Hatma ya nchi chini ya CCM: Masikio yote Dodoma

Hatma ya nchi chini ya CCM: Masikio yote Dodoma

Juliana Shonza

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2012
Posts
2,009
Reaction score
1,607
Kama alivyosema Mzee Mkapa katika moja ya hotuba yake makini aliyoitoa mwishoni mwa miaka ya 2004 ambayo imenukuliwa katika vyombo mbalimbali vya habari na katika jarida la Mzalendo la Chama Cha Mapinduzi, kuwa CCM ikipiga chafya wengine wote wanapata homa"

Ukweli huo umebaki hivyo na utabaki hivyo milele kuwa CCM ndio Baba ndio Mama wa nchi hii, ni CCM pekee yenye kuweza kufanya uamuzi wa dhati wa hatma na mustakabali wa nchi.

CCM inakutana wiki hii mjini Dodoma kufanya maamuzi ya hatma ya nchi, kuamua nani anakuja kuwa mrithi wa Jakaya, nani anakuwa Rais wa awamu ya tano, maana ukweli ni kuwa mgombea wa CCM ndio Rais wa Tanzania kwani hakuna Chama wala kikundi cha walafi kinachoweza kutoa Rais ama chenye uhakika wa kupata hata wabunge 20 katika uchaguzi wa 2015.

Wananchi, vyombo vyote vya habari na vyama vya siasa wooote masikio yao yameelekezwa Dodoma kusikiliza nini CCM inataka kuamua, ndio ni kwa sababu CCM ndio baba wa Taifa hili na maamuzi ya baba ni maamuzi ya Familia nzima, CCM ikiamua Taifa limeamua.
 
Kauli yako inaonyesha udikteta uliokubuhu,japo ndiyo ukweli,kwani roho nyingi zimeteketea kwa ajili ya ccm kuingangania ikulu,kuwanyamazisha,wote wanaokosoa maamuzi ya kishetani yanayofanywa na ccm,,ndiyo,maamuzi ya ccm lazima yafuatwe,kwani kuyapinga ni kujitafutia kifo,ulemavu,au hukumu nyingine yoyote ya kikatili, towaonee huruma albino wetu.
 
JULIANA unajua umewambia ukweli waofuasi wao na wao hataki ukweli na hata wakubwa wao wanajua hilo kuwa CCM inawenyewe pamoja na mimi wewe na hao wasema hovyo.
 
Juliana Shonza

Kwani mpaka sasa hivi bado huna habari kuwa mwaka huu ni kinyume chake masikio ya wananchi na wandishi wa habari yameelekezwa Dodoma kusikilizia kifo cha CCM na wandishi wa habari wametega kamera zao kupiga picha kaburi la CCM.

Mwaka huu CCM inakwenda Dodoma kujikaanga kwa mafuta yake yenyewe,inakwenda Dodoma kujichimbia kaburi yenyewe,na ina kwenda Dodoma kujizika yenyewe.
 
Last edited by a moderator:
mnaona watu waliobobea kuelezea kitu mpaka kinasisimua
wale wa chadema (ccc)chadema cha chakavu wanaishia kusema hovyo wamepagawa
 
JULIANA unajua umewambia ukweli waofuasi wao na wao hataki ukweli na hata wakubwa wao wanajua hilo kuwa CCM inawenyewe pamoja na mimi wewe na hao wasema hovyo

Ni kweli CCM ina wenyewe wengine ni wadandiaji ambao mtaishia kufa kwa kugongwa kama wadandia trein.
 
Juliana Shonza

Laiti ungejua huku mtaani palivyobadilika usingesema hivyo

Laiti ungejua kuwa mtu anayeonekana ni CCM anatazamwa vipi mtaani usingesema hivyo.

Laiti ungejua kuwa huu ni mwaka 2015 na sio 2004 usingeropoka hivyo

Hata hivyo...kwa minajili ya kujifariji unaruhusiwa kuongea chochote

My dear...Times have changed.....Things are no longer at ease
 
Last edited by a moderator:
Eti itabaki hivyo milele, au ulikusudia kuandika itabaka hivyo milele, maana nasikia ccm ni wabakaji wa demo kras ia.
 
Heheheheee siasa mchezo umebakia kufanya siasa kwenye jf na fb jukwaani huonekani,ure finnished cdm ndio iliyokubeba toka umeenda kwa chama cha maficcm kwishney hta kualikwa kwenye mkutano wa mtaa hawakutaki utaishia humuhumu tu jf kupiga siasa hahahahahahaaaa....
 
Ni mtazamo mzuri sana wenye ukweli ndani yake siku sasa zinahesabika za kupata mrithi wa jk.

Sio vibaya kwa watu kujipa matumaini lakini hakuna mwanachama wa ccm akijuae chama hicho kama mwenyekiti wake, na ni huyo huyo aliyewatahadhalisha wanachama wake kuwa wajiandae kisaikolojia!!! NYANI ANAPOZIDI KUPANDA MTI NDIO MATAKO YAKE YANAPOZIDI KUONEKANA. Mwaka huu mtaumbuka!!
 
Kama alivyosema Mzee Mkapa katika moja ya hotuba yake makini aliyoitoa mwishoni mwa miaka ya 2004 ambayo imenukuliwa katika vyombo mbalimbali vya habari na katika jarida la Mzalendo la Chama Cha Mapinduzi, kuwa CCM ikipiga chafya wengine wote wanapata homa"

Ukweli huo umebaki hivyo na utabaki hivyo milele kuwa CCM ndio Baba ndio Mama wa nchi hii, ni CCM pekee yenye kuweza kufanya uamuzi wa dhati wa hatma na mustakabali wa nchi.

CCM inakutana wiki hii mjini Dodoma kufanya maamuzi ya hatma ya nchi, kuamua nani anakuja kuwa mrithi wa Jakaya, nani anakuwa Rais wa awamu ya tano, maana ukweli ni kuwa mgombea wa CCM ndio Rais wa Tanzania kwani hakuna Chama wala kikundi cha walafi kinachoweza kutoa Rais ama chenye uhakika wa kupata hata wabunge 20 katika uchaguzi wa 2015.

Wananchi, vyombo vyote vya habari na vyama vya siasa wooote masikio yao yameelekezwa Dodoma kusikiliza nini CCM inataka kuamua, ndio ni kwa sababu CCM ndio baba wa Taifa hili na maamuzi ya baba ni maamuzi ya Familia nzima, CCM ikiamua Taifa limeamua.

View attachment 252853
 
Haya mawazo ya kubaki milele ndio yatakayo watokea puani mwakahuu.
Kwamawazoyenu hayo ya kuwa mtaongoza nchi hii milele ndio katika mawazo hayo mnafanya dharau ya kila aina katika taifa hili, kwakufanya kazi kwa mazoea kwa mawazo hayohayo ya kubaki milele.
Na october tuta wahukumu kwa mawazoyenu hayo hayo ya kubaki milele.

Kwakuwa kwa mawazo hayo yakubaki milele ndio mnasahau wajibuwenu kwa wana nchi, na mnabaki katika mawazo yakudhani kwamba watanzania bado ni wadhaifu wa kutambua mabaya na mazuri katika chama hicho unacho kiita cha milele.

Milele yenu imesha fika mwisho, "October" !.
 
Back
Top Bottom