Hatua gani inatakiwa ili nihame kwenda kwa mwajiri mwingine?

makalango

JF-Expert Member
Feb 10, 2017
448
252
Habari za muda huu?

Samahani naombeni msaada wenu,,mimi niliajiriwa katika halmashauri fulani na mwajiri wangu ni DED lakini baadae nikaomba ajira sekreteriati ya utumishi wa umma hiyo barua ya maombi nikapitisha kwa mwajiri wangu akaipitisha baadae nikaitwa interview nikafaulu zote mbili na kupangiwa kituo cha kazi katika moja ya masharika ya serikali na sekreteriati ya ajira nashukuru Mungu kwa hilo.

Swali langu nitafanyaje kuhamisha taarifa zangu za utumishi kutoka kwa DED ambaye ni mwajiri wangu wa sasa kwenda kwa mwajiri mpya? Barua niliyo pangiwa kituo iliyotoka sekreteriati ya ajira imetumwa kwa wafuatao:

1. Katibu mkuu utumishi wa umma

2. Katibu tume ya utumishi wa umma

3. Mkurugenzi wa shirika hilo.
 
Rudi ulipoanzia kaongee na DED ndo atakusaidia nini cha kufanya,huku sidhani na cha ajabu kwa nini hujakaa na hao watu wa ofisi hizo zote kushauriana nao maana lazima wanajua taratibu zote,lakini wewe umekuja Jf.
 
Rudi ulipoanzia kaongee na DED ndo atakusaidia nini cha kufanya,huku sidhani na cha ajabu kwa nini hujakaa na hao watu wa ofisi hizo zote kushauriana nao maana lazima wanajua taratibu zote,lakini wewe umekuja jf
Ahsante mkuu nimekuelewa.
 
Rudi ulipoanzia kaongee na DED ndo atakusaidia nini cha kufanya,huku sidhani na cha ajabu kwa nini hujakaa na hao watu wa ofisi hizo zote kushauriana nao maana lazima wanajua taratibu zote,lakini wewe umekuja jf
Kwa hiyo unataka kusema huku JF hakuna watumishi wa serikali HRs wanaojua hizo taratibu?

Mbona kama unataka kutupanga mkuu
 
Hata usiwe na shida mkuu... Kuna mfumo unaitwa HCMIS na LAWSON unafanya kazi ya kuhamisha taarifa zako zote za kiutumishi na jambo lingine pia fanya uwasiliane na Afisa Uajiri/ Utawala/ Rasilimali watu wa sehemu uliyotoka, unapoenda na wao watalink taarifa zako kwa njia ya barua na system(mfumo)..

Mwajiri atahuisha taarifa zako zote na zitamfikia Katibu mkuu utumishi wa umma na Katibu tume ya utumishi wa umma

Cha msingi ni taarifa sahihi na ufuate utaratibu utakaoelekezwa na HRs wa kwenu na huyo mpya
 
Hiyo barua haikukuelekeza chochote? Yani imekupangia tu sehemu ya kazi bila maelezo yoyote?

Kwa vyovyote vile Katibu Mkuu Utumushi atahusika. Pia na Afisa Utumishi mahali ulipo sasa atahusika.
 
Ahsa
Hata usiwe na shida mkuu... Kuna mfumo unaitwa HCMIS na LAWSON unafanya kazi ya kuhamisha taarifa zako zote za kiutumishi na jambo lingine pia fanya uwasiliane na Afisa Uajiri/Utawala/Rasilimali watu wa sehemu uliyotoka, unapoenda na wao watalink taarifa zako kwa njia ya barua na system(mfumo)..

Mwajiri atahuisha taarifa zako zote na zitamfikia Katibu mkuu utumishi wa umma na Katibu tume ya utumishi wa umma

Cha msingi ni taarifa sahihi na ufuate utaratibu utakaoelekezwa na HRs wa kwenu na huyo mpya
Ahsante mkuu
Hiyo barua haikukuelekeza chochote? Yani imekupangia tu sehemu ya kazi bila maelezo yoyote?

Kwa vyovyote vile Katibu Mkuu Utumushi atahusika. Pia na Afisa Utumishi mahali ulipo sasa atahusika.
Imeandikwa kk katibu mkuu then imeandikwa nimepangiwa kazi kituo fulani na nikaripoti ndani ya siku 14 hao ni sekreteriati ya ajira
 
Ahsa

Ahsante mkuu

Imeandikwa kk katibu mkuu then imeandikwa nimepangiwa kazi kituo fulani na nikaripoti ndani ya siku 14 hao ni sekreteriati ya ajira
Sasa hapo nenda kwa Afisa utumishi mahali ulipo...wakakufungashie data za utumishi wako, then ukaripoti Kituo kipya ndani ya hizo siku 14.

Sent from my SM-J200F using JamiiForums mobile app
 
Sasa kama barua ya awali walipitisha wanakusumbua nini? Ukiona wanakuzingua nenda karipoti kituo Kipya then unaenda UTUMISHI kuwachoma (maana hata wasipohamisha taarifa zako zinachakatwa na utumishi tu). Hao wanakuonea donge tuu,yaani Maafisa Utumishi wanajiona kama Miungu watu kabisa.

Je, Hiyo barua yako imeeleza juu ya kwenda na taarifa zako za kiutumishi kutoka ulipohama/au huenda DED wako ameandikiwa ya kwake kuwa Mtumishi wako anahamia Shirika fulani.Au kama unaweza nenda Sekretarieti ya Ajira waeleze waone namna bora ya kukusaidia.
 
Sasa kama barua ya awali walipitisha wanakusumbua nini? Ukiona wanakuzingua nenda karipoti kituo Kipya then unaenda UTUMISHI kuwachoma (maana hata wasipohamisha taarifa zako zinachakatwa na utumishi tu).Hao wanakuonea donge tuu,yaani Maafisa Utumishi wanajiona kama Miungu watu kabisa...
Ndio alipitisha Ded mwenyewe tena nikaambatanisha na hiyo hiyo barua ambayo ndio nimepata hiyo kazi shida ni wasaidizi wake ndio wananisumbua kweli basi tu nikawalazimisha ipelekeni hivyo hivyo kwa mwajiri maana wanaanza kujenga sababu ohoo hii barua yako haina Kk kwa ded wako mara Ded wako hana taarifa za kuhusu ww yani wanakatisha tamaa aisee
 
Ndio alipitisha Ded mwenyewe tena nikaambatanisha na hiyo hiyo barua ambayo ndio nimepata hiyo kazi shida ni wasaidizi wake ndio wananisumbua kweli basi tu nikawalazimisha ipelekeni hivyo hvyo kwa mwajiri mana wanaanza kujenga sababu ohoo hii barua yako haina Kk kwa ded wako mara Ded wako hana taarifa za kuhusu ww yani wanakatisha tamaa aisee
Unalea upuuzi wa hao wapuuzi wa kwa DED; Yaani wafanyakazi wa Local Government wako Local siku zote sijui kwanini. Ingekua enzi zangu hao ni kuwachomea utumishi faster.

Ukishawaonesha barua zote hizo; wewe nenda kwa DED ambae alikua mwajiri wako wa awali then mwambie walichokujibu hao wasaidizi wake kinyume na utaratibu alafu ufanye makabidhiano..then nenda karipoti ajira mpya.
 
Ahsante mkuu nimekuelewa kesho ndio nategemea ded anijibu kwa mandishi ili nami nijue pa kwenda
 
Back
Top Bottom