Hatua 6 za kumzuzua mwanamke

Hatua 6 za kumzuzua mwanamke

marahaa1

Member
Joined
Sep 1, 2016
Posts
68
Reaction score
98
Ukweli usemwe. Ndoto ya kila mwanaume katika hii dunia wakati mmoja au mwingine hufikiria kuwa na kipawa cha kuweza kumzuzua mwanamke yeyote anayemzimia. Uzuri ni kuwa hauhitaji kuwa tajiri ama kuvutia ili uwe na kipawa kama hiki.


Kujifunza kuzuzua mwanamke si jambo kubwa vile, mwanzo ni rahisi zaidi kwa mtu yeyote yule kutimiza jambo hili kama atafuata hatua zinazohitajika kwa umakini.

Wengi wa wanaume wanashindwa kumzuzua mwanamke wa ndoto yake kwa sababu wanatumia mbinu ambazo zimepitwa na wakati ama kutumia mitindo ambayo haikubaliki.
Well, nimekuandalia hatua 6 za kufanya ili umzuzue mwanamke yeyote yule.

1. Pokea pongezi
Wanaume wengi wanatabia ya kukataa kupokea pongezi kutoka kwa mwanamke. Balada ya wewe kuguna ama kutojiskia huru wakati mwanamke anakupongeza, mbona usitumie nafasi hii kutumia maneno ya utamu kama ile 'asante, 'nashukuru' nk.
Kupokea pongezi kutoka kwa mwanamke ni kama vile kupokea zawadi kutoka kwake, hivyo kufanya hivi kutakuwa kukimfurahisha mwanamke kila wakati.

2. Kuwa na maoni chanya kujihusu
Kama hujiamini wewe mwenyewe ama unajiona huwezi kutimiza kumfurahisha mwanamke je unatarajia mwanamke akupende? Hivyo basi iwapo unataka kumzuzua mwanamke unafaa ujiamini wewe mwenyewe kama mwanaume.
Njia rahisi ya kutimiza hii ni kuhakikisha unavalia nguo za kupendeza, unavalia marashi yakunukia, na kuwa nadhifu. Wanawake wengi wanapenda mtizamo aina hii.

3. Jifundishe kudensi
Ok wengi wangeuliza kwa nini nijifunze kudensi? Kudensi ina uhusiano wowote upi na kumzuzua mwanamke?

Jibu rahisi. Kwanza ni kuwa wanawake wanapenda sana wanaume ambao wanajua kudensi. Hivi ushajiuliza kwa nini dancers wengi wanapendwa na wanawake?
Pili ni kuwa wanawake wanaamini ya kuwa dancers wengi wanaujua mchezo ikija maswala ya chumbani.

Tatu ni kwa hautarajii mwanamke unayemzimia adensi na wanaume wengine wakati mumeenda kwa kilabu.
So ni muhimu kujifunza kudensi, atleast style moja mbili za kumdanganya.

4. Tumia jina lake
Siri nyingine ya kumzuzua mwanamke ni kumtaja jina lake wakati wa maongezi. Kulingana na mwandishi maafuru wa kiingereza Dale Carnegie, anadai ya kuwa sauti tamu zaidi kwa sikio la mwanamke ni kusikia ukitaja jina lake.

Kama umekuwa ukifanya uchunguzi ni kuwa wengi wanahepa kutumia majina ya wapenzi wao nk. Hivyo wewe usikubali kuanguka ndani ya hio kategoria. Waonaje sasa uanze kutumia jina lake kila wakati unapomtext ama kuongea naye? Amini usiamini jambo hili linafanya kazi kama uchawi.

5. Muangazie yeye
Iwapo unataka mwanamke akuchukie kwa siku moja basi ongea na kujisifu wewe mara kwa mara wakati mnapoongea pamoja. Iwapo unataka kumzuzua mwanamke basi kinachohitajika ni kuhakikisha unampa atenshen yako yote wakati mko pamoja mnaongea.

6. Kuwa mcheshi
Imethibitishwa ya kuwa hakuna mtu angependwa kujihusisha na mtu anayeboa. Hivyo kama unakipawa cha ucheshi ama unauwezo wa kumfanya mwanamke avutiwe nawe basi hio ni silaha kubwa ya kumfanya mwanamke azuzuike kwako.

