Hatma ya vijana kisiasa Tanzania

mkuu betlehem habari za siku nyingi.. Mkuu umepotea sana kwenye anga hizi. Naomba usikate tamaa kuendelea kuuelimisha huu umma humu Jf maana wengi hawajielewi kama mleta mada.

Vijana waliotajwa hapa juu ndio hawajielewi,life is about choices lakini unahitaji tafakuru pana kufanya decision..
vijana hawa hawakuwa na independent thought katika maamuzi yao thus why oftentimes wazee hawaamini vijana.

Wangefanya maamuzi sahihi leo hii wangekuwa mbali either ndani au nje ya CDM,they are push over,vijana tuache papara...
 
Wanajamvi naomba nikiri wazi kwamba naandika mada hii nikiwa na masikitiko makubwa sana.Nimejaribu kufuatilia maisha ya kisiasa ya vijana ambao waliondoka/walifukuzwa CHADEMA kutokana na mienendo yao ya kisiasa na kusitika sana.Nidiriki kusema kwamba Mh.Zitto Kabwe amechangia sana kuwaweka vijana hawa kwenye majonzi makubwa sana.

Mh.Zitto ni moja ya vijana waliofanikiwa sana kubadilisha mitazamo ya vijana kuhusu masuala ya kisiasa na kushawishi vijana wengi kujiunga na siasa na hata kupelekea vijana wengi kugombea ubunge kupitia CHADEMA 2010.Lakini mienendo ya Zitto na ushawishi wake kwa vijana umeacha majonzi wakubwa sana kwa vijana.

Leo vijana waliopotezewa future na Zitto wamekuwa wanaishi maisha ya kuombaomba,wale wa kike wamekuwa chakula ya wakubwa,kuna baadhi walikuwa walimu wamefukuzwa,waliogombea ubunge kupata mtaji mkubwa kwa uchaguzi wa 2015 sasa hawana jukwaa la kisiasa.

Kuna kijana mmoja yeye alijiunga na NCCR na baada ya muda mfupi alikuwa Katibu wa uenezi vijana,akapewa kazi kwenye taasisi ya Mbatia akafukuzwa kwa kukosa maadili leo hii ukimuona na kumsikiliza inasikitisha,amekata tamaa ya maisha kabisaaa.

Mh.Zitto Kabwe nasikitika sana kwa kitendo chako cha kurudisha nyuma harakati za baadhi ya vijana katika kupigania haki,uwazi na uwajibikaji katika Taifa hili.Vijana hawa walikuamini na kutoaminika,historia ina kila sababu ya kukuhukumu, tatizo lako ni kuwaona watanzania ni wajinga na una akili kuliko wanasiasa wote wa upinzani Tanzania.Umejenga imani kwamba bado unauwezo wa kuwashawishi watanzania ukiwa kama Zitto,kuwashawishi watanzania kwasababu ni watu wepesi wa kusahau.

Hatuwezi kubadilisha taifa hili bila kubadilisha fikra zetu,fikra za Zitto zinapaswa kushawishi fikra za wengine na si kupotosha kwa makusudi.Vilevile fikra za vijana wa CHADEMA zisiwe fikra za utumwa bali fikra kutoa mwanga kwa jamii nzima juu ya nini chama kinasimamia.Tusiwe ufuasi wa watu bali wafuasi ya falsafa,itikadi,sera na maadili mema.

Mungu wape ufahamu na busara vijana wa Tanzania,tuna jukumu kubwa kwenye kizazi hiki.

nitajie kijana wa chadema anaejielewa,,ambae sio mtumwa wa fikra za mbowe na slaa.
 
juliana shonza hakukubali kuwa mtumwa wa fikra za viongozi madikteta wa chadema ndio maana amefukuzwa...hakukubali kuwa mtumwa kama misukule akina ben, yericko, kilewo, heche n.k
 
Deogratius Kisandu ni miongoni mwa wahanga.

Vijana ambao bado hawajajitegemea nawashauri waache kuparamia siasa kwa kutaka kufanya siasa kama kazi ya kuwapatia chakula! Mtu yoyote aliyejitegemea hawezi kuingia mwili mzima kwenye siasa kama anao hana potential hiyo! Vijana wengi ndo wanaorudisha nyuma harakati za upinzani maana siyo wavumilivu! Wakisia leo Lowasa anagawa elfu 10 kwa wanabodaboda utaona watavyofurika siku hiyo! Wakisia leo kuna mkutano wa upinza nako wanafurika. Wanawakataa mafisadi lakini hawako tayari kuachia pesa hata kama inatoka kwa fisadi na inafahamika wazi kuwa ni hongo kwao. Vijana wakijikinai japo kwa mwaka mmoja wakakataa kuhongwa na mafisadi na wakawaunga mkono wapinzani kwa dhati nchi hii itaondoka kwenye kongwa la utumwa wa CCM hata kama wakitumia pesa na majeshi yote nchini! Kwa hali ninavyoiona upinzani unaungwa mkono na midle age yaani kuanzia 30 up to 50 maana hawa wanajua wanachokifanya! Vijana under 30s wanashangilia siasa kama kuna pesa nyuma yake otherwise hakuna kitu hapo! Tuhakikisheni vijana wanakuwa na ajira kwanza ndo tuwashirikishe kwenye mapambano bila hivyo usaliti hautaisha maana njaa ni kali nchi hii!
 
Last edited by a moderator:
juliana shonza hakukubali kuwa mtumwa wa fikra za viongozi madikteta wa chadema ndio maana amefukuzwa...hakukubali kuwa mtumwa kama misukule akina ben, yericko, kilewo, heche n.k

Itakuwa vizuri na wewe kutokuwa mtumwa wa watu kwenye chama chako cha ACT.Tunahitaji kizazi cha vijana chenye fikra pevu,hili ndio dhumuni kubwa la uzi huu,kazi yangu ni kukuelimisha,mtoto humfundishi jujitegemea kwa siku moja
 
vijana wa chadema vipi mbona hawana lolote?

Vipi katibu mwenezi wa ACT, nyie ndo mnaoongelewa humu, hamueleweki mnafanya nini kwenye siasa! Wakati wezenu wanaungana kuippinga ccm nyie mnaungana na ccm kuwapinga wapinzani! Mtapewa hela ya kula tu lakini hamtatajirikia pesa za mafisadi maana wao wanajua utamu wa pesa kuliko nyie! Mtumikieni kafiri mpate chakula yenu!
 
mkuu betlehem habari za siku nyingi.. Mkuu umepotea sana kwenye anga hizi. Naomba usikate tamaa kuendelea kuuelimisha huu umma humu Jf maana wengi hawajielewi kama mleta mada.

Mkuu mayange ,sijakata tamaa ila nimeamua kutuliza akili kidogo kwa sababu kuna wakati najihisi kama napata hasira kidogo.

Niliku- pm kitu muhimu kama hukuona, check spam.

Ndugu Mayange, hebu tusubiri kidogo.
 
Last edited by a moderator:
1. Mtela Mwampamba(green guard wa ccm)
2.Juliana Shonza(Mke wa Mwigulu wa ccm)
3.Habib Mchange.(Anamchanganyiko w ACT na CCM,anamsubiri Zitto amuamlie pa kwenda)
4.Nyakarungu(ACT).
5.Kitila Mkumbo(ACT)
6............
7............
8............

Ongezea wengine.
 
Mkuu mayange ,sijakata tamaa ila nimeamua kutuliza akili kidogo kwa sababu kuna wakati najihisi kama napata hasira kidogo.

Niliku- pm kitu muhimu kama hukuona, check spam.

Ndugu Mayange, hebu tusubiri kidogo.

mkuu betlehem nakuelewa sana.. Nasikitika sana na sielewi tunakoelekea.
 
Last edited by a moderator:
mkuu betlehem nakuelewa sana.. Nasikitika sana na sielewi tunakoelekea.
Hata mimi nasikitika vile vile ila sina cha kufanya.La msingi ni way foward! kuwa despaired na kuamua kuacha liwalo nao si uamuzi sahihi.Kwa hiyo ni hivyo tu kwamba la msingi ni kila penye mkwamo au matatizo; basi tunaangalia way foward ambayo ni possible na inaonekana kuwa na afadhali ukilinganisha na nyingine.Kitaalam hivyo ndivyo inavyotakiwa kuwa.
 
ila nakumbuka kunapost uliiweka hapa jf kuhusu kutoa elimu ya uraia hasa vijana wanaovamia siasa bila ya hata kujua siasa ikoje na kujikuta wanakuwa washabiki 2.
 
ila nakumbuka kunapost uliiweka hapa jf kuhusu kutoa elimu ya uraia hasa vijana wanaovamia siasa bila ya hata kujua siasa ikoje na kujikuta wanakuwa washabiki 2.

Mkuu mayange kuna mambo mawili au matatu,

1.Kuna tatizo la elimu ya uraia kwa baadhi,
2, Kuna tatizo la baadhi kukubali kutumika bila kujali sana wala kufikiri wanatumiwa na nani na katika kufanya nini,
3. Halafu vile vile kuna kitu mtaani wanaita "Kujitoa fahamu"

Naomba niishie hapa kwa sasa.
 
Last edited by a moderator:
Sipendi kulizungumzia hili but...

Juliana Shonza ni nyota iliyozimwa na waliotakiwa kumsaisia.Nilijaribu kadiri ya uwezo wangu.

Miongoni mwa vijana wote hao,yeye alikua na potentials but i still believe she can reclaim her dream and ambitions. Huyu ni Victim tu wa Wanasiasa wanaoweza kumkanyaga kila mtu ili wafike wanakotaka.

Najua hawezi kukiri hili

naunga mkono hoja.,Juliana ni nyota iliyozimwa na wanasiasa wenye tamaa,na wasiojali kukanyaga migongo ya wengine kufikia malengo binafsi
 
juliana shonza hakukubali kuwa mtumwa wa fikra za viongozi madikteta wa chadema ndio maana amefukuzwa...hakukubali kuwa mtumwa kama misukule akina ben, yericko, kilewo, heche n.k

kwahiyo akakubali kuwa mtumwa wa fikra za zito,anakuambia hama nae akahama af yeye anakomaa na mahakama.utumwa wa fikra mbaya sana
 
Mkuu mayange kuna mambo mawili au matatu,

1.Kuna tatizo la elimu ya uraia kwa baadhi,
2, Kuna tatizo la baadhi kukubali kutumika bila kujali sana wala kufikiri wanatumiwa na nani na katika kufanya nini,
3. Halafu vile vile kuna kitu mtaani wanaita "Kujitoa fahamu"

Naomba niishie hapa kwa sasa.

nimekuelewa mkuu..
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom