Hatua za kuchukua baada ya kutapeliwa

Joined
Nov 30, 2022
Posts
28
Reaction score
19
Nafanya biashara ya delivery...

Nimepeleka bidhaa kwa mteja, mteja kapokea ila kazuga mtandao mbovu kashindwa Fanya transaction..

Nimemuamini atatuma baadae,kapotea mazima, ukimtafuta inabaki anakupa kalenda tu..

Details zake nilizo nazo ni namba ya simu tu basii...

Polisi nimeenda,wananiambia ni ngumu kumpata kwa namba tu..nifanyeje wadau..
 
Kama hayo ndiyo majibu ya Polisi basi kazi ipo!!

BTW: Zoezi la usajili wa namba za simu kwa alama za vidole ni a failed project.
Mkuu umesahau huku ni bara la giza,mambo yetu yapo kigizagiza tu,unategemea majibu gani kwa hao polisi bila kujiongeza.
 
Unajiita Genius Kipanga huku upstairs ni zero? Ulimwachiaje mzigo mtu ambaye hajalipia?
 
Pole asee.
Hii taharuki ata mim imenikuta.
Kuna mdada nafanya nae biashara hua natuma pesa ananitumia mzgo.
Ila term hii ni mwezi sasa nimetuma pesa mzgo haujatumwa napigwa karenda tu.

Ila yeye picha zake ninazo, na maeneo anayofanyia kaz kariakoo napafaham na miamala ninayo ila mim nipo mwanza.

Najiuliza kuchoma nauri nikamshughurikie napo naona kuna mawili.

Kiufupi hata tz na africa derivery hatuiwez wengi wana tamaaa na njaa njaa tu.
 
Umemuamini ??, kama mtandao unasumbua unabeba mzigo wako chap, hakuna kuacha mzigo hamjifunzi tu..
 
Kama n mteja wa kiume. Tafuta pisi kali mpe namba ya mdeni wako. Mwambie ajitongozeshe kwa hyo jamaa. Wakat huo kuwa na Rb yko mfukon. Siku ya pisi kal na mdeni wako wakikutana ma ww unatokea na hyo Rb yko. Unamchukua kama kuku.
Note: Its take time and consume money.
 
Mkuu umesahau huku ni bara la giza,mambo yetu yapo kigizagiza tu,unategemea majibu gani kwa hao polisi bila kujiongeza.
Hapa tunataka 'facts'.

'Kujiongeza' ama ujanja ujanja ni rushwa.

Emb kama unajua njia halali na halisi za kisheria kuchukua, basi tumia uelewa huo kumshauri mwenzako hatua za kufuata.

Nadhani ndiyo msaada anaoutaka toka kwa wadau.

'Kujiongeza' kila mtu anakujua.
 
Hii ya 'kumchukua kama kuku' nimeipenda. 😃😃😍
 
Wabongo kwenye biashara za online bado sana ,95% si waaminifu.

Fanya biashara za online kwa taasisi kubwa tu ila hawa wajasiliamali wa online hao ni matapeli tu.
 
Wabongo kwenye biashara za online bado sana ,95% si waaminifu.

Fanya biashara za online kwa taasisi kubwa tu ila hawa wajasiliamali wa online hao ni matapeli tu.
kabisa mkuu, bado roho ya umasikin na njaa vinatawala kwa wajasiriamali.
Ila wakiwa waaminifu na wakaacha tamaa umasikin watauaga.
 
Watu ni wapumbavu kweli….Sasa wewe jinga hadi leo unategemea polisi wakupatie haki yako.Matako yako.
 
Yule muigizaji msomali yule, alie shiriki nyimbo ya ray c unanimaliza wewe unanimaliza wewe wanamuita gallas cjui, huyo jamaa alikitana na shabiki wake mtandaoni anavodai yeye akaona isiwe kesi yule shabiki alikia anajishughulisha na biashara za mapambo sijui thamani mbalimbali na ana page insta ya muda tu jamaa kaingia mkenge kampa pesa apatiwe zile thamani yule dada kachimba jamaa akawa ana lalamika insta akidai yule dada ni tapeli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…