Hatufanyi jaribio kuingia kwenye ndoa

unataka umtume wapi tena



Mara mbili tu.
Kijana wa Musoma na mmoja wa Kigoma.
Tulienda Singida na safari nyingine Dar.(ni kazi ya dharura)

Hekima inahitajika sio kazi rahisi hasa kumnadi kijana anayetoka Mkoa wa Mara wengi wanafikiri Mkoa huo woote ni Wakurya.

Uelewa mdogo kwa jamii kutoka kabila moja kwenda lingine ni tatizo na vyaweza geuka kuwa Kizuizi ila kwa wataalamu wa shortcut hilo sio gumzo kwao.

Kazi nyepesi ukiwa na Kijana anayeuzika kwa Maadili n.k
Wakimtazama Mshega sura ni kijana Busara/Hekima ni za mtu aliyekula CHUMVI nyingi.

Mwisho wa yote kicheko kwa pande zote mbili utayaona Meno 32 nje nje.
 
Nimekupata mkuu
 
mkuu umedadavua vema kabisa,,, na umenukuu wako wachache sana!!!!....means wengi ni maboya au vimeo, na ndoano nyingi haziwe fika mbali.... tufanyaje?
 
Inashauriwa Vijana au wawili wanapokubaliana sasa tuingie kwenye ndoa,


1.Binti/Mwanamke anapaswa kujua ni wakati wa kumlinda ili isigeuzwa kama hio ndio nafasi yakutajirika kupitia huyo mume mtatajiwa.


2.Kwa suala mahari wana familia wa upande wa binti/mke mtarajiwa wajue hawako sokoni kumwuuza binti yao bali muoaji atatoa mahari kama njia ya kusema asanteni sana kumtunza huyu mrembo mpaka nami nimemwona anifaa awe wangu wa Maisha.

3.Mambo haya hutofautiana kutoka kabila moja hadi kabila jingine,Wengine unapofika wakati wa vijana kuoa au kuolewa udhania ni kuuza ama kununua.Hapo ndiko chimbuko la mfumo dume na unyanyasaji wa wanawake ulikoanzia jamaa anatumikisha mke kwa suluba nyingi huko akimshambulia mkeo kwa maneo makali HAKUNA KUKAA KWA HASARA HAPO NIMELIPA MAHARI KUBWA SANA.

4.Kwa makabila mengine binti hana sauti na haruhusiwe kuongea chochote kipindi cha kuolewa kwake,hio sio nzuri sana inaondoa uhalisia wa wahusika wa ndoa.Japo si vema pia bintivakawa mjuaji kuliko wazazi na wanakamati.Aweza kushauri jambo pale anapoona mambo yanataka kuharibika ila busara na upole vitamfanya asikilizwe zaidi.


4.Uwezo wa kulipa mahari,maandalizi ya harusi hadi harusi yenye hutofatiana kutoka kijana hadi kijana,familia hadi familia,ukoo hadi ukoo,kabila moja hadi kabila jingine na Hata Taifa hadi Taifa.

Siku za hivi punde imetokea kasi ya kushinda namna ya kufunga ndoa,Kwenye Nchi yetu ni vyepesi watu kuchangia harusi kuliko mtoto kwenda shule.

Kama uwezo wenu ninyi mnaoana ni wa chini kwa wakati huo hakuna sababu yakukamuana hadi jasho la mwisho.kuna uwezekana ni ninyi kuja kumiliki mali mingi sana mara tu baada ya kuingia kwenye ndoa yenu.


Wenye uwezo wa kati pia funguni harusi sawasawa na uwezo wenu.


Matajiri nao hakuna dhambi kuwa harusi za kifahari ila itapendeza mkidumu kwenye ndoa,ni aibu na fedheha kutumia gharama nyingi kuingia kwenye ndoa kisha baada ya mwezi unasikia hao walishaachana.

Kuiga fulani alifunga harusi kubwa kwa weza kupelekea kuvunjika kwa mahusiano ya uchumba.
WASWAHILI WALISEMA;UKIMWIGA TEMBO UTAPASUKA MSAMBA.
 
Hapo kwenye Utii napinga sema labda useme Kuheshimiana!
​
 
Hakuna kuheshimiana bila mambo haya kuwepo kwa Wanandoa:-

Mwanamume kupenda mke wake kuliko wanawake wengine wote.

Mwanamke kumtii mume wake pindi anapomweleza mambo yenye kujenga familia yenye uadilifu,Ufanisi na Amani.

Changanya uaminifu (wote wawili) kufanya mambo kwa masikilizano.

Epuka kutunza makosa ya mwenzio huleta mlipuko wa chuki,
kudharauliana.

Ukuta wa mahusiano huanguka,hupelekea kuzorota kwa penzi la kweli na kuanza kulala wakipeana migogo.

Kushamiri kuhasimiana hata kuachana kirahisi mno kana kwamba hawajawahi hata kukaribiana vile.

Ndoa nyingi ziko kwenye hatari ya kuanguka ni kwa sababu hakuna utii wala upendo.

Utii (sio ujinga wa mwanamke kuburuzwa na mwanamume) na Upendo sio uzuzu
wa mwanamume kutawaliwa na mwanamke.
 
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…