Hatma ya mafao ya wafanyakazi hatarini

B

bea

Senior Member
Joined
Oct 25, 2010
Messages
139
Points
225
B

bea

Senior Member
Joined Oct 25, 2010
139 225
Wadau mliopo kazini ambao bado mna imani na fedha za mafao mnazokatwa hali si nzuri.Mimi nimeshuhudia baadhi ya watu walioonyesha nia ya kuchukua mafao yao lakini kumekuwa na kuzungushwa sana na hawa psssf.Kifupi kuna tatizo kubwa na pesa za wafanyakazi.

Kuna jamaa mmoja mkataba wake uliisha toka mwaka jana mwezi wa 6 mfuko wa NSSF anadai kam 90 Million kila siku akienda anazungushwa hadi juzi ameugua kutokana na mawazo yanayo sababishwa na ukata.Wanamwambia pesa zako ni nyingi huwezi kupewa kwa mkupuo hata kumpa kidogo wanashindwa.

Haya mambo kwa waliopo kazini hawajajua na wanamatumaini na pesa zao.Kifupi leo nawaambia hali ya fedha za hifadhi ya jamii sio salama kutokana na kusuasua malipo.Fanyeni kautafiti kutembelea ofisi za hii mifuko mtakuta watu wanavyoangua vilio.

Nafikiri hizi pesa baada ya single account kuanzishwa na serikali ndo inajitapaga kuzitumia kwa madai hii nchi ina pesa.Kwa hiyo jiandaeni.Najua wahanga mpo wengi anzeni kufatilia
 

Forum statistics

Threads 1,336,567
Members 512,648
Posts 32,543,498
Top