Hatma ya Makamba CCM kujulikana leo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hatma ya Makamba CCM kujulikana leo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Apr 9, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Apr 9, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Saturday, 09 April 2011

  HATMA ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusuf Makamba inatarajiwa kujulikana kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho kinachoanza leo.

  Kikao hicho kinaanza asubuhi hii mjini hapa, huku kukiwa na taarifa kuwa sekretarieti yake huenda ikavunjwa.

  Taarifa kutoka vyanzo mbalimbali vya ndani ya CCM, zinadai kuwa uamuzi huo unachukuliwa ikiwa ni hatua ya chama hicho kujivua gamba linaloonekana kuchuja mbele ya umma.


  Chanzo chetu cha habari kilidai kuwa, baada ya kuvunjwa sekretarieti, Makamba ambaye ndiye mwenyekiti wa sekretarieti hiyo, atawasilisha taarifa ya kuomba kustaafu.Hatua hiyo inamwezesha Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kuteua sekretarieti nyingine ambayo itakiongoza hadi mkutano mkuu unatarajiwa kufanyika mwakani.


  Makamba amekuwa akituhumiwa kusababisha chama hicho kufanya vibaya kwenye Uchaguzi Mkuu uliopita.


  Anatuhumiwa kutoa kadi kwa baadhi ya wagombea wa chama hicho ambazo zilitumika kuingiza wanachama mamluki na kuruhusu kila mwanachama wa CCM kupiga kura ya maoni.


  Halmashauri kuu ilikuwa imeagiza kura za maoni ndani ya chama hicho zihuhusishe wanachama hai, lakini aliagiza kila mwanachama kushiriki bila kujali kama ni hai au hajalipia kadi yake.


  Kulingana na kanuni za chama hicho, iwapo sekretarieti hiyo itavunjwa, licha ya Makamba watakaopoteza nafasi zao ni Naibu Makatibu wakuu CCM bara na Zanzibar, George Mkuchika na Saleh Ramadhan Ferouz, Katibu wa Itikadi na Uenezi, John Chiligati; Katibu wa Mipango, Kidawa Saleh na Katibu wa Kitengo cha Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.


  Wanaotajwa kuchukua nafasi ya Makamba ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi na Waziri wa Habari, Ajira, Utamaduni na Michezo, Dk Emmanuel Nchimbi huku ikidaiwa kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Abdulrahman Kinana amekataa nafasi hiyo. Mwingine anayetajwa ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Stephen Wassira lakini inadaiwa kuwa kasoro inayomkumba ni pale alipokihama chama hicho na kwenda NCCR-Mageuzi.


  Akipokea wanachama wapya kutoka Chadema jana, Rais Kikwete alisema kikao hicho ni muhimu kwa chama chao huku akiwaomba radhi wanachama kwa matokeo ya Uchaguzi Mkuu na kuwataka wasahau yaliyopita, wagange yajayo.

  "Tunaanza vikao muhimu vya kujenga chama chetu," alisema Rais Kikwete.Wanachama wapya waliojiunga na CCM ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Mbeya, Shambwele Shitambala na Katibu Mwenezi wa Chadema Wilaya Ileje, Henry Sayuni.Rais Kikwete alisema Tanzania ina vyama vingi, lakini ukweli utabaki kuwa CCM ndicho makini huku akisema vingine siyo vyama, bali mkusanyiko wa wanaharakati.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Apr 9, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,592
  Trophy Points: 280
  ‘Kamati Kuu CCM kujivua gamba'

  na Martin Malera, Dodoma

  KIKAO cha Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC), kinafanyika leo mjini Dodoma, huku kukiwa na uvumi kuwa huenda kukatokea mabadiliko makubwa kwa wajumbe wa sekretarieti ya chama hicho.

  Miongoni mwa mabadiliko yanayoweza kutokea ni kuondolewa kwa Katibu Mkuu wa CCM, Luteni Yusuf Makamba, Mhazini Mkuu, Ammos Makalla, Katibu wa Itikadi na Uenezi, John Chiligati, Naibu Katibu Mkuu Bara, George Mkuchika, Bernad Membe, Kidawa Hamid Salehe na Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Ramadhani Feroz.

