Hatuna haja ya kuleta wataalamu kutoka Misri kujifunza umwagiliaji

Hakuna shaka kwamba Misri ndio babu wa umwagiliaji duniani. Hata hivyo tumeshajifunza kitambo toka kwao, na hata sehemu nyingine duniani kwamba umwagiliaji ni uhandisi unaotaka uwekezaji wa kutosha!

Siasa tamu za kusema wataalamu watanzania wanaweza kunufaika na ziara ya Rais wa Misri kwa kwenda kujifunza wenzetu wao walivyofanikiwa kwenye umwagiliaji ni upuuzi!

Inajulikana tatizo letu ni fedha, sio wataalamu!Tunao wabobezi wa umwagiliaji kila kona, kuanzia wizarani mpk ngazi ya kata!Wapo magwiji wa umwagiliaji vyuo vikuu wakiongozwa na SUA!

Wataalamu hawana cha kujifunza kutoka Misri, serikali inatakiwa ijifunze kutoa hela za umwagiliaji na isirushe mpira wa kitoto! Serikali haijawahi kutoa pesa za umwagiliaji kulingana na usanifu, nimefanya utafiti wa miradi kadhaa na kugundua serikali hutoa wastani wa chini ya 30% ya fedha ya usanifu wa mradi wa umwagiliaji, ndio maana hakuna mradi wa umwagiliaji uliojengwa ukakamilika toka Nyerere astaafu.

Kwa mito tuliyonayo, maziwa na mabwawa hakika Tanzania inatakiwa iwe mzalishaji mkuu wa mazao ya biashara na chakula duniani!Tanzania ni kati ya nchi zenye maji mengi zaidi yanoyofaa kwa kilimo cha umwagiliaji lakini ndio kati ya nchi zinazotumia umwagiliaji kwa kiwango cha chini kabisa!

Mpaka njaa itukomeshe, au mpaka apatikane kiongozi anayejua chakula ni kipaumbele cha kwanza ndipo tutakapopiga hatua! Hizi za kunufaika kutoka Misri ni siasa tamu za mgongo wa chupa!

Mtendahaki

Moja ya shida kubwa ya nchi nyingi za Afrika ni kujifanya hawajui tatizo la umaskini wao. Ndio maana usishangae kiongozi mmoja anauliza kwanini wanafunzi wanafeli, au anawasumbua maafisa elimu kwa wanafunzi kufeli. Tumekuwa wepesi kutibu dalili badala ya kiini cha tatizo. Hata mie siamini kama tunashida ya wataalamu wa umwagiliaji, shida yetu ni tumewekeza kiwango gani kwenye sekta hiyo ya umwagiliaji?
 
This is the poorest argument of the day, unataka kufanya mass production kwa maigizo ya kupooza njaa??
Yale yale ya usomi koko.Hivi unaelewa maana ya mass production au ulikariri notisi? Mass production ni uzalishaji mkubwa wa kukidhi bidhaa za kutosha watu wengi.Sasa kijiji chenye watu elfu moja ukiweza kuanzisha mradi wa umwagiliaji wa chakula cha kuwaweza kulisha hao mass elfu moja na ziada wakauza hiyo sio mass production? YOU are producing for masses of people be it in a village or whatever.Wasomi kama nyie mwafaa tu kuweko kwenye mikutano ya kisiasa hasa ya CHADEMA NA SIO KWENYE FIELD ZA KITAALAMU zinazohitaji matumizi ya vichwa kumatch mtu alichosoma na uwezo wa kuTOLEA majibu ya changamoto za mazingira zilizopo kwa kutumia raslimali chache zilizopo
 
Kama hatutaki huo utaalamu kutoka Misri ndo tunapaswa kujiongeza na kutumia utaalamu wa kwetu.
Utaalamu wetu tumekaa nao, tumeukalia ndio maana hauonekani.
Tukilia lia tu kila siku na kulaumu Serikali hatutafika popote.
Watendaji wakuu ni sisi wenyewe.
kwanza jiografia ya misri na kwetu ni tofauti sana, wao wako mediteranian sio tuko tropical aina ya kilimo ni tofauti mbinu za kilimo tofauti majira vilevile, haya leo hii trekta linauzwa milioni hamsini, wakulima wangapi wanamudu? hatakama ninazo kwanini nisinunue fuso la mchanga kwa pesa ileile likaniingiza pesa kuliko hicho kilimo cha mkataba na Mungu?
 
