Hatma ya ubunge wa Jitu Son yakaribia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hatma ya ubunge wa Jitu Son yakaribia

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Sep 25, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Sep 25, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [h=2][/h]JUMANNE, SEPTEMBA 25, 2012 06:44 NA ELIYA MBONEA, ARUSHA

  MAHAKAMA ya Rufaa Tanzania, mbele ya jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji Mkuu Othman Chande, imemaliza kusikiliza rufaa ya aliyekuwa mgombea Ubunge Jimbo la Babati Vijijini, Laurence Sharubu Tara wa Chama cha NCCR–Mageuzi.

  Tara, alikata rufaa kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu ya Tanzania chini ya Jaji Fatuma Masengi, uliompa ushindi Mbunge wa Babati Vijijini (CCM), Virajila Jitu Son.

  Jopo la majaji, Salum Masati, Natalia Kimaro na Jaji Mkuu Chande, walisikiliza hoja za upande wa mawakili wa utetezi.

  Akiwasilisha utetezi wa hoja zake mbele ya jopo hilo, Wakili Mwandamizi, Severine Lacena, alidai mawakala hawakuwa na mamlaka ya kukagua vifaa alivyopewa msimamizi wa uchaguzi katika vituo.

  Alisema kutokana na mamlaka aliyokuwa nayo msimamizi wa kituo, aliwaelekeza kujaza na kusaini fomu za rangi ya pinki, kutokana na kutokuwapo kwa fomu zenye rangi nyeupe.

  “Msimamizi wa kituo ndiye, alikuwa akiongoza mawakala kujaza fomu hizo, sasa mrufani kupitia kwa mawakala wake, walipewa fomu zenye rangi ya pinki, wakati mjibu rufani walipewa fomu zenye rangi nyeupe ambazo ndio Orijino,” alisema Lawena.

  Pamoja na kuwasilisha hoja nyingine, wakili Lawena aliomba jopo hilo la Majaji kutengua uamuzi uliotolewa na Mahakama Kuu wa kumpatia ushindi mbunge wa CCM.

  Kwa upande wa mjibu rufani wa kwanza ambaye ni Serikali kupitia kwa mawakili wa Serikali, Monica Otaru na Timon Vitalisi, waliliambia jopo la majaji hapakuwa na ukosefu wa fomu wala malalamiko.

  Wakili Monica, alidai mbele ya jopo la majaji pamoja na mambo mengine bado mawakala hawakulalamika juu ya kujitokeza kwa malalamiko kama hayo.

  “Tunaiomba mahakama hii, itupilie mbali rufani iliyopo mbele yenu na ninaomba muuone uamuzi uliotolewa na Mahakama Kuu ya Tanzania, ulikuwa sahihi,” alisema Wakili Monica.

  Naye Wakili Mwandamizi, Duncan Oola anayemwakilisha Jitu Son alilieleza jopo hilo la majaji kama kungekuwa na upungufu wowote kwenye uchaguzi ama kabla ya au baada ya kupiga kura fomu namba 14, ndio ilipaswa kujazwa.

  “Hakuna lalamiko lolote lililojazwa kwenye fomu namba 14, kinyume chake hawa wafungua Rufani wanaposema kulikuwa na upungufu, basi walipaswa kuonyeshaupungufu kwenye fomu namba 14, ambazo hawakuzijaza,” alisema Oola na kuongeza:

  “Kutumia fomu namba 21 B kujazia matokeo haikuwa sahihi. Hivyo naomba rufaa hii, itupiliwe mbali tena kwa gharama,” alisema Oola.

  Novemba 2010, Tara ambaye ni Diwani wa Kata ya Bashnet, alifungua kesi iliyoanza kusikilizwa Februari 16, mwaka huu, akiiomba Mahakama Kuu imtangaze kuwa mbunge halali wa jimbo hilo, kwani ndiye alikuwa mshindi halali na kudai alishinda kwa tofauti ya kura 58, baada ya kupata kura 32,248 na Jitu Son akipata kura 32,190 katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.

   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Sep 25, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  Jaji Mkuu Chande hana kazi nyingi ? Yaani kajiingiza kwenye kila rufaa ya Uchaguzi wa Ubunge?
   
 3. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #3
  Sep 25, 2012
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Huyo Mrufani anaitwa Laurent Surumbu Tara.
   
 4. a

  anney Senior Member

  #4
  Sep 25, 2012
  Joined: Jul 9, 2010
  Messages: 156
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  I hope Chande's presence will help to have fair decision in deciding this case.
   
 5. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #5
  Sep 25, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,335
  Likes Received: 2,659
  Trophy Points: 280
  Kwani mkuu kazi ya Jaji ni nini? nadhani jina la Jaji Mkuu litakua lakutatiza, huyo ndugu kisheria anaruhusiwa kusikiliza kesi kama majaji wengine wasio na wadhifa wa Jaji Mkuu...
   
 6. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #6
  Sep 25, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,798
  Likes Received: 3,884
  Trophy Points: 280
  sure?? do you realy know him?? he is a puppet for is your info!!
   
 7. F

  FJM JF-Expert Member

  #7
  Sep 25, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Ndio madhara ya kujaza majaji wa kichina! Inabidi afanye kazi yeye sasa.
   
 8. Marire

  Marire JF-Expert Member

  #8
  Sep 25, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 11,420
  Likes Received: 260
  Trophy Points: 180
  sasa wewe mpaka ureply post ndeefu au kwakuwa unatumia kalaptop ka wizi sisi wa tecno tuumie vidole?
   
 9. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #9
  Sep 25, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  Nilidhani kuna JIJI Kiongozi ambaye ndio Jaji Kiongozi wa Mahakama za Rufaa Nchini; Kwanini Jaji Mkuu

  Aanze kuingilia ? Hizi sio rufaa za kwanza kukatwa...
   
 10. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #10
  Sep 25, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Jaji Kiongozi kazi yake ni nini tena ?

  Unajua kuna JAJI KIONGOZI ?
   
 11. i

  iseesa JF-Expert Member

  #11
  Sep 25, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 944
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Per diems ( Fedha ya kujikimu)
   
 12. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #12
  Sep 25, 2012
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Hana imani na majaji wengine.
   
Loading...