  Uchunguzi uliofanywa na Tanzania Daima kwa wiki moja sasa tangu kuanza kwa mkutano wa tatu wa Bunge mjini hapa, umebaini kuwa mazungumzo ya baadhi ya wabunge ambao ni wajumbe wa NEC, ni kutaka Mwenyekiti wa CCM taifa, Rais Jakaya Kikwete, aisafishe sekretarieti na viongozi wengine kama hatua ya kujivua gamba.

  Wakati wakitaka baadhi ya wajumbe wa sekretarieti watimuliwe, wanachama hao wa CCM wamekuwa wakitaja majina ya watu wanaodhani wanafaa kuchukua nafasi hiyo.

  Duru za siasa kutoka ndani ya chama hicho Dodoma, zinawataja mtu kama Abdulhaman Kinana na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Emmanuel Nchimbi kuwa ndio wanaofaa kushika nafasi ya Makamba.

  Baadhi ya wajumbe wa NEC wapo mjini hapa kwa zaidi ya wiki moja, wakidaiwa kupanga mikakati ya kupitisha hoja zao na kutoleana uvivu, hasa kwa wanachama wa CCM wenye mahusiano mabaya kiasi cha kushindwa kusalimiana.

  Hadi sasa ajenda za kikao hicho zinatajwa kuwa ni tathmini ya uchaguzi mkuu kuanzia hatua ya kura za maoni, uteuzi hadi uchaguzi mkuu na ajenda inayohusu hali ya kisiasa nje na ndani ya chama na mengineyo kama mwenyekiti ataruhusu hoja hiyo.

  Mmoja wa wabunge maarufu na mjumbe wa NEC, aliliambia gazeti hili kwamba kikao hicho kilichosubiriwa kwa hamu, lazima kifanye maamuzi mazito yakiwemo kuivunja au kuwatimua baadhi ya wajumbe wa Sekretarieti.

  "Kama kweli tunataka kuanza upya, lazima NEC ifanye maamuzi magumu ikiwemo kuwatimua baadhi ya watendaji ndani ya chama na hata wengine kuwapoka kadi yetu, vinginevyo tunajidang'anya," alisema mbunge huyo.

  Tayari Kamati ya Maadili na Kamati Kuu (CC), imemaliza vikao vyake jana ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya NEC inayotarajiwa kukutana leo na kesho katika ukumbi maarufu wa White House mjini hapa.

  Kwa muda mrefu sasa, CCM imekuwa katika wakati mgumu kutokana na malumbano ya wenyewe kwa wenyewe yaliyodumu kwa muda mrefu na yaliyopata kuundiwa tume bila mafanikio.

  Malumbano ya hivi karibuni, yalihusisha Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM), dhidi ya viongozi wastaafu akiwemo Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa na Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Samuel Sitta.

  Mbali ya malumbano ya wenyewe kwa wenyewe, chama hicho pia kimekuwa kikiandamwa na tuhuma za ufisadi hasa kwa baadhi ya wajumbe wake ambao ni wajumbe wa Kamati Kuu (CC) na Halmashauri Kuu (NEC).

  Wapo wanachama wanaoamini kuwa suluhu ya kuondokana na hali hiyo ni kuwavua uongozi makada hao na kuwaacha na ubunge ambao umetokana na ridhaa ya wananchi wa majimbo yao.

  Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Shambwe Shitambala na Katibu Mwenezi wa Wilaya ya Ileje, Henry Kayuni, wamejiunga na CCM mjini hapa.

  Hafla ya kuwakabidhi kadi wanachama hao iliyohudhuriwa na wabunge wote wa CCM, ilifanyika katika viwanja vya ukumbi wa White House mjini hapa na walikabidhiwa na Mwenyekiti wa CCM taifa, Rais Jakaya Kikwete.

  Akizungumza baada ya kukabidhiwa kadi, Shitambala ambaye amepata kusimamishwa uongozi na CHADEMA, alisema kuwa amefurahi kurudi CCM kwani ni chama kikubwa na kuahidi atakuwa mwanachama mwaminifu kwa chama chake.