Pesa yote anapeleka kujenga uwanja wa ndege Chato na kununua midege kwa pesa taslim, wakati angewekeza kwenye kilimo cha umwagiliaji tungekuwa mbali sana.
Watanzania tunapigwa changa la macho

Sent using Jamii Forums mobile app
Nyie watu sijui mleogwa na nani
Mwanzo mlisema kipaumbele ni elimu elimu elimu,sasa mmerukia kilimo
 
Hali ya hewa hairuhusu kwenda shamba kulima kupanda na kupalilia utegemee mavuno, at that times mvua ilikuwa inatosha, but not now!Its erratic and non predictable ndio maana kila mwaka wakulima wanalia mazao kukauka
wakati wetu mvua ilikuwa mil 1700 hadi leo ni mil zile zile hazijawahi pungua unaposema mvua hazipo sio kweli labda utaalamu ndio haupo,
 
Yeah hata kule ambako Wahandisi wameshtukizwa na kuonekana wamefanya kaz chini ya kiwango ni kwa sababu hela zinazotolewa ni chini ya actual design parameters. Haiwezekani na haitakaa itokee utake kitu kizuri na imara halafu bajeti ikiwa finyu. Kila kitu kizuri kina gharama zake. Ila kwa kuwa tunapenda quantity bila ya quality,hapo ndipo shida inapoanza.
Niseme wazi wataalamu wengi tulionao ni twegemezi miradi wanayoiweza ni government projects tu na sana sana Donor projects za donors wa nje. Ambazo lazima ziwe na pesa toka serikalini au kwa donors wa nje.Ndio maana kilio chao muda wote ni hela hela hela!!!!

Wataalamu wetu wengi ni zero kwenye community projects ambako jamii husika yenye tatizo liwe la mabwawa kilimo cha umwagiliaji nk huhusika. iKO HAJA vyuo vyetu kuweka mitaala yao vizuri na kuweka msisistizo mkubwa kwenye community projects.
 
Hakuna shaka kwamba Misri ndio babu wa umwagiliaji duniani. Hata hivyo tumeshajifunza kitambo toka kwao, na hata sehemu nyingine duniani kwamba umwagiliaji ni uhandisi unaotaka uwekezaji wa kutosha!

Siasa tamu za kusema wataalamu watanzania wanaweza kunufaika na ziara ya Rais wa Misri kwa kwenda kujifunza wenzetu wao walivyofanikiwa kwenye umwagiliaji ni upuuzi!

Inajulikana tatizo letu ni fedha, sio wataalamu!Tunao wabobezi wa umwagiliaji kila kona, kuanzia wizarani mpk ngazi ya kata!Wapo magwiji wa umwagiliaji vyuo vikuu wakiongozwa na SUA!

Wataalamu hawana cha kujifunza kutoka Misri, serikali inatakiwa ijifunze kutoa hela za umwagiliaji na isirushe mpira wa kitoto! Serikali haijawahi kutoa pesa za umwagiliaji kulingana na usanifu, nimefanya utafiti wa miradi kadhaa na kugundua serikali hutoa wastani wa chini ya 30% ya fedha ya usanifu wa mradi wa umwagiliaji, ndio maana hakuna mradi wa umwagiliaji uliojengwa ukakamilika toka Nyerere astaafu.

Kwa mito tuliyonayo, maziwa na mabwawa hakika Tanzania inatakiwa iwe mzalishaji mkuu wa mazao ya biashara na chakula duniani!Tanzania ni kati ya nchi zenye maji mengi zaidi yanoyofaa kwa kilimo cha umwagiliaji lakini ndio kati ya nchi zinazotumia umwagiliaji kwa kiwango cha chini kabisa!

Mpaka njaa itukomeshe, au mpaka apatikane kiongozi anayejua chakula ni kipaumbele cha kwanza ndipo tutakapopiga hatua! Hizi za kunufaika kutoka Misri ni siasa tamu za mgongo wa chupa!

Mtendahaki
Kimsingi umenena vyema. Kwa upande wangu naona tatizo ni mitazamo ya watawala, kwani wanadhani umwagiliaji ni kusemasema maneno tu na kwamba mtu yoyote binafsi anaweza tengeneza miundombinu ya umwagiliaji
Ileweke kuwa uwekezazaji katika miundombinu ya ya umwagiliaji inahitaji uwekezaji mkubwa wa serikali kama ilivyo katka miradi ya barabara, reli, bandari, mabomba ya mafuta/gesi nk.
 
Niseme wazi wataalamu wengi tulionao ni twegemezi miradi wanayoiweza ni government projects tu na sana sana Donor projects za donors wa nje. Ambazo lazima ziwe na pesa toka serikalini au kwa donors wa nje.Ndio maana kilio chao muda wote ni hela hela hela!!!!

Wataalamu wetu wengi ni zero kwenye community projects ambako jamii husika yenye tatizo liwe la mabwawa kilimo cha umwagiliaji nk huhusika. iKO HAJA vyuo vyetu kuweka mitaala yao vizuri na kuweka msisistizo mkubwa kwenye community projects.
haohao ukiwakuta kwenye maonyesho ya nanenane utashangaa nchi hii njaa sijui inatokea wapi?
 
Nyie watu sijui mleogwa na nani
Mwanzo mlisema kipaumbele ni elimu elimu elimu,sasa mmerukia kilimo
Huoni elimu inaendana na kilimo? hujui kuna elimu ya kilimo??

Unakimbilia viwanda malighafi utapata wapi wakati kilimo kimedumaa??
 
unauhakika na hiki ulichogandamizia RED?

Vipi lower moshi irrigation scheme?
Vipi dakawa irrigation scheme?

