Clark boots
JF-Expert Member
- Jun 5, 2017
- 6,401
- 5,525
Habari za pilikapilika za kutwa nzima wanaJF!
Ni wakati/muda tu umenilazima kuyaandika haya kuhusiana na hatma ya wasomi wetu nchini hasa kwenye suala la ukosefu wa ajira ndani ya miaka hii minne toka serikali ya awamu ya tano ilipoingia madarakani na miaka ijayo mbeleni.
Ni ukweli usiopingika kuwa sasa ajira zimekuwa adimu Serikalini hata mashirika/taasisi binafsi, licha ya wafanyakazi hewa wote wale waliondolewa, ufisadi au utakatishaji fedha za umma uliokomaa na pesa zetu nyingi zinazorudishwa serikalini kutoka kwa mafisadi Ila bado suala la ajira ni kizungumkuti.
Ni dhahiri kabisa kuwa suala/sekta ya ajira ni sekta nyeti kwa kila taifa, nadhani serikali yenyewe inahimiza watu kuhusu elimu ili ije kuwakomboa watu katika maisha yao na tegemeo kuu ni ajira.
Vijana mamia kwa mamia wanahitimu elimu za juu kila mwaka na wanajazana mitaani tu, Ajira Hamna. Ni muda sasa serikali ikaliona hili japo si wote na tunaamini hakuna serikali yoyote inayoweza kuajiri wasomi wote katika taifa husika basi hata kwa kiwango fulani/nusu yao si haba.
Inasikitisha sana nyakati hizi kuona msomi wa shahada anamaanika, elimu imekuwa haina thamani tena na watu kujenga dhana kuwa elimu ni upotevu wa muda/wakati.
Leo nilikuwa nafuatilia hizi ajira kada ya kilimo kutoka sekretariet ya ajira. Vijana wengi wameitwa kwenye usaili halafu nafasi ni 10 tu. Kiukweli haiingii akilini unahitaji watumishi 10 halafu unaita interview watu 1300 sawa na 0.7% ya watu wote. Inasikitisha sana.
Ni muda muafaka sasa wa Serikali kuliona hili kwani hali ni tete na elimu yetu bado sana wala haiwezi kumjenga kijana kuweza kujiajiri mwenyewe baada ya kuhitimu masomo yake. Ni muda mrefu sana Graduates wanaozeana huku mitaani.
Sasa umekuwa ni muda wa kutengeneza, vibaka, majambazi, machangudoa, wezi, matapeli.
Naomba serikali iliangalie hili kwa jicho la tatu.
Nawasilisha.