  Kwa upande wake, Rais Kikwete alisema kuwa kuna vyama vingi vya siasa nchini, lakini vingine ni mkusanyiko wa wanaharakati.

  "Yaliyopita si ndwele, tugange yajayo, Nashangaa kuna wabunge wa baadhi ya vyama, hata baada ya kuwa wabunge, lakini bado silka zao bado ni za kiwana harakati. Chama imara ni CCM," alisema kwa kifupi Kikwete.
   
 3. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #3
  Apr 9, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,592
  Trophy Points: 280
  kazi ya kujivua gamba na JK yupo madarakani ni kichekesho.................................
   
 4. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #4
  Apr 9, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,592
  Trophy Points: 280
  Kutimuana hakutaondoa migogoro bali itakuwa ni petorli ya kuchochea mpasuko...........................CCM inachohitaji ni katiba mpya inayowamilikisha wanachama chama chao badala ya huu utaratibu wa viongozi kukinadi chama kwa wafanyabiashara wakubwa wakubwa...................
   
 5. K

  KWELIMT Member

  #5
  Apr 9, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 89
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mmmh, mi sidhani kama kuitimua sekretarie itasaidia kurejesha hali ya maelewano,issue ya msingi ni kuua makundi yote ndani ya ccm. SURUALI CHAFU ITATAKATA KWA KUONDOA MIFUKO YAKE?

  Ili CCM iweze kurejesha imani kwa watanzania hawana budi kufanya maamuzi magumu kuishinikiza serikali itimize wajibu wake kwa kuwachukulia hatua wezi wanaotafuna pesa zetu kila kukicha
  .
   
 6. dazu

  dazu JF-Expert Member

  #6
  Apr 9, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 365
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Wanaoenda ccm wakati huu walikua ni mapandikizi tu kwenye upinzani. Ccm haijawahi kuwa mbovu ktk historia yake kama sasa, iweje mtu atoke chama makini kama cdm aende ccm? Na katibu mkuu wakimweka Nchimbi watakua wameruka mkojo na kukanyaga kinyesi.
   
 7. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #7
  Apr 9, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Sisiemu na kujivua gamba.... wanaelekea kufa sasa!!!!
   
 8. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #8
  Apr 9, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Wakuu leo kinafanyika kikao cha halmashauri kuu ya CCM mjini Dodoma miongoni mwa mambo yanayotarajiwa ni kuvunjwa kwa sekretariati ya CCM taifa ambayo mwenyekiti wake ni Mzee Makamba.Mheshimiwa Makamba ni katibu mkuu wa CCM chini ya uongozi wake mpasuko mkubwa ndani ya chama hicho umezidi kuongezeka kuliko wakati mwingine tangu kuanzishwa kwa CCM mwaka 1977.


  Mwenyekiti wa CCM Rais J Kikwete atalazimika kutangaza jina la katibu mkuu mpya na sekretariate mpya ndani ya kikao cha halmashauri kama hatua ya CCM kujivua gamba hasa baada ya Watanzania wengi kukatishwa tamaa na mwenendo wa CCM kukumbatia wala rushwaa.
   
 9. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #9
  Apr 9, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  labda anaweza kuwa SHITAMBALA SAMBWE! HUWEZI JUA ccm wamechanganyikiwa kweli!
   
 10. D

  DEKAKA Member

  #10
  Apr 9, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kikwete asemapo ccm ndiyo chama tu, vingine ni wanaharakati tu' anasahau kuwa hata kutafuta uongozi kwa nguvu hata kuchakachua ni harakati pia. Hivyo wakati wa ccm unakwisha sasa tunaelekea kuwamwaga
   
 11. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #11
  Apr 9, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,585
  Likes Received: 4,693
  Trophy Points: 280
  JK ndiye mlezi wa ufisadi woooooooooote unaoitafuna nchi hii, hivyo ni ndoto kwa CCM kujivua gamba, labda ****** ang'atuke kwanza.
   