Kapunga?
Kilosa?
name them.........................
HIZI ZOTE ENZI ZA NYERERE. CHUNGUZA NA ALILIONA HILI BAADA YA NJAA YA 1974 NDIO IKAANZA IDARA YA UMWAGILIAJI NA KUJENGA MIPYA NA KUBORESHA YA ZAMANI ? Baada ya hiyo uliyotaja tueleze ni ipi baada ya huyo mzee yaani toja 1995
 
Mababu walikuwa wanazalisha nn cha kuuza nje??Enzi hizo kihenge kimoja tu kilitosha kuvuka mwaka!To this population bro ambayo inaongezeka kwa kutegemea wakulima wanaojikimu!
Hapa ndipo sasa tunatakiwa kutumia ujuzi na elimu zetu kuzidisha mara mamilioni kile walichofanya.
Haiwezekani na haikubaliki kizazi hiki kushindwa kuzalisha chakula cha kutosha huku wachache kwa jina la siasa wakiishi maisha ya kifahari kwa jasho la wasioshiba.
Kwanza tuzalishe cha kutosha watu wetu ndipo tuwaze kuexport.
 
Hakuna shaka kwamba Misri ndio babu wa umwagiliaji duniani. Hata hivyo tumeshajifunza kitambo toka kwao, na hata sehemu nyingine duniani kwamba umwagiliaji ni uhandisi unaotaka uwekezaji wa kutosha!

Siasa tamu za kusema wataalamu watanzania wanaweza kunufaika na ziara ya Rais wa Misri kwa kwenda kujifunza wenzetu wao walivyofanikiwa kwenye umwagiliaji ni upuuzi!

Inajulikana tatizo letu ni fedha, sio wataalamu!Tunao wabobezi wa umwagiliaji kila kona, kuanzia wizarani mpk ngazi ya kata!Wapo magwiji wa umwagiliaji vyuo vikuu wakiongozwa na SUA!

Wataalamu hawana cha kujifunza kutoka Misri, serikali inatakiwa ijifunze kutoa hela za umwagiliaji na isirushe mpira wa kitoto! Serikali haijawahi kutoa pesa za umwagiliaji kulingana na usanifu, nimefanya utafiti wa miradi kadhaa na kugundua serikali hutoa wastani wa chini ya 30% ya fedha ya usanifu wa mradi wa umwagiliaji, ndio maana hakuna mradi wa umwagiliaji uliojengwa ukakamilika toka Nyerere astaafu.

Kwa mito tuliyonayo, maziwa na mabwawa hakika Tanzania inatakiwa iwe mzalishaji mkuu wa mazao ya biashara na chakula duniani!Tanzania ni kati ya nchi zenye maji mengi zaidi yanoyofaa kwa kilimo cha umwagiliaji lakini ndio kati ya nchi zinazotumia umwagiliaji kwa kiwango cha chini kabisa!

Mpaka njaa itukomeshe, au mpaka apatikane kiongozi anayejua chakula ni kipaumbele cha kwanza ndipo tutakapopiga hatua! Hizi za kunufaika kutoka Misri ni siasa tamu za mgongo wa chupa!

Mtendahaki

Hujui ulichokiandika. Ungejua tatizo letu kubwa si pesa ila utaalamu usingenena haya. Nikuulize swala dogo tu, Hivi mlolongo wa kudumu wa umwagiliaji uko vipi toka hatua ya mwanzo mpaka mwisho.

Hawa wamisri wako mbali sana katika suala la umwagiliaji, si zungumzii suala la nadharia ya kujua hiyo sekta nahitaji kwa vitendo.

Narudia tena SITAKI DISTINCTION ZA SUA JUU YA UMWAGILIAJI NATAKA UMWAGILIAJI KWA VITENDO.

Ukitaka kuelewa ninachokueleza waulize vijana wa DIT (FTC) na wahandisi wa chuo kikuuu wanapokutana kazini. Sina mengi.
 
Hapa ndipo sasa tunatakiwa kutumia ujuzi na elimu zetu kuzidisha mara mamilioni kile walichofanya.
Haiwezekani na haikubaliki kizazi hiki kushindwa kuzalisha chakula cha kutosha huku wachache kwa jina la siasa wakiishi maisha ya kifahari kwa jasho la wasioshiba.
Kwanza tuzalishe cha kutosha watu wetu ndipo tuwaze kuexport.
unachosema ni sahihi kabisa, nikupe mfano katika magereza yetu kuna wababa wana afya na nguvu za kutosha utashangaa wanafanyakazi za kukatia maua! halafu tunaambiwa jkt wamepokonywa shamba kwa kushindwa kuliendeleza, kweli? hawa vijana elfu 30 waliotapakaa kwenye magereza nchini kwanini wasitumike kwenye uzalishaji mali badala ya kukatia maua na kusenya kuni? leo hii tukianzisha mradi wa ushirikiano kati ya JKT na Magereza, mbona njaa itakuwa historia.
 
Tulishafanya kilimo kwanza kwa miaka 10,ni wakati sasa wa kuchakata mazao ya kilimo viwanda

Halafu kabombe tunaomba tuheshimiane, ujue wakati wa utani na muda watu wanajadili mambo ya msingi. Kilimo kwanza kwa power tiller? Heshima ni kitu cha bure.
 
Back
Top Bottom