Hatua kwa hatua jinsi ya kuanzisha biashara

Masokotz

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
3,495
5,531
Mwongozo huu unaweza kutumika kwa aina nyingi za biashara lakini kwa leo nitajikita katika katika biashara ya Independent Consultant/Consultant/Mshauri Mwelekezi

Consultant ni mtu mwenye,ujuzi,utaalamu na taarifa kuhusu jambo fulani ambaye anatoa huduma ya kushauri, kuelekeza, kusimamia, kutaarifu, kutafiti na hata kufundisha wengine juu ya jambo hilo ili kuwasadia kufikia lengo lao.

Unaweza kuwa mshauri wa kibiashara, kisheria, kiufundi, kielimu, kibinafsi, mahusiano,masoko, kilimo, ufugaji, afya, malezi, muziki, manunuzi,
uajiri,etc

Unaweza kuwa mshauri katika eneo lolote lile unalolimudu na amini nakuambia kuna mtu ambae yuko tayari kulipia ili kuzungumza na wewe kuhusiana na eneo fulani la utaalamu wako.

Yupo mtu ambaye anahitaji ujuzi ulio nao.Yupo ambaye anahitaji taarifa ulizo nazo, yupo mtu ambaye anahitaji muda wako.

Consultants wote huwa wanauza maarifa yao na muda wao. Hii ndio bidhaa yao kuu.

Ili kuanzisha consultancy firm ni lazima uwe na maarifa, na uwe na Muda. Muhimu zaidi ni lazima ufahamu thamani ya bidhaa yako hii (Muda wako na Maarifa yako). Ni lazima pia ufahamu ni wapi bidhaa yako ina soko zaidi.

Ili kuanzisha consultancy firm ni lazima uongeze thamani ya bidhaa zako, yaani uongeze thamani ya Muda wako, na uongeze thamani ya Maarifa yako.

Ili kuongeza thamani ya muda wako ni lazima ufahamu matumizi bora na sahihi ya muda kwani muda tulio nao wote ni limited 24hours. Ili kuongeza thamni ya maarifa yako ni lazima uwe na utamaduni wa kujifunza kwa njia tofauti.

Katika matumizi ya muda ni muhimu ukafahamu kabisa ni wakati gani huwa ni bora kwako kufanya jambo fulani mfano kusoma, kufundisha, kuandika, kusongea, kupumzika n.k.

Kwa kufahamu wakati bora utaweza kupangilia ratiba yako kwa kuzingatia wakati bora na sahihi kwa kufanya jambo fulani.

Mfano kuna watu ambao wako mentally active usiku zaidi kuliko mchana hivyo basi zile kazi ambazo zinahitaji ubongo huzianya usiku.

Sasa nirudi kwenye lengo la msingi la UZI HUU.

Kabla ya kufanuya jambo lolote tambua eneo ambalo ungependa kujikita zaidi kulingana na kiwango chako cha elimu, uzoefu, mtandao wako na hata hobby yako.

Pili thaminisha thamni ya ujuzi huu (Price) kama mtu atapaswa kukuilipa unafikiri akulipeje? Unapofikira Bei hakikisha unakuwa na bei kulingana na Demand ya huduma, supply ya huduma, hali ya uchumi, malengo yako, umaarufu wako na wateja unaowalenga.

Weka bei rafiki kwa ina zote za wateja,usiweke bei ya chini sana wala usiweke bei ya juu na daima hakikisha unakuwa na Premium Prices kwa wale ambao wanataka huduma za ziada.

Unapotambua eneo lako la uzamifu basi unatakiwa uchagua brand. Je utatumia personal brand au independent brand.

Kumbuka hata ukichagua Independent brand bado utahitaji kuwa na personal Brand.

Baada ya kumaliza hatua hizo hapo juu hatua inayofuata ni kujisajili. Kama fani uliyochagua ina association au regulatory body basi jiunge nao mapema kabisa.

Vile vile unaweza kujisaji kwa kutumia sheria ya Majina ya Biashara na Hata kujisajili kulipa kodi na kujipatia leseni ya biashara kulingana na uwezo wako.

Kumbuka kama wewe ni mshauri mwelekezi usihangaike kukodisha Fremu kwa ajili ya ofisi katika hatua za mwanzo bali unaweza kutumia maeneo yafuatayo kama ofisi ya muda:
  1. Kwenye hotel na migahawa mikubwa yenye utulivu ambapo unaweza kupata free wifi na ukanunua kinywji cha moto au baridi na ukafanya kazi taratibi kwa saa nne ha 6 huku unakunywa soda na kutumia MB zao na kuonana na wateja wako hapo hapo.
  2. Kwenye hubs and co working spaces ambapo unaweza kupata huduma za meeting rooms,meza na kiti pamoja na mtandao wa watu tofauti wanaoweza kuwa wateja wako
  3. Nyumbani kwako iwapo una mtandao na mazingira tulivu ya kufanya kazi.
Jambo la kuzingatia ni kuhakikisha kwamba sehemu unayofanyia kazi ni sehemu tulivu, unayoweza kukutana na mtu na kufanya naye mazungumzo kwa utulivu. Vile vile iwe sehemu rahisi kufikia ili kupunguza gharama za uendeshaji.

Baada ya kuchagu sehemu ya kufanyia kazi ni muhimu sana uwe na website kwa ajili ya kutangaza biashara yako.

