Hatma ya wasomi wetu Tanzania

Hatma ya wasomi wetu Tanzania

Yaani hapa ndipo ulipaharibu kabisa hoja yako nzuri. Hivi ina maana ukikosa ajira serikalini unakuwa kibaka au changudoa? Kwa nini unawafunga fikra wahitimu wetu, Je serikali hata ikitengeneza fursa za ajira nyingi iwezekanavyo, inaweza kuajiri wote katika kada zote? Je wakibaki hata 500 tu nchi nzima, ina maana watakuwa majambazi?
Sikumaanisha kuwa wahitimu wote wanakuwa hvyo ila hyo ni mojawapo ya impact kubwa ambayo inasababishwa na ukosefu wa ajira kwa wasomi.
Tukija upande wa kuajiri, nimezungumzia japo nusu ya wahitimu maana sidhani kama kuna nchi ambayo inaajiri graduates wote toka vyuon ila japo kiasi Fulani kinachoridhisha itasaidia kuliko hii hali inayoendelea.
 
Bado kuna uhitaji mkubwa wa wataalam serikalini, sio kweli kwamba imefika muda eti wataalam wametosha..

Pamoja na nchi kuwa maskini sera mbovu na kukosa ubunifu kwa serikali ya CCM ndio sababu..

Hakuna aliyepo huko juu anafikiria kuondokana na umaskini katika hii nchi, wamebaki kupiga kelele za watu wajiajiri, kuajiajiri sawa ila mwisho wa siku mteja ni nani? Nani utampa hizo huduma hiari watu wapo katika tope la umaskini?
Asante kwa mchango wako mkuu
 
Back
Top Bottom