Hitimisho: Matumizi ya mbinu hizi na sanaa nyingine za kutongoza tulizichapisha awali zitaksaidia wewe pakubwa kuhakikisha ya kuwa unamzuzua yeyote yule.
 
Haya mambo hayana formula una weza ukawa mcheshi kama joti na ukashndwa kueleweka tu.

Kuna mwingine hataki umuite jina ana taka baby, sweetie na mbwembwe nyingii
Cha msingi ni mtu mwenyewe akubaliane na hali yako.

Ahsante lakini mada nzuri hiyo
 
Hahahahah elewa usikalili haya mambo hayaihaji elimu sana wala shule na binadamu tupo tofauti
 


KERO HIZI MBONA NI JINSI TU YAKUMMALIZA HUYU KIUMBE WAKATI WENYEWE WAKO BUSY

Meet Our Teams.jpeg
 
....The great question that has never been answered, and which I have not yet been able to answer, despite my thirty years of research into the feminine soul, is 'What does a woman want?'....
Sigmund Freud
 
Haya mambo hayana formula una weza ukawa mcheshi kama joti na ukashndwa kueleweka tu.

Kuna mwingine hataki umuite jina ana taka baby, sweetie na mbwembwe nyingii
Cha msingi ni mtu mwenyewe akubaliane na hali yako.

Ahsante lakini mada nzuri hiyo
Hakuna mwanamke anataka ucheshi wa joti ha ha ha ha , Na pia ucheshi usipitilize ukawa kama chizi tena, yani ucheshi wa kawaida, binafsi napenda aniite jina langu hasa akiwa anasisitiza jambo, babe sweetie na honey hivyo vitu pia unaweza kutumia ila ukiwa unabembelezwa au vyovyote vile akichanganya jina na hizo mbwembwe nyengine vinanoga kwakweli.
 
My be ulaya hukooo. Yaani Tanzania ukiwa na waleti y kueleweka tayari usha wazuzua
mwanamke anaekupenda kiukweli hajali hata hiyo wallet, ukiona unapendwa kwa ajili ya wallet jua mmepangwa 10, mana kila mwanaume anayo wallet lol
 
mbona kipengele cha mtonyo sijakiona hapo bila pesa halima ndala ndefu atanielewa kweli na kuzuzuka na mimi?
 
Hakuna mwanamke anataka ucheshi wa joti ha ha ha ha , Na pia ucheshi usipitilize ukawa kama chizi tena, yani ucheshi wa kawaida, binafsi napenda aniite jina langu hasa akiwa anasisitiza jambo, babe sweetie na honey hivyo vitu pia unaweza kutumia ila ukiwa unabembelezwa au vyovyote vile akichanganya jina na hizo mbwembwe nyengine vinanoga kwakweli.

Sawa
Kuwa elewa nyie ni kazi kweli, hujataja pesa lakini, nadhani ulisahau.
 
mwanamke anaekupenda kiukweli hajali hata hiyo wallet, ukiona unapendwa kwa ajili ya wallet jua mmepangwa 10, mana kila mwanaume anayo wallet lol
Mnasemaga tu hivyo lakini mwisho wa Siku wallet ya kueleweka ndio mpango Mzima
 

Sawa
Kuwa elewa nyie ni kazi kweli, hujataja pesa lakini, nadhani ulisahau.
Hici pesa na mapenzi vinahusiana VIPI??...UNAJUA MANA YA KUPENDANA, Nyie mnaenda tafuta MAPENZI (Kufanyana) ndo mana PESA NI KIGEZO, Ushawahi kupendwa wewe?? Mwanamke akikupenda yeye ndio kila siku unaweza mkuta nakununuliwa zawadi na mara nyingi mnakuwa mnapanga mambo kwa pamoja kama anakupenda, KAMA MTU HANA FUTURE NA WEWE, Na umemtongoza anakwambia nina mtu ila unalazimisha na wakati wakulamizisha unatumia silaha ya pesa jua kwa huyo mwanamke utakuwa kitega uchumi hakuna asiependa pesa, HATA WANAUME WANALELEWA NAKUPEWA PESA.
 
Back
Top Bottom