Hatua za kupata udhamini ughaibuni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hatua za kupata udhamini ughaibuni

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by MAKULILO, Feb 2, 2012.

 1. MAKULILO

  MAKULILO Member

  #1
  Feb 2, 2012
  Joined: May 30, 2010
  Messages: 84
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 15
  HATUA ZA KUPATA UDHAMINI UGHAIBUNI (3)

  Ada ya Maombi ya Udahili - Application Fee


  NA: ERNEST BONIFACE MAKULILO (MAKULILO, JR.)
  CALIFORNIA, USA

  View attachment 46534

  Leo hii katika hatua za kupata udhamini ughaibuni tunaangalia Ada ya Maombi ya Udahili (Application Fee). Utambuaji wa ada ya maombi ni kiasi gani, inalipwaje, utawezaje kufanya maombi kwenye vyuo vingi hukui ukilipa ada ya maombi kiasi kidogo? Hayo ni baadhi ya mambo muhimu sana katika kujua ada ya maombi katika udahili na kupata udhamini wa elimu.

  Awali ya yote ni lazima utambue kuwa kama unafanya maombi, na chuo husika wameweka kiwango fulani kama ada ya maombi na mwombaji kutolipa ada hiyo, maombi hayo ya mwombaji huwekwa kapuni bila kufanyiwa tathmini maana yamekosa ada hiyo. Ofisi ya udahili (admissions office) inaeleza kinagaubaga kuwa ada ya maombi kama ipo katika chuo hicho au la, na kama ada ya maombi ipo wataelezea ni kiasi gani na italipwaje.

  Katika moja ya makala zilizopita nilielezea kwa juu juu utofauti ulipo kati ya uombaji vyuo Ulaya na Amerika. Utofauti mmoja wapo na wa msingi ni huu wa ada ya maombi. Kwa Ulaya ( na hata Australia, New Zealand nk) wao hawana hii ada ya utumaji maombi. Lakini kwa upande wa Amerika hususani USA na Canada wao ni lazima ulipe ada ya maombi. Hivyo unapochagua pa kufanya maombi yako kuna maana kubwa sana hususani kujua gharama utakazotumia na kuweza kuomba vyuo vingapi.

  Ili mtu uweze kupata ufadhili mmoja wa chuo, usitegemee kuomba chuo kimoja kisha kuweka matumaini yako yote hapo. Kama ule msemo wa kiingereza usemao “Don’t put all eggs in one basket” hivyo inabidi uombe si chini ya vyuo 20 ili uweze kupata ufadhili walau wa vyuo viwili ili uwe katika wakati mzuri wa kuchagua ni chuo kipi uende kati ya ulivyopata, na hapo utaangalia kiasi cha udhamini ulichopewa pamoja aina ya kozi, na kipindi kingine unaangalia mahali ulipopata.

  Sasabasi kwa kuwa inabidi ufanye maombi si chini ya 20 itakugharimu kiasi kikubwa cha fedha kama ada ya maombi. Nini ufanye uweze kuomba vyuo vingi kujiongezea nafasi ya kupata? Hapa ndipo nakushauri mwaombaji ni vyema aombe vyuo vingi vya ulaya ambapo hakuna ada ya maombi na vyuo vichache vya Marekani au Canada kama atapenda. Hii itakupa nafasi nzuri ya kuibuka mshindi na kupewa udhamini, ila kama utaomba mfano vyuo viwili au kimoja naamini kabisa utakosa na utabaki kulaumu kuwa udhamini ughaibuni umegubikwa na upendeleo nk kumbe hujafuata mbinu za kuwa mshindani madhubuti.

  Kwa wanafunzi wa kimataifa (International Students) ada ya maombi huwa tofauti na wazawa. Kwa wastani ni kwamba mwomabi wa kimataifa anatakiwa alipe ada si chini ya dola 50, na vyuo vingi huwa ni kati ya dola 50 na 100. Na malipo haya lazima yafanywe kwa Check (Lazima mwenye account ya Bank iwe ya benki ya Kimarekani kama utaomba Marekani na ya Kikanada kama utaomba Canada), au Debit/Credit Cards ambazo zina uwezo wa kufanya malipo kwa njia ya mtandaoni (Online Transaction) kama vile Visa au Master Cards. Swali la kujiuliza ni kwamba: Je, unayo Visa/Master Card ya kukuwezesha kulipa ada ya malipo kwa njia ya mtandao? Je, una kiasi kitakiwacho kulipwa? Kama huna, suluhisho lako ni Ulaya, Australia na New Zealand ambapo wao huko hawana hii ada ya maombi.

  Umakini unatakiwa sana kabla hujalipa ada ya maombi kuepukana na matapeli wa mtandaoni (scams). Ni wengi sana wametapeliwa mtandaoni kwa wao bila kuwa makini. Fanya utafiti wa tovuti uitembeleayo na pia njia za ulipaji nk. Unaweza kuniuliza swali lolote kama unahisi tovuti unayotaka kulipa ina walakini, naweza kukujulisha kama ni matapeli au la, maana nina uzoefu wa kutosha mtandaoni kuwatambua matapeli hawa.

  Kwa habari zaidi za mambo ya udhamini wa elimu ya juu, jiunge na jukwaa la Scholarship Forum ili uweze kupata taarifa nyingi. SIGN UP at www.scholarshipnetwork.ning.com


  Maswali au maoni, niandikie Makulilo@makulilofoundation.org

  MAKULILO
   
 2. Mazigazi

  Mazigazi JF-Expert Member

  #2
  Mar 11, 2015
  Joined: Jul 6, 2012
  Messages: 3,987
  Likes Received: 2,153
  Trophy Points: 280
  Mada nnzuri sana wananchi tuchangamkie fursa
   
 3. Payer

  Payer JF-Expert Member

  #3
  Mar 13, 2015
  Joined: May 10, 2014
  Messages: 827
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Safiii
   
 4. t

  till hustling Member

  #4
  Mar 14, 2015
  Joined: Mar 7, 2015
  Messages: 24
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 5
 5. mr gentleman

  mr gentleman JF-Expert Member

  #5
  Mar 15, 2015
  Joined: Aug 1, 2012
  Messages: 2,615
  Likes Received: 2,732
  Trophy Points: 280
  Lakini pia inatakiwa watu wajue kuwa kabla haujafanya application lazima uwe na vifuatavyo mkononi:-

  1. Passport
  2. matokeo ya Ielts au Teofl


  Hivi ni vitu muhimu sana unapoanza kufanya application.
   
 6. mr gentleman

  mr gentleman JF-Expert Member

  #6
  Mar 15, 2015
  Joined: Aug 1, 2012
  Messages: 2,615
  Likes Received: 2,732
  Trophy Points: 280
  Hii post imemlenga nani?
   
 7. Slim5

  Slim5 JF-Expert Member

  #7
  Mar 15, 2015
  Joined: Jan 7, 2014
  Messages: 15,776
  Likes Received: 12,971
  Trophy Points: 280
  Inamlenga mlengwa
   
Loading...