eneo ninalotaka kulisemea hivi sasa tanzania yetu kisiwa cha amani viongozi wetu wamekuwa ni waoga wa kukubali kukosolewa kwa makosa yao na kwa kibri hawataki kurekebisha makosa ili hali watu wanayaona na hawataki kufuata ushauri

Kubwa lililopo ni kulaumu mitandao ya kijamii hili la mitandao haliepukiki hata mimi niliyekuwepo kisiwani ukerewe ambae ni maskini kilio changu kinasikika na unakisoma ila ni jeuri na kibri hutaki kutatua tatizo

Kwakua wewe hutaki kutatua tatizo ushakua sehemu ya tatizo

tukianza na kiongozi mkuu wa nchi yeye anawapiga vijembe watu wa mitandao ya kijamii lakini sisi hufurahi tunajua ujumbe umegonga medula na lile tatizo hataki kuliondoa watu wakisema ukweli ni kejeli na udaku

Juzi limetokea tukio la maaskari kuuwawa viongozi wetu waandamizi badala ya kutafuta suluhu wao wamekwenda mbali na kuona kama hawa majambazi wapo humu kwenye mitandao ya kijamiiu na mmoja mwenye kutoa kauli hizo kipindi cha kampeni hakukauka humu na ni memba hivi sasa wanaona wanakejelia tu kwa kuambia makosa yao wayatafutie ufumbuzi kama viongozi

mbona humu kwenye mitandao mnachukua mabaya tu na kuna mazuri na mkishayakopi hamtoi shukrani kwenye mitandao, kuna vichwa timamu ndio maana kila mkilinganisha na yenu mnakiri makosa kimoyomoyo na kuzigeuza ni kejeli

Labda niseme kwenye mitandao ya kijamii kuna sheria na kanuni kama ni kejeli kwa serikali au nchi hata sekunde tano haidumu hewani wewe memba unalijua hilo ila umeamua tu kulipindua kumfurahisha mkuu sababu hapendi mitandao ya kijamii lakini kutwa anaperuzi

Kumbukeni humu mnapotaka kuwashughulikia kama wahalifu ndimo tulipowafahamu mimi huku ukerewe nilikuwa siwafahamu

Kwenye kampeni ilikuwa sio kejeli leo kushauriwa mfanyaje na kujirekebisha ni kejeli basi mtakamata watu wote kama mtaendelea hivyo kwa sababu kila eneo ni lawama

Labda mitandao ife au muifunge ila penye kosa patasemwa bila woga

Hakuna mikusanyiko mpaka 2020

aksanteni
 
Kipara eeh kwanza makofi kwa mkurugenzi melo pili kwa mods wote tatu kwa wapenda ukweli hata wakikumata dhamana juu yangu wewe wambie ukweli kurudi nyuma mwiko
 
Watakuwa wamekuelewa.Tatizo hawqtaki kusikia mawazo mbadala yaani mpaka sasa hawajui kuwa mawazo mbadala uwaga yanakuwaje yaweza kuwa yenye kejeli,au hata matusi lkn hiyo yote inakuwa na ujumbe.watu hawapendi polisi wanavyoumia na kufa ndio maana uchukia mpaka kutoa lugha kali.Ukweli Mangu anatakiwa ajiudhuru ameshindwa kabisa kulifanya jeshi letu liwe la kiwango yaani popote pale askari amepata mafunzo na ana silaha wanauwawa kinyama vile na kuchukua silaha.hapana aikubariki sawa tuwape pole ila sio jambo zuri.kiwango hicho ni kikubwa mno tena kwa watu walio na mafunzo.Inakuwa kama movie za kikorea
 
Wakiambia ukweli wananuna mwinyi aliwahi kujiuzulu fuateni mfano
 
Kipara eeh kwanza makofi kwa mkurugenzi melo pili kwa mods wote tatu kwa wapenda ukweli hata wakikumata dhamana juu yangu wewe wambie ukweli kurudi nyuma mwiko
Ukiona viongozi wanatupa shutuma kwa wanaowaongoza hiyo ni dalili ya kushindwa!
 
Back
Top Bottom