Hatumtaki Mtendaji wa Kata ya Kwakilosa mkoa wa Iringa, tunaomba Serikali ya mkoa iingilie kati suala hili

MTAKA HABARI

Senior Member
Jan 17, 2019
123
149
Sisi wananchi wa kata ya Kwakilosa iliyopo manispaa ya Iringa tunanyanyasika na mtendaji wetu wa kata aitwaye Upendo Msafiri Amulike kwanza ana majibu mabaya kwetu wananchi na tukiuliza kuhusu mapato ya kata anakuwa mbishi.

Wananchi wamekuwa wakipigwa faini kwa habari ya ishu ya usafi lakini ukiuliza kuhusu matumizi ya pesa haieleweki na amekuwa ni mtu ambaye haeleweki na ni mjanja sana kwa mambo ya kifedha.

Pia wakati wa uchaguzi akiwa kama msimamizi wetu wauchaguzi alitujibu vibaya hasa alipoiba fedha za uchaguzi na kudai ameibiwa, ni muongo.

Hatumtaki huyu mtendaji Upendo Amulike asimamishwe kazi na ahamishwe hapa kata ya Kwakilosa. Wakati wa ziara za mkuu wa mkoa alipofika kwenye kata tulitoa hili lalamiko lakini ilionekana muda umekwishwa.

Hatumtaki huyu mtendaji na mara nyingi amekuwa akiwasema vibaya watendaji wa mitaa kwa mkurugenzi hadi kusababisha baadhi ya watendaji wa mitaa kuhamishwa na mkurugenzi, amekuwa ni tatizo huyu mtendaji na mara nyingi anatutishia sana kwa cheo chake.

Naomba uongozi wa mkoa wa Iringa uingilie kati madai yetu kwa huyu mtendaji wa kata Bi. Upendo Msafiri Amulike kwa kweli hatumtaki tutafutieni mtendaji mwingine.
 
Watendaji wengi wa serikali ni miungu watu, ukifuatilia zaidi utapigwa viboko.
 
Peleka malalamiko yako kwa Mkurugenzi wa manispaa. Mamlaka ya kinidhamu kwa mtu kama huyo inaishia kwenye level ya halmashauri tu otherwise useme ulishapeleka malalamiko yako na hayajafanyiwa kazi.
 
Hamumtaki kwani mlimchagua ninyi? Mmemwambia hamumtaki akasemaje? Mnashindwa nini kumwachia Mungu ili yeye ndo awatetee?
 
Bela vanyalukolo ndauli?Hamumtaki mtoto mzuri Pendo?Eee..nyeee!Ngoja mletewe malaika na bwana Njovu.Ni vema amletee Afisa Utumishi Bwana.Umar Mkangama awe Mtendaji wenu. Je, mtampenda je tukimleta au mtagoma akifika? (Tumia sauti ya Mike Tee unavyosoma).
 
Uzuri wake hautuhusu anatunyanyasa wananchi tumeshalalamika kwa mkurugenzi hakuna jipya nadhani hatujuhi kama sisi ni wahehe wa Iringa
 
Watendaji wengi wa serikali ni miungu watu, ukifuatilia zaidi utapigwa viboko
Kabisa wapo kama miungu watu tangu wapewe rungu na Rais Ikulu tunanyanyasika wananchi.

Wahehe tunanyanyasika na huyu binti mdogo
 
Dalili za uchawi hizi, acha uchawi ndugu yangu, malipo huwa Ni hapa hapa duniani, utakumbuka hii kauli siku moja.
 
Back
Top Bottom