Unaweza kuongeza na kurasa za mitandao ya kijamii, ili kuongeza mtandao. Katika website yako hakikisha unakuwa na segemu ya kuweka maandiko (Publications) mbalimbali ambayo unaweza kuweka mambo mbalimbali kama vile CASE STUDIES, WHITE PAPERS, RESEARCH REPORTS na CURRENT TRENDS za eneo lako.

Hii ina maana kwamba kama mshauri unapaswa kutumia muda wako mwingi kuandaa CASE STUDIES, WHITE PAPERS na TAFITI ambazo zitazidi kuonesha utaalamu wako.

Hakikisha unakuwa na Emails za wateja wako na watu wengine ambao unaweza kuwatumia hizi report zako ili kuhakikisha kwamba unawafikia watu wengi sana.

Ni matumaini yangu kwamba andiko hilo litawapa hamasa wale ambao wanafikiri kwamba kujiajiri ni kazi ngumu/rahisi ili watambue kwamba jambo la muhimu ni kuwa na nia madhubuti pamoja na bidii.

Iwapo unahitaji ushauri,msaada katika kufikia lengo la kuanzisha biashara yako usisite kuwasiliana nasi kwa EMAIL:MASOKOTZ@YAHOO.COM ambapo utaweza kupata huduma za usajili wa Biashara yako, Kutengenezewa Website, Kufundishwa jinsi ya kufanya case studies, kuandika white papers na hata kukuza biashara yako kwa gharama nafuu na uhakika.

Tuwasiliane kwa masokotz@yahoo.com
 
Kwanza asante kwa ujuzi
pili ni mawazo niliyonayo na maswali
1. kutokana na ufukara sijui niuite umaskini nilionao nimeamua nianze kuchuuza viatu vya kike kutoka maduka ya k-koo na kuuzia mbagara
2. nawaza nianzishe utengenezaji wa sabuni za magadi maarufu kama sabuni za kigoma
swali langu 1 kwako🖕 je mawazo yangu hayo kuna huduma yoyote ya kitaalam nawezapata toka kwenu?
kama ndyo ni ipi?
Asante
 
Kwanza kabisa hongera kwa kufikia hatua hiyo,Pili sababu sio ufukara nafikiri utakuwa umeona fursa mahali na sio ufukara.Kama ulivouliza swali lako moja jibu ni NDIO kuna huduma nyingi ambazo tunaweza kukupatia ikiwamo jinsi ya kubrand hizo sabuni zako,jinsi ya kuzizalisha na kuziuza,na hata jinsi ya kuweza kutengeneza fursa kwa ajili ya jamii yako na kuweka ushindani wa kibiashara.Iwapo ungependa kupata huduma zetu tafadhali tutumie ujumbe ukieleza kwa ufupi tu malengo yako kibiashara katika biashara yako,changamoto zako na fursa unazoziona kisha tunaweza kuangalia namna ya kukufanya kuwa mzalishaji na mjasiriamali bora.Kila la heri
 
Consultancy business ni hukk Juu, kwa wazungu, Bongo is not applicable sana, na Kwa wazungu huwezi fanya biashara bila kufanyiwa consultancy ila Tanzania yetu sio lazima.

Na pia hii biashara ukiitegemea hakiamungu unalaza watoto njaaa, hii sio ya kutegemea hata kidogo.

andoza
 
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu,ni hofu yako tu,unafikiri kwamba watu hawahitaji consultancy?unafikiri watu hwako tayari kulipia huduma hio?Unafikiri kwamba hii biashara haifai kufanywa na wabongo?Unaweza kuwa sahihi ili usiwe sahihi.Ninchoamini ni kwamba hakuna fursa rahisi ya kufanikiwa zote zinahitaji bidii na maarifa na kujituma.Changamoto zi biashara zipo kila mahali hata huko wazungu.Binafsi nafahamu kampuni nyingi za kibongo zinazoajiri consultancies kwa shughuli mbalimbali.

Mtazamo wako unaonesha zaidi hofu na sio ujasiri
 
Consultancy business ni hukk Juu, kwa wazungu, Bongo is not applicable sana, na Kwa wazungu huwezi fanya biashara bila kufanyiwa consultancy ila Tanzania yetu sio lazima.

Na pia hii biashara ukiitegemea hakiamungu unalaza watoto njaaa, hii sio ya kutegemea hata kidogo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu hawa watu wana umuhimu sana kuliko tunavyofikiri. Wanaongeza tija sana kwenye biashara. Kuna kipindi unafanya biashara kwa mazoea ili kuepuka hili sio mbaya ukapata assessment kwa watu wa nje.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza kabisa hongera kwa kufikia hatua hiyo,Pili sababu sio ufukara nafikiri utakuwa umeona fursa mahali na sio ufukara.Kama ulivouliza swali lako moja jibu ni NDIO kuna huduma nyingi ambazo tunaweza kukupatia ikiwamo jinsi ya kubrand hizo sabuni zako,jinsi ya kuzizalisha na kuziuza,na hata jinsi ya kuweza kutengeneza fursa kwa ajili ya jamii yako na kuweka ushindani wa kibiashara.Iwapo ungependa kupata huduma zetu tafadhali tutumie ujumbe ukieleza kwa ufupi tu malengo yako kibiashara katika biashara yako,changamoto zako na fursa unazoziona kisha tunaweza kuangalia namna ya kukufanya kuwa mzalishaji na mjasiriamali bora.Kila la heri
I 'll keep in touch
ngoja baada ya wik 4 nitakucheki mkuu
 
Back
Top Bottom