Hatua za kufuata ili kuipata simu iliyo ibiwa

Hatua za kufuata ili kuipata simu iliyo ibiwa

LEGE

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2011
Posts
5,122
Reaction score
9,223
wakuu ni kama mwezi sasa na wiki kadhaa zimepita tangia nilivyoibiwa simu na vibaka waliochana nyavu nakuiba kupitia dirishani.

ni simu aina ya huawei y530.risit na mpaka box lake bado lipo kwa hiyo IME number ipo.

nimepata wazo hili baada ya kusikia kuwa ukiwa na IME number unaweza pata simu yako kwa kwenda kwenye campun ya simu kama voda airtel or tigo unawapa IME number nao wana kujulusha kuwa now simu yako inatumiwa na sim card ya aina gani (Number gani).

tatizo langu ni kuwa je ni hatua zipi natakiwa kuchukua au kufuata ili niweze ipata simu yangu.
nikienda moja kwa moja kwenye kampun naweza saidiwa au ndio mpaka nipitie polisi??

maana nikisikia suala la polisi ndio nachoka kabisaa najua nitaishia kuzungushwa tuu.

au kama kuna mtu anafaham kuna kampun yoyote inatoa huduma hiyo ni kampun gani hata kama iwe nje ya tanzania.
au hata kama kuna mtu anaweza fanya shuguli hii plz naomba mnijuze.

ishu ni kuwa simu imenitia hasara kubwa sana.kuna watu nilikuwa nawadai ndio basi tena.
 
Hilo linawezekana kupitia polisi, na kuna barua inaandikwa inaenda kusainiwa na mkuu wa police mkoa. Mara nyingi watu wanapotumia simu kufanyia uhalifu huwa process kama hizi zinafanyika kwa haraka sana ila kwa issue kama yako ni ngumu kidogo. Kusaidiwa mara moja labda ingekuwa Tanzania tuna mtandao mmoja wa mawasiliano ya GSM. huenda ingesaidia.
 
Unafanya biashara na record unaweka kwenye simu? au. Anway kuitrace simu kwa imei inawezekana japo kuna cost za kutosha na kuzingatia model ya simu yako inaweza kuwa mara nne ya gharama ya simu yako. Potezea..
 
Back
Top Bottom