Hatua za kuanza kujifunza Computer Programming.

xpl0it

Senior Member
Feb 21, 2014
124
88
Hatua za kuanza kujifunza Computer Programming.

Ndugu wasomaji,

Watu wengi wanashindwa kujua waanzie wapi kuanza kujifunza programming au wanawezaje kuwa programmers wakisasa, hivo nafurahi kwamba leo watakuwa wamepumzika wamekaa mahali wakisoma makala ya msaada sana. Leo tunakwenda kujifunza hatua za kuanza kujifunza computer programming na kuanza kuandika code nzuri zenye logic. Hatua hizi tutazigawanya katika makundi mawili, moja likiwa ni kuchagua language, kujifunza language na mwishoni ni kujifunza mwenyewe.


1) Kuchagua Language

Chagua programming language.

Computer programming inafanyika kama set of instructions ambazo computer inafollow (ikijulikana kama binary coding). Instructions hizi zinaweza kuandikwa katika languages mbalimbali, au namna mbalimbali kuzipangilia instructions hizo. Languages tofauti tofauti zinatumika kutengeneza programs tofauti tofauti.

Chukulia languages kama C, C#, C++ na zingine zihusianazo na hizo.

Languages hizi zinatumika sana kutengeneza computer applications kama games. C na C++ ni ngumu kwa beginner kujifunza ila sio kwamba haiwezekani kwake yeye kujifunza. Kujifunza hizo hazitakupa tu uelewa wa kiundani wa programming (programming languages nyingi zinarithi baadhi ya concepts au zaidi kutoka kwa C & C++), lakini pia jinsi computer inavofanya kazi. zinajulikana na kutumika zaidi, hatahivyo C#, language inayofanana sana na Java, inaanza kufahamika zaidi.

Chukulia Java au javascript.

Hizi ni languages nzuri za kujifunza kama unataka kufanya kazi kutengeneza web plugins(javascript) au program za simu(java). Hizi languages zinahitajika sana sahivi, hivo ni vema pia kuzijua. Fahamu akilini mwako kwamba Java na javascript ni language tofauti kabisa, hatakama majina yao yanafanana.

Jaribu Python.

Python ni language ambayo ni rahisi kutumika popote na hutumika katika takriban platforms zote. Ukiachilia mbali uwezo wake, ni language rahisi sana kwa beginner kuanza kujifunza nayo, hivo ijaribu!

Chukulia PHP. PHP inasimama badala ya PHP: Hypertext Processor.

Ni language ya kutengeneza programs za web na ni rahisi sana kujifunza na umaarufu wake(umaarufu nikimaanisha kwamba kutakua na tutorials zake nyingi kwaajili ya kujifunzia). Ni language nzuri kwa upande wa server side programming.

Usijiwekee Limit kwa hizo languages!

Kuna tani nyingi za language, zote zikifanya kazi tofauti. Kama ukitaka kufanya kazi kama programmer, itakubidi ujue zaidi ya moja, hivo jifunze nyingi uwezavyo.

2) Kujifunza hiyo Lugha

Fikiria kuhusu kwenda chuo/college

Wakati kampuni nyingi zinaajiri programmer watajali zaidi kuhusu skills (ujuzi) ulionao kuliko college uliyosoma au grades zako ulizopata ukiwa huko, inasaidia sana kupata degree. Utajifunza zaidi kiufanisi kuliko ukijifundisha mwenyewe, vyote hivo huku ukiendelea kupata usaidizi kutoka kwa waalimu wako(na hata pia marafiki zako).

Jifunze kutokea kwenye Universities za mitandaoni.

Iwe kwamba unasomea degree yako mtandaoni kwa kulipia ada na degree halisi mwishoni au unasomea vipindi vya bure kama MIT wonderful Coursera, unaweza kujifunza vingi kuhusu programming kutoka kwenye course hizo zilizopangiliwa.

Jaribu kutumia vyombo(tools) vya online.

Tumia huduma za bure kama Google University Consortium au Mozilla Developer Network kujifunza zaidi kuhusu programming. Hizi kampuni zinataka developers zaidi kusaidia platforms zao kunawiri na resources zao zinaweza kuwa baadhi ya bora zaidi katika web.

Jifunze kutumia tutorials za mitandaoni(Online tutorials).

Kuna programmers wengi wenye websites ambapo watakufundisha kanuni na misingi mbalimbali, ikiwemo pia tricks chache. Tafuta tutorials kuhusu language unayotaka kujifunza kupata hizi.
Madarasa mengi ya bure ya online yanapatikana kujifunzia coding kutokana nazo. Khan Academy inafundisha computer coding, kwa kutumia tutorials rahisi na videos. Code Academy ni site nyingine ya bure kujifunzia huko, zikiwa na tutorials za hatua-kwa-hatua.

Anzia chini kama utaweza.

Kunaprograms nyingi zimetengenezwa kufundishia watoto jinsi ya kuprogram. Program kama MIT Scratch zinasaidia sana na uchanga ulionao, itakuwa rahisi kuchukua (kama program yoyote). Jiepushe na kits, kwasababu hazitakufundisha sana kitu chenye manufaa.

3) Kujifundisha mwenyewe

Anza na kitabu kizuri au tutorial kuhusu programming.

Pata kitabu kizuri na cha kisasa cha kuhusu programming language unayotaka kujifunza. Reviews/maoni kwenye Amazon au websites zinazofanana na hiyo huwa zitakusaidia kutambua vitabu vya muhimu kutoka kwa visivyo muhimu.

Pata interpreter ya hiyo language.

Interpreter ni computer programming nyingine tu lakini itabadilisha mawazo uliyoyaandika kwenye programming language kwenda katika "machine code" ili uone vitu vikifanya kazi. Programs nyingi zinapatikana na utahitajika kuchagua moja tu ambayo itakuwa sahihi kwako.

Soma kitabu!

Hapa ndipo wabongo tulipo na tatizo. Kusoma vitabu kunatuongezea mawazo mbalimbali kutoka kwa wengine na kuweza kutufanya tufahamu vitu vingi. Chukulia mifano wa programming language kutoka kwenye kitabu na uiweke kwenye interpreter yako. Jaribu kubadilisha mifano na kuifanya program ifanye vitu tofauti.

Jaribu kuweka mawazo yako pamoja kutengeneza program inayofanya kazi.

Anza na vitu rahisi, kama program ya kubadilisha thamani ya fedha, na ufanye juhudi kwenda kwenye program ngumu na ukiwa unaendelea kusoma na kujifunza kuhusu programming language yako.

Jifunze Language nyingine.

Wakati ukianza kuprogram vizuri kwenye katika language yako ya kwanza, unaweza ukataka kujifunza ya pili. Utajifunza mengi kama hiyo language ya pili ni tofauti kimitindo ukilinganisha na ile ya kwanza. Kwa mfano, kama ulianzia katika Scheme, unaweza ukajaribu kujifunza C or Java baada yake. Kama ulianza katika Java ungeweza kujifunza Perl au Python.

Endelea kuprogram na kujaribu vitu vipya!

Kuwa programmer mzuri, unapaswa kuendana na mabadiliko ya kiteknolojia. Ni mchakato endelevu, na unatakiwa kujifunza language mpya, mitindo mipya, na kimsingi zaidi: Kuprogram vitu vipya!


Umeenjoy Post hii? Usisahau kushare na wenzako wapate kujifunza! Unakaribishwa pia kupost comment.


The Programmer
 
You are a good teacher umepangilia vizuri material zako. Ni vema ukafikiria kitengeneza audio na video tutorial kwa lugha hii hii. Zinaweza kuwasaidia ambao ni vigumu kusoma maneno. Utapata subscribers wengi maana ujuzi hauzeeki, hatuishi kujifunza.
 
You are a good teacher umepangilia vizuri material zako. Ni vema ukafikiria kitengeneza audio na video tutorial. Zinaweza kuwasaidia ambao ni vigumu kusoma maneno. Utapata subscribers wengi maana ujuzi hauzeeki, hatuishi kujifunza.
Nashukuru sana kaka... Najitahidi kupata njia mbalimbali ambazo zitafanya wananchi wenzangu wa kitanzania wenye moyo huu wa programming na teknolojia kiujumla kujifunza na kufahamu mambo mbalimbali na sisi Tanzania kufika mbali katika ulimwengu huu wa Sayansi na Teknolojia. Naimani tunaweza!

Nina forum yangu hii hakerhub.000webhostapp.com ambamo ndo napendelea kushare mambo mbalimbali yahusuyo Programming, Hacking, na habari mbalimbali ya yaliojiri katika ulimwengu wa Teknolojia. Nafikiria baadae kuanzisha Channel ya Youtube ambapo ntakuwa natengeneza tutorial kwa ajili ya watanzania kujifunza na kupanuka ufahamu juu ya maswala haya ya programming na kadhalika.
 
Safi sana mkuu
Nashukuru sana kaka! Inapendeza sana Tanzania baada ya miaka kadhaa baadae tuwe mbali sana katika tasnia hii ya Kompyuta na Teknolojia yetu.

Yafaa tutengeneze ata product yetu moja, itakayokuja kutumika na vizazi vyetu baadae huko. Yote hii Inawezekana tukiamua kubadili mindset yetu na kunia kusonga mbele.
 
Ulichokiandika ni sahihi. Kama unataka kujifunza programming languages zaidi ya moja ni vyema beginner akanza na C. Hii ndiyo language ambayo syntax yake inafanana na languages nyingi.
 
Ulichokiandika ni sahihi. Kama unataka kujifunza programming languages zaidi ya moja ni vyema beginner akanza na C. Hii ndiyo language ambayo syntax yake inafanana na languages nyingi.
Hakika kabisa ndugu! Ukijua hiyo apo au C++ inakuwa rahisi sana kujifunza hata nyingine maana syntax na paradigm zake hazitofautiani saaana!
 
Ulichokiandika ni sahihi. Kama unataka kujifunza programming languages zaidi ya moja ni vyema beginner akanza na C. Hii ndiyo language ambayo syntax yake inafanana na languages nyingi.
Hakika kabisa ndugu! Ukijua hiyo apo au C++ inakuwa rahisi sana kujifunza hata nyingine maana syntax na paradigm zake hazitofautiani saaana!
 
Kwanza ukiwa unajifunza sizani kama ni vyema kuangalia ni ipi ngumu au rahisi! Unatakiwa uangalie nn unahitaji kutimiza?? Unataka web development...go for html and css ...javascript...python etc

Unataka software development angalia java c++ and the alike!

Sometimes ni vyema ukaanza na lugha ngumu ili ikujenge! Kuanza na lugha rahisi ukija kutana na ngumu kama java au c++ unaweza ona maisha magumu!!
 
Nadhani maelezo yote yamejitosheleza kabisa katika makala hiyo niliyoiandika apo juu. Labda unambie tu ni kipengele gani ambacho wewe hukipati kabisa?
 
Nadhani maelezo yote yamejitosheleza kabisa katika makala hiyo niliyoiandika apo juu. Labda unambie tu ni kipengele gani ambacho wewe hukipati kabisa?
Muulize amesoma masomo gani, wakati mwingine masomo ni msingi wa kusoma/kujifunza kitu.
 
Back
Top Bottom