Wanajamvi naomba nikiri wazi kwamba naandika mada hii nikiwa na masikitiko makubwa sana.Nimejaribu kufuatilia maisha ya kisiasa ya vijana ambao waliondoka/walifukuzwa CHADEMA kutokana na mienendo yao ya kisiasa na kusitika sana.Nidiriki kusema kwamba Mh.Zitto Kabwe amechangia sana kuwaweka vijana hawa kwenye majonzi makubwa sana.
Mh.Zitto ni moja ya vijana waliofanikiwa sana kubadilisha mitazamo ya vijana kuhusu masuala ya kisiasa na kushawishi vijana wengi kujiunga na siasa na hata kupelekea vijana wengi kugombea ubunge kupitia CHADEMA 2010.Lakini mienendo ya Zitto na ushawishi wake kwa vijana umeacha majonzi wakubwa sana kwa vijana.
Leo vijana waliopotezewa future na Zitto wamekuwa wanaishi maisha ya kuombaomba,wale wa kike wamekuwa chakula ya wakubwa,kuna baadhi walikuwa walimu wamefukuzwa,waliogombea ubunge kupata mtaji mkubwa kwa uchaguzi wa 2015 sasa hawana jukwaa la kisiasa.
Kuna kijana mmoja yeye alijiunga na NCCR na baada ya muda mfupi alikuwa Katibu wa uenezi vijana,akapewa kazi kwenye taasisi ya Mbatia akafukuzwa kwa kukosa maadili leo hii ukimuona na kumsikiliza inasikitisha,amekata tamaa ya maisha kabisaaa.
Mh.Zitto Kabwe nasikitika sana kwa kitendo chako cha kurudisha nyuma harakati za baadhi ya vijana katika kupigania haki,uwazi na uwajibikaji katika Taifa hili.Vijana hawa walikuamini na kutoaminika,historia ina kila sababu ya kukuhukumu, tatizo lako ni kuwaona watanzania ni wajinga na una akili kuliko wanasiasa wote wa upinzani Tanzania.Umejenga imani kwamba bado unauwezo wa kuwashawishi watanzania ukiwa kama Zitto,kuwashawishi watanzania kwasababu ni watu wepesi wa kusahau.
Hatuwezi kubadilisha taifa hili bila kubadilisha fikra zetu,fikra za Zitto zinapaswa kushawishi fikra za wengine na si kupotosha kwa makusudi.Vilevile fikra za vijana wa CHADEMA zisiwe fikra za utumwa bali fikra kutoa mwanga kwa jamii nzima juu ya nini chama kinasimamia.Tusiwe ufuasi wa watu bali wafuasi ya falsafa,itikadi,sera na maadili mema.
Mungu wape ufahamu na busara vijana wa Tanzania,tuna jukumu kubwa kwenye kizazi hiki.