Hatuna haja ya kuleta wataalamu kutoka Misri kujifunza umwagiliaji

unauhakika na hiki ulichogandamizia RED?

Vipi lower moshi irrigation scheme?
Vipi dakawa irrigation scheme?

Kapunga?
Kilosa?
name them.........................
Mara ya mwisho umefika lini lower Moshi. Halafu kwa taarifa yako Lower Moshi ilikuwa ni msaada wa Japan ndio maana walimaliza. Lakini sasa ukifika lower Moshi ni jalala

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu, well said!! hata kwenye ile thread ya jana ya Rais wa Misri kuna mtu nilimpinga kwa hii hoja ya kujifunza. Hii lugha ya kila kitu eti tujifunze kwa wenzetu naona inatudharirisha sana.

Anyway, hapo nilipokuquote, nafikiri tatizo letu siyo kuwa hatuna pesa bali ni priorities!! Imagine kama pesa za Boeing Dreamliner zingepelekwa kwenye kilimo ingekuwaje!!? Kilimo chetu kinazidi kuzorota badala ya kuimalika!! Binafsi huwa nalinganisha na enzi zile za late 70s na early 80s nilipokuwa mdogo tukiwenda likizo kuwasalimia Bibi na babu kijijini, kwa kweli ukilinganisha na sasa utaona ni kiasi gani uzalishaji ulivyoshuka. AT LEAST KIJIJINI KWETU!!

Awamu hii wanadai VIWANDA ............. tatizo kama hakuna mali gafi, viwanda ni ndoto za mchana!!
True, tunaota mchana kweupe
 
Mkuu, tatizo letu kuwa ni kuwa hakuna government initiatives na lack of vision!!

Hivi kweli kati ya viwanda na kilimo kipi kilitakiwa kiwe kipaumbele chetu kwanza!!? Nchi ya 70 % wakulima, over 80 % elimu ya msingi ........... Seriously!!?
Tulishafanya kilimo kwanza kwa miaka 10,ni wakati sasa wa kuchakata mazao ya kilimo viwanda
 
Tatizo sio pesa wala utaalamu, tatizo ni uvivu, hao wamisri unafikiri kila kitu wanafanyiwa na serikali, huko lazima ujitume lasivyo utakufa njaa, hakuna biashara ya kupigana mizinga mchana kutwa. Watu wao wanajituma. Chukua mfano mwanza, unakuta mtu anaishi pembeni ya ziwa halafu anakwambia ana njaa. hata akitumia kopo kumwagilia anaweza kupata chakula lakini unamkuta anashinda chini ya mti kula miwa tu.
 
Mkuu, tatizo letu kuwa ni kuwa hakuna government initiatives na lack of vision!!

Hivi kweli kati ya viwanda na kilimo kipi kilitakiwa kiwe kipaumbele chetu kwanza!!? Nchi ya 70 % wakulima, over 80 % elimu ya msingi ........... Seriously!!?
70% wakulima ilikua enzi za nyerere, sasa 70% wamekua solar panel, mchana kutwa wamekaa vijiweni wanaota jua.
 
Mbowe amejaribu wameharibu miundombinu.Kama kujifunza wangeenda hata kwenye Mashamba ya Mbowe badala ya kuyaharibu
nitumie namba ya mbowe niwasiliane nae sie huku tunahitaji kweli huo mradi tutampa shamba bure na vijana wakumsaidia wapo tele,
 
unauhakika na hiki ulichogandamizia RED?

Vipi lower moshi irrigation scheme?
Vipi dakawa irrigation scheme?

Kapunga?
Kilosa?
name them.........................
Najua ninachosema:
Lower Moshi - 1930 (British - wakoloni) mpk leo haujakamilika
Dakawa -1981 (North Korea) mpk leo haujakamilika
Kapunga - initiated 1983, started 1988 mpk leo haujakamilika
Kilosa hata usiongelee, naijua nje ndani hakuna mradi wa maana, sio mvumi irrigation scheme, wala Idodi or mention whatever!
Hakuna mradi ambao serikali imejenga ukaisha, full stop
 
Eti wataalam wetu wanasema hawapewi pesa.Kukusanya vijana 100 wakachimba mtaro,wakafanya kazi kwenye shamba husika la mpunga wakalipwa kutokana na mavuno nako kunahitaji pesa gani?halafu mtu anajiita msomi

Tatizo linaanzia juu mpaka chini. Viongozi wa kisiasa Hawajui nchi ina nini na watu wenye ujuzi au uwezo gani na vinaweza kutumika vipi.
Vivyo hivyo wasomi H awajui watumie vipi usomi wao, na mara nyingi wanafikiri kazi yao ni kuratibu miradi inayobuniwa na kufanywa na wageni.
 
Sasa sijui tunahitaji nini, maana kila Juhudi ifanywayo inabezwa.
Heri kenda shika kuliko kumi nenda rudi.
Tujiongeze.
 
70% wakulima ilikua enzi za nyerere, sasa 70% wamekua solar panel, mchana kutwa wamekaa vijiweni wanaota jua.
weacha tu vijana wote wanendesha bodaboda na vibanda vya kunyoa nywele, huu mradi wa rea umeme unatumiaka kuchaji simu na kuchoma nyimbo kwenye memory card, wanaolima ni vibibi tu huko vijijini,
 
Umeandika andiko la mwaka huu. Yaani uliyo ongea yako wazi 100% mimi ni mmoja wa waathirika wa sera za kilimo cha Tanzania. Professional yangu ni drip irrigation. Lakini ukiingiza vifaa vya umwagiliaji wa matone TRA hawajui kipi ni kipi watakuambia lazima hiki ulipie yaani siasa kila mahali. Ina kera. Inaudhi sasa nimeamua kukaa kimya ili roho yangu iwe na amani

Sent using Jamii Forums mobile app
Serikali inapiga porojo, wanasiasa wanapiga porojo za umwagiliaji wakati hawaujui!Wao ndio waende China, Japana, Israel na Egypt wakajifunze namna wenzao wanavyowekeza pesa za kutosha kwenye miundombinu ya umwagiliaji
 
Sasa sijui tunahitaji nini, maana kila Juhudi ifanywayo inabezwa.
Heri kenda shika kuliko kumi nenda rudi.
Tujiongeze.
Utakuwa hujaelewa nilichoandika, sual la kubeza halipo hapo hili ni suala la maslahi mapana ya wananchi maskini
 
Hakuna shaka kwamba Misri ndio babu wa umwagiliaji duniani. Hata hivyo tumeshajifunza kitambo toka kwao, na hata sehemu nyingine duniani kwamba umwagiliaji ni uhandisi unaotaka uwekezaji wa kutosha!

Siasa tamu za kusema wataalamu watanzania wanaweza kunufaika na ziara ya Rais wa Misri kwa kwenda kujifunza wenzetu wao walivyofanikiwa kwenye umwagiliaji ni upuuzi!

Inajulikana tatizo letu ni fedha, sio wataalamu!Tunao wabobezi wa umwagiliaji kila kona, kuanzia wizarani mpk ngazi ya kata!Wapo magwiji wa umwagiliaji vyuo vikuu wakiongozwa na SUA!

Wataalamu hawana cha kujifunza kutoka Misri, serikali inatakiwa ijifunze kutoa hela za umwagiliaji na isirushe mpira wa kitoto! Serikali haijawahi kutoa pesa za umwagiliaji kulingana na usanifu, nimefanya utafiti wa miradi kadhaa na kugundua serikali hutoa wastani wa chini ya 30% ya fedha ya usanifu wa mradi wa umwagiliaji, ndio maana hakuna mradi wa umwagiliaji uliojengwa ukakamilika toka Nyerere astaafu.

Kwa mito tuliyonayo, maziwa na mabwawa hakika Tanzania inatakiwa iwe mzalishaji mkuu wa mazao ya biashara na chakula duniani!Tanzania ni kati ya nchi zenye maji mengi zaidi yanoyofaa kwa kilimo cha umwagiliaji lakini ndio kati ya nchi zinazotumia umwagiliaji kwa kiwango cha chini kabisa!

Mpaka njaa itukomeshe, au mpaka apatikane kiongozi anayejua chakula ni kipaumbele cha kwanza ndipo tutakapopiga hatua! Hizi za kunufaika kutoka Misri ni siasa tamu za mgongo wa chupa!

Mtendahaki
kwahiyo SUA wameshindwa kuzalisha wataalamu hadi tuagize misri?
 
Najua ninachosema:
Lower Moshi - 1930 (British - wakoloni) mpk leo haujakamilika
Dakawa -1981 (North Korea) mpk leo haujakamilika
Kapunga - initiated 1983, started 1988 mpk leo haujakamilika
Kilosa hata usiongelee, naijua nje ndani hakuna mradi wa maana, sio mvumi irrigation scheme, wala Idodi or mention whatever!
Hakuna mradi ambao serikali imejenga ukaisha, full stop
Hayo unayosemankuhusu Kilosa, yote kweli tupu. Hamna kitu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
weacha tu vijana wote wanendesha bodaboda na vibanda vya kunyoa nywele, huu mradi wa rea umeme unatumiaka kuchaji simu na kuchoma nyimbo kwenye memory card, wanaolima ni vibibi tu huko vijijini,
Ipo siku hao watakosa chakula cha kununua ndipo tutakapoona mchele wa plastiki una maana
 
Eti wataalam wetu wanasema hawapewi pesa.Kukusanya vijana 100 wakachimba mtaro,wakafanya kazi kwenye shamba husika la mpunga wakalipwa kutokana na mavuno nako kunahitaji pesa gani?halafu mtu anajiita msomi

mkuu huyo mleta mada ni mtaalamu koko asiye na mbinu mbadala.Kila siku ni kupiga yowe pewsa serikali itoe pesa!!!! Huyu mleta mada na wenzie waliosoma ambao elimu zao haziwezi buni mbinu mbadala za kutatua changamoto za kilimo cha umwagiliaji AANGALIE huyu mwenzie wa India AMBAYE mjadala wake tuliweka humu ambaye kafanya maajabu wakati hajawahi soma kilimo na anasifika dunia nzima

Habari nzima hii ya huyo mhindi ilivyojadiliwa Jamii forums hii hapa chini
Rais Magufuli akatembelea kijiji cha Hiware Bazar kilichoko India
 
Eti wataalam wetu wanasema hawapewi pesa.Kukusanya vijana 100 wakachimba mtaro,wakafanya kazi kwenye shamba husika la mpunga wakalipwa kutokana na mavuno nako kunahitaji pesa gani?halafu mtu anajiita msomi
Umwagiliaji ungekuwa kuchimba hiyo mitaro kama ya barabara, basi kuna haja gani ya kwenda Egypt??
 
28 Reactions
Reply
Back
Top Bottom