Hatma ya tanesco, askofu kakobe kujulikana wiki hii | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hatma ya tanesco, askofu kakobe kujulikana wiki hii

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bujibuji, Jan 28, 2010.

 1. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #1
  Jan 28, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,323
  Likes Received: 22,154
  Trophy Points: 280
  Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, amekubali kumaliza sakata hilo ambalo liliibuka mwishoni mwa mwaka jana baada ya Tanesco kutaka kupitisha nyaya za umeme juu ya mabango ya kanisa hilo.

  Hata hivyo, lengo hilo la Tanesco liligonga mwamba baada ya waumini wa Kanisa hilo kutanda na kuweka ulinzi kwa saa 24 kanisani hapo.

  Akizungumza na Nipashe jana jijini Dar es Salaam, Askofu Mkuu wa Kanisa hilo, Zakaria Kakobe, alisema mazungumzo ya kutaka kusitisha mpango huo wa Tanesco yanakwenda vizuri na kwamba wiki hii ukweli utajulikana.

  Kakobe alisema amefanya mazungumzo na Waziri wa Nishati na Madini ambaye ana dhamana na masuala ya umeme na anaamini kuwa yatazaa matunda.

  Mwishoni mwa mwaka jana Tanesco ilitangaza kupitisha nyaya zake juu ya mabango ya Kanisa hilo kitendo ambacho kilipingwa na waumini wake.

  Kutokana na kitendo hicho cha Tanesco, waumini wa Kanisa hilo waliamua kujipangia zamu za kulinda Kanisa lao usiku na mchana.

  Askofu Kakobe alisema ulinzi unaofanywa na waumini wake ni wa uhakika na kwamba Tanesco hawawezi kupenya.

  Walinzi hao wa Kanisa wanafanya kazi hiyo huku wakiwa wamevalia tisheti zilizoandikwa maneno "Tanesco muogopeni Mungu mmeshindwa Richmond mmegeukia Kanisa"

  Baadhi ya waumini wa Kanisa hilo waliliambia Nipashe kuwa ulinzi huo unajulikana kama "ulinzi wa kumdhibiti adui."
  Ngeleja aliingilia kati sakata hilo baada ya waumini wa Kanisa hilo kujitokeza hadharani na kutangaza vita na Tanesco ambapo waliapa kufa kuliko kuruhusu nyaya zipite juu ya mabango yao.

  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #2
  Jan 28, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,582
  Likes Received: 3,883
  Trophy Points: 280
  Aibu kwa Tanesco kwa nini wanafanya mambo kiholela holela, wamepoteza muda na mali kitu kilichotakiwa kuzuilika. Risk assesors wengine inabidi kujifunza this is good case study.
   
Loading...