Hatuhitaji kuwatangazia watu jina la mtoto

Hatuhitaji kuwatangazia watu jina la mtoto

Joined
Dec 4, 2018
Posts
15
Reaction score
28
Mungu amewabariki mmepata mtoto. Mkamwita jina ambalo limewapendeza kama wazazi. Watu wanapokuja kuwasalimia mnawaeleza jina la mtoto wenu. Taratibu jina linakua na hatimaye mtoto mwenye jina anajitambua. Analitangaza kwa watu yeye mwenyewe. Akiulizwa jina lako nani? Anasema naitwa Mwigamba Muchimati. Ninyi kama wazazi hamhitaji tena kuwa mnawaambia watu wanaowatembea juu ya jina la mtoto. Ataulizwa na atasema mwenyewe. Naitwa Mwigamba Muchimati.

Katika mazingira fulani fulani kama wazazi mtalazimika kutaja jina la mtoto wenu kwa watu au kwenye mamlaka fulani. Lakini halitafanyika kwa nguvu kubwa. Jina la mtoto litatangazwa na mtoto mwenyewe. Atatoka hadharani na kujisemea mwenyewe.

Kwanini sasa tutumie nguvu nyingi kumsemea mtu ambaye yupo na ana afya njema? Mtu mzima hujisemea mwenyewe. Na hata kama kuna hitilafu ya afya kidogo, kipi kipya kusema Mwigamba Muchimati anaumwa. Kwani huyu Muchimati ni malaika asiyeumwa? Mwanadamu gani duniani hajawahi kuumwa ili aninyooshee kidole mimi Muchimati kwamba naumwa? Tunaumwa sote na tutakufa wote. Dhambi gani kusema tunaumwa?

Inafikia kukamatana na kutishana eti tunatangaza habari za uongo. Huyu Mwigamba Muchimati aliyezushiwa uongo wa ugonjwa ilhali ni mzima au kifo ilhali yu hai, anao uwezo wa kujitokeza hadharani bila kumjibu mtu na kuendelea kufanya shughuli zake. Hayo ni majibu tosha kwa hao wazushi, kuna haja ya kutishana na kupeana kesi kweli hapo?

Asanteni.
 
Wakawaita wazazi wake. Wakawauliza "eti ni kweli mwana wenu alizaliwa kipofu na Yesu ndiye amemponya?" Wazazi wake wakajibu, "sisi tunajua kuwa alizaliwa kipofu, kuhusu kuponywa na Yesu hatujui. Huyo ni mtu mzima, anaweza KUJIELEZA MWENYEWE, muulizeni"
Yes, Mungu yupo anaponya. Na mipango yake haipanguliwi kwa hila za wanadamu.

Alikusudia apigwe afe na akazikwe haraka hata Kama ni usiku na maiti yake isiagwe. Aka survive, qmmk. Yu hai mpaka leo. Very shame.

Hajaomba hata maji ya kunywa.

World order, we must obey all of us.
 
Back
Top Bottom