 12. NAHUJA

  NAHUJA JF-Expert Member

  #12
  Apr 9, 2011
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 15,054
  Likes Received: 15,648
  Trophy Points: 280
  kweli sisiem wamekwisha maana hata ile ya kukusanya watoto karimjee ili wajaze viti wakubwa wakose kuchangia imeleta picha mbaya
   
 13. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #13
  Apr 9, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  hahaa JK yaani CCM ni sawa na gari linatakiwa kubadilishwa injini sio kubadilisha oil
   
 14. JIULIZE KWANZA

  JIULIZE KWANZA JF-Expert Member

  #14
  Apr 9, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 2,573
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Gamba la kwanza JK Akabidhi nchi kwa jeshi, tuandike katiba na uchaguzi mpya ilo ndo gamba la kujivua
   
 15. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #15
  Apr 9, 2011
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Kumtoa Makamba uongozini ni sawa na kutoa ndoo moja ya maji toka Baharini, kama kweli wanataka CCM irudi kuwa chama cha wakulima na wafanyakazi wa Tz njia na nafasi wanayo kama tu watapenda iwe hivyo
   
 16. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #16
  Apr 9, 2011
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Hivi mkosaji akitubu madhambi yake Kanisa litamkataa? CCM inwahitaji wanachama wake wote na kama kuna waliopoteza mvuto hada waliowakosesha kura mwaka jana basi watafute makada wengine watakovutia kundi la vijana.
   
 17. M

  Maimai Senior Member

  #17
  Apr 9, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 174
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  we do not give a damn kwanza kikabu chenyewe kimechoka nadhani kinasubiri mpaka mwanaye mwamvita awe mkuu wa mkoa ama mbunge ndo ang,atuke. Vijitu vingine taabu sana vinajipendelea tu na familia zao.' kesho utasikia j.makamba waziri usishangae hata kidogo. Makamba hafai angebakia tanga tu awe katibu kata wa kata ya mkata aliyekataa kukata kata kwa kutumia kata... Hahaha yaani makamba hafai kabisa anawaponza ccm kwa ujinga wake. Nadhani imefiika muafaka wa chairman wa ccm asiwe raisi. Makamba chakachuaaaa. Mgosi unguna uchelewe kusoma alama za nyakati. Wilabeooooo kalungi
   
 18. Lighondi

  Lighondi JF-Expert Member

  #18
  Apr 9, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 585
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Wanaanza kuvuna waliyopanda!!!
  Walipanda majungu, ufisadi, ubaguzi.
  Mbegu zikaota na kuzaa wizi, makundi, dharau kwa wakongwe, ujuaji, upotoshaji wa makusudi, mifarakano, udanganyifu na wizi wa kutupwa.
  Sasa vimekomaa na viko tayari kuvunwa wanasingizia "eti jirani ndiye chanzo cha yote hayo"
  Tutaona na kusikia mengi zaidi ya haya.
  Tusubiri!!!!!!
   
 19. Kyalow

  Kyalow JF-Expert Member

  #19
  Apr 9, 2011
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 2,118
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  duuuh!!....ndugu yangu umekiua kibabu cha watu...nmecheka hadi basi.kinacho mponza elimu yake mgogoro yule(makamba)
   
 20. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #20
  Apr 9, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  HATMA ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusuf Makamba inatarajiwa kujulikana kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho kinachoanza leo. Kikao hicho kinaanza asubuhi hii mjini hapa, huku kukiwa na taarifa kuwa sekretarieti yake huenda ikavunjwa. Taarifa kutoka vyanzo mbalimbali vya ndani ya CCM, zinadai kuwa uamuzi huo unachukuliwa ikiwa ni hatua ya chama hicho kujivua gamba linaloonekana kuchuja mbele ya umma.

  Chanzo chetu cha habari kilidai kuwa, baada ya kuvunjwa sekretarieti, Makamba ambaye ndiye mwenyekiti wa sekretarieti hiyo, atawasilisha taarifa ya kuomba kustaafu. Hatua hiyo inamwezesha Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kuteua sekretarieti nyingine ambayo itakiongoza hadi mkutano mkuu unatarajiwa kufanyika mwakani.

  Zaidi: Hatma ya Makamba CCM kujulikana leo
   